Baasi punguza kulialia tutamchapa aliyekukanyaga ati! Basiiii nyamaza mtoto waache wakulima wajadiri mambo ya korosho.Kila mtu aliona wizi tena wa kishamba kabisa wa kura ulivyofanyika, swala la mahakamani labda uchaguzi ungefanyika leo lakini kwa wakati ule mahakama ilikuwa imeminywa na haikuwa huru kabisa.
Kwa taarifa yako Jiwe ndio ameipa korosho thamani. Labda ukisema kuharibu korosho ni jiwe naweza kukubaliana na wewe sababu wakati Jiwe anaingia common price ya korosho ilikuwa 1700 tu bei ya juu..alipoingia ikaenda 4200. Kuanzia hapo wakulima wakashtuka kuwa kumbe inawezekana. Kama uliisikia wakulima wa korosho walikuwa wananywesha soda mbuzi kwa kushangilia bei.Dah, yaani jamaa anabwabwaja sjui hata mti wa korosho kama anaujua, shortly aliyeharibu zao biashara ya korosho ni JPM a.k.a JIWe
Sio kweli. Ishu ya shamba ilijitokeza mara moja tu wakati wa kampeni ya kuzuia kangomba. Hata hivyo badae iliendelea. Mimi ni mnufaika mmojwapo wa kangomba kwa mwaka jana.Jaribu kuwa na kumbukumbu kidogo, tozo zimeongezwa, sasahivi imeongezeka sh 40 kwa kila kilo, enzi za JPM utaratibu wa ununuzi haukuwa mzuri, mpaka uonyeshe shamba la korosho, likaguliwe ndo utauza, haikukaa vema sana
Baada ya bei kupanda akaona donge akaharibu biashara yenyewe yote alianza kwa kuwadhulumu korosho zao na baadae bei ikashuka kuliko aliyoikuta,usimtetea muharibifu na dhulumati.Kwa taarifa yako Jiwe ndio ameipa korosho thamani. Labda ukisema kuharibu korosho ni jiwe naweza kukubaliana na wewe sababu wakati Jiwe anaingia common price ya korosho ilikuwa 1700 tu bei ya juu..alipoingia ikaenda 4200. Kuanzia hapo wakulima wakashtuka kuwa kumbe inawezekana. Kama uliisikia wakulima wa korosho walikuwa wananywesha soda mbuzi kwa kushangilia bei.
Enzi hizo si shinyanga wala kigoma wanaijua korosho. Leo nenda shinyanga utakuta wanalima korosho. Huko kusini watu wanamiminika kulima korosho.
Soko huwa linatafutwa na linalindwa. Ukilivuruga, huwezi kuamka na kulipata tena maana siku zote wapo wanaotafuta masoko. Na hicho ndicho viongozi wengi wa serikali hawajui. Unakuta mara waziri mkuu anainuka na kusema, kuanzia leo marufuku kupeleka mahindi nje ya nchi, halafu baada ya muda utasikia, tumeruhusu mahindi kuuza nje! Hopeless kabisa. Watu wanahangaika kutafuta soko, unavuruga, halafu baadaye unasema eti wauze nje. Huko nje walikuwa wamekaa wanakusubiria wewe? Ukisikia hivyo, unakuwa huna shaka kuwa wajinga wamejikusanya, wapo huko serikalini kwaajili ya kuwaharibia wenye uelewa.Siasa imehusika vipi na kukosekana wanunuzi kwenye mnada??
Sasa ye ndio aliyeipandisha kwa kuondoa mtu kati kwa nini aone donge. Labda wewe usiojua kuwa hata kukodi shamba la korosho ilikuwa 100000 tu na watu hawakodi, wakati sasa hivi hata mill 2 mkulima hakupi shamba.Baada ya bei kupanda akaona donge akaharibu biashara yenyewe yote alianza kwa kuwadhulumu korosho zao na baadae bei ikashuka kuliko aliyoikuta,usimtetea muharibifu na dhulumati.
Hili ni gazeti la lini?Gazeti la Nipashe la leo limeripoti kwa masikitiko makubwa kuwa mnada wa korosho umesitishwa baada ya kampuni za wanunuzi kukosekana! .
Hii inatokea huku Nape Nnauye na Zito Kabwe waliojipambanua kama watetezi wa wakulima wa korosho na wakapiga kelele sana miaka yote mitano ya Serikali ya awamu ya tano wakiwa kimya kabisa kana kwamba hawajui kinachowatokea wakulima wa korosho mwaka huu.
Je, wakulima wa korosho watetewe na nani?
Nguvu ya Nape, Zitto, Membe kulisemea zao la korosho imeenda wapi?
View attachment 1994504
AsanteHili ni gazeti la lini?
Na huo mnada umefanyika wapi na ni lini? Kwa sababu leo ni Jumatatu na minada huwa inafanyika Ijumaa ya kila Wiki.
Mnada wa mwisho ulifanyika tarehe 29/10/2021 ambapo; Bei ya juu ilikuwa 2,170 na bei ya chini ni 2100/=
Hakuna Mwananchi alikuja kufurahia utekelezaji wa kauli za huyo JPM. Watu wamedhulumiwa korosho zao na waliolipwa wamelipwa kwa bei ya 2640 wakati yeye majukwaa i anatangaza 3500.Mbwembwe zote pamoja na kuondoa vikwazo na tozo kadhaa lakini wapi; mlimshambulia sana JPM alipoamua kununua ili wananchi wapate chochote, sasa hawa watawala wana la kusema kutokana na aibu hii?
Wanasiasa wabaya sana kuhusika kwenye ustawi wa biashara
Mnada wa juzi hayati JPM amezuiaje wanunuzi kuja?Hakuna Mwananchi alikuja kufurahia utekelezaji wa kauli za huyo JPM. Watu wamedhulumiwa korosho zao na waliolipwa wamelipwa kwa bei ya 2640 wakati yeye majukwaa i anatangaza 3500.
We ulikuwa hushangai kila siku alikuwa anatoa maagizo kwa BOT zitoke hela na bado wakulima walikuwa hawapati fedha zao? Jiwe na watu ndio wanajua yale mabilioni wameyapeleka wapi
Kumbe marehemu anaweza kuporomosha bei ya korosho?Maamuzi ya Magufuli yamechangia zaidi ya 80% kuharibu biashara ya Korosho hapa nchini.
Tangu afanye yale maamuzi ya ki-Jiwe bei ya Korosho imekuwa ikiporomoka siku hadi siku. Nakumbuka mwaka uliofuata baada ya Serikali kudhulumu wakulima, korosho bei ya Juu ilikuwa 2600 na sasa hivi bei ya imefika 2400.
Baada ya Magufuli kusema atanunua korosho kwa 3500 na badala yake akaanza kudhulumu kwa kuchukua korosho za watu ambapo alikuja kuwalipa Tzs 2640 na wengine kutokulipwa kabisa ndipo mambo yalipoanza kuharibika. Leo hii hakuna mkulima atakayekubali kuuza korosho zake kwa Serikali. Never.
Magufuli alipayuka majukwaani na kusema atafufua viwanda, ila hakuna kiwanda cha Korosho kimefulfuliwa chini ya Utawala wake na hakuna korosho ilibanguliwa.
Ila wakulima wa Korosho walishamlilia MUNGU wao na kumuachia yeye kwani yeye ni Alfa na Omega.
Magufuli ana gundu ameitia nuksi hii nchi kila alikopita ameharibuSiasa imehusika vipi na kukosekana wanunuzi kwenye mnada??
Msitoe visingizio kwa mtu ambaye hayupo mbona wakati yupo hukubwatuka hivi!!!Mwendazake amezuia wanunuzi?
Mbona mwaka jana wanunuzi walikuja?