Sababu ni 2 tu; either fundi alikosea kuweka helbow au maji hayatoshi kusafisha KIMBA lote lililotupiwa humo shimoni. Kama kuna blockage kwenye helbow then uchafu utakua unakwenda kidogo sana kwa kila flashing 1. Nakushauri, tafuta fundi tindua hicho choo then fanya inspection upya. Blockage sometimes hutokea hivi; wakati ume set choo (hasa hivi vya kuchuchumaa ) labda ilifanyika kabla hujaweka jamvi au marumaru, so wakati sasa unaweka jamvi (choo kikiwa tayari kimefungwa ) kuna madongo ya cement yanaingia ndani ya choo, kwasababu ya ubize wa fundi huaga analazimisha kumwaga maji, kinachotokea yale madongo yanashindwa kupanda ule mkunjo wa helbow then yana settle pale katikati, baada ya muda fulani lile dongo linakua kama JIWE and hence litaanza kuzuia kinyesi kisipite kwenda shimoni. Just uzoefu wangu katika kujenga jenga nyumba nilikowahi kufanya cause hili liliwahi kunikuta kwenye kibanda changu nilichoa anzia maisha.