Mnadhibiti vipi harufu ya "nnya" isitapakae hapo sebuleni?

Mnadhibiti vipi harufu ya "nnya" isitapakae hapo sebuleni?

Dah! Ukute kimba la mnywa komoni au bia kwa sana.kuna harufu hazivumiliki aisee.

Air freshner inasaidia kidogo,chumba cha choo kuwe kikubwa na dirisha kubwa la kuingiza hewa safi.

Shimo la choo lisiwe mbali na chemba,mfumo wa kusafirisha maji taka ..fundi bomba auweke vizuri kuzuia harufu kurudi ndani.

Shimo pamoja na chemba viwe na bomba la kutolea hewa ( kupumua).

Angalau utapunguza tatizo.
Choo chako hakina snorkel za kupumua nje au ndio umeweka ventilation ndogo sana kama kidirisha cha kununulia luku!
 
Asante aisee. Kuna jambo huwa linanifikirisha kidogo. Ile harufu haitoki chembani. Yani nionavyo, ni kimba fresh kabisa vile mtu kamaliza akitoka tu, balaa. Pengine hiyo size na madirisha makubwa yaweza saidia. Asante sana ndugu

Asante sana
Kuna masela wanaachiaga makimba size ya matoke 😂 unakuta ngoma inaelea imegoma kupelekwa na gharika ya cistern
 
Sababu ni 2 tu; either fundi alikosea kuweka helbow au maji hayatoshi kusafisha KIMBA lote lililotupiwa humo shimoni. Kama kuna blockage kwenye helbow then uchafu utakua unakwenda kidogo sana kwa kila flashing 1. Nakushauri, tafuta fundi tindua hicho choo then fanya inspection upya. Blockage sometimes hutokea hivi; wakati ume set choo (hasa hivi vya kuchuchumaa ) labda ilifanyika kabla hujaweka jamvi au marumaru, so wakati sasa unaweka jamvi (choo kikiwa tayari kimefungwa ) kuna madongo ya cement yanaingia ndani ya choo, kwasababu ya ubize wa fundi huaga analazimisha kumwaga maji, kinachotokea yale madongo yanashindwa kupanda ule mkunjo wa helbow then yana settle pale katikati, baada ya muda fulani lile dongo linakua kama JIWE and hence litaanza kuzuia kinyesi kisipite kwenda shimoni. Just uzoefu wangu katika kujenga jenga nyumba nilikowahi kufanya cause hili liliwahi kunikuta kwenye kibanda changu nilichoa anzia maisha.
Hili tatizo lipo kwangu aisee. Helbow ya chumbani imepishana kidogo. Sasa hivi natumia hichi choo kwa ajili ya kuogea na haja ndogo tu
 
Ninaomba ushauri. Nimechunguza nyumba zetu nyingi zina shida sana ya harufu toka msalani mtu akipiga tukio kubwa. Bora huko vyumbani mtapambana na hali zenu, hiki cha wote jirani na sebule ni changamoto jamani.

Ukute una wageni kisha mtu akaenda kutupia, kisha ukute ni wale watu "nya" inanuka kama wamemeza nyoka ni balaa. Mimi huwa ninaona aibu sana.

Hivi shida ni ufundi ama ndo ipo hivyo, lazima mchezee harufu mpaka mkome? Wenzetu mmefanyeje hadi hamteseki? Msaada tafadhali.
Shida huanza na designing ya nyumba wakati wa ujenzi. Choo ni sehemu very private ambayo unatakiwa uiseti katika kona very private kwenye nyumba au eneo la nje ya nyumba.

Kuna nyumba unakuta mlango wa choo upo open eneo la sebuleni mtu anakuona ukiingia na kutoka kwann kikitokea kizungumkuti huko ndani habari zisifike sebuleni na kuleta fedheha kubwa¹.1111
 
Dah! Ukute kimba la mnywa komoni au bia kwa sana.kuna harufu hazivumiliki aisee.

Air freshner inasaidia kidogo,chumba cha choo kuwe kikubwa na dirisha kubwa la kuingiza hewa safi.

Shimo la choo lisiwe mbali na chemba,mfumo wa kusafirisha maji taka ..fundi bomba auweke vizuri kuzuia harufu kurudi ndani.

Shimo pamoja na chemba viwe na bomba la kutolea hewa ( kupumua).

Angalau utapunguza tatizo.
Mara nyingi choo cha mtu kikiwa na harufu kali huwa ni changamoto inayoitwa constipation. Choo kimekaa muda mrefu kwenye mfumo wa kutoa taka mwili so kikitoka Babu hiyo smell yake mzoga unasubiria.....
 
mkuu ndo maana tunashauriwa kabla ya kununua ramani mitaani na kuanza ujenzi, mchukue mchora ramani mpeleke kwny kiwanja moja ya vitu atakavyoviangalia ni jua linachomoza na kuzama wapi, lengo ni kujua mpangilio wa vyumba, sebule na vyoo vikaaje ili kuepusha icho ulicho kisema pamoja na hali ya joto na baridi ktk nyakati tofauti za kila siku. Ukinunua ramani kienyeji inaweza isiendane na mazingira ya kiwanja chako mfano choo kuwepo kunakotokea upepo harufu yote itaishia sebuleni na vyumbani iyo nyumba itakua kero maisha yake yote.
Choo kuna namna ya kukiset katika upande wa nyumba ambao watu hawawezi jua nani anafanya yake au hata kusikia mizinga 21 ikiwa inapigwa kutoa heshima kwa wageni wa waalikwa.

Cha msingi wakati wa kusanifu jengo ni vema kila chumba kiwekwe kwa minajiri ya future desires na matarajio. Sio umemaliza ndipo uanze kutathimini sasa ubora.
 
Hiyo Utrap ni muhimu sana wala si tatizo katika mfumo wa choo cha ndani.

Shida ni location ya choo kwenye nyumba lakini pia mtumiaji nae umakini wake.....

Unatakiwa unaposhusha mzigo unazindikiza salamu zako na kopo moja la maji ili mzigo ushuke.
 
Kwa uzoefu wangu, harufu ya nya' wakati na baada ya kujisaidia utaikata vizuri tu kama..

1. Dirisha la chooni litakuwa wazi(fungua vioo) wakati unajisaidia
2. Kisha ukimaliza kujisaidia tupia sabuni hata ya unga kwenye sinki na shimo kisha umwage maji mengi/flash. Nakuhakikishia utatoka chooni na harufu imeshakata tayari
Kuna sabuni ya kuoshea choo ninatumia hakuna mtu amekuja akakosa isifia. Unamwaga tone kidogo balaa lake inapambana na harufu kama vile polisi inavyopambana na Chadema.
 
Asante aisee. Kuna jambo huwa linanifikirisha kidogo. Ile harufu haitoki chembani. Yani nionavyo, ni kimba fresh kabisa vile mtu kamaliza akitoka tu, balaa. Pengine hiyo size na madirisha makubwa yaweza saidia. Asante sana ndugu

Asante sana
Kuna watu wakiwa constipated ni mtihani. Akishusha mzigo balaa lake linaweza kudumu siku nzima.

Shida watu mboga za majani na matunda wanaonja badala ya kula. Maji na juice ni hadi wapewe ila hawatumii.
 
Kitoe kitu huku ukimimina maji kunako sink
Yaani kisiweke pause kunako sink kiende direct.
 
Tumia cha nje mana sometimes cha ndani n fedheha
Ndio maana wanasema ule ustaarabu wa choo cha nje still inabidi tuuendeleze kwasababu kwa wale wenyeji wenye nyumba ndogo, kusikia mizinga ni rahisi sana. Sasa ukiwa na choo cha nje inakuwa nafuu ingawa swala la usafi still lipo pale pale
 
Maisha yangu yote natumia choo cha ndani
hata kama fundi alitumia kanuni zote za ujenzi

Vitu hivi viwili kimoja kikikosekana na kimoja kikiwa hakifanyiki tegemea harufu mbaya

kama choo kilikosekana DIRISHA kubwa ambalo litakuwa linatoa na kuingiza hewa safi tegemea halufu kurudi sebureni
hii inatokana na kasumba ya choo kujengewa kidirisha tu kadogo n ukutwe kanafungwa muda wote
DIRISHA LA CHOONI linatakiwa liwe wazi muda wote sio linafungwa na vioo masaa 24

kusukuma kinyesi au hata mkojo na maji mengi
Nyumba niliyopanga sasa hivi haina mfumo wa kufrash mimi na familia yangu sheria ukikata GOGO lazima usukume na maji Ndoo ya lita 5 mpaka uhakikishe KINYESI chote kiondoke
hata akija mgeni si mstaarabu huwa naenda kufarsh mwenyewe au mkewangu najua wengine ustaarabu ZERO au mazoea ya vyoo vyao vya kulenga
Kuna mshikaji huwa haflush akishamaliza kutuma salam kwa watu watatu. Huwa ananikwaza sana nashindwa kumwambia sababu si swala la mtu mzima kutojua......

Unajua matumizi ya choo cha ndani yanahitaji usafi wa kiwango cha juu sana.
 
tumia sabuni za chooni zile za maji zina perfume kali sana, mtu akiingia chooni kabla ya kufanya chochote anamwaga kwanza kidogo chini na kuisambaza na maji kidogo akiwemo kwenye sink lenyewe na nje ya sink. kwa njia hii ata kimba liwe na harufu gani hutokaa usikie harufu.

Na ukishindwa hii ya sabuni basi wewe nunua air fresher iwe inapulizwa kabla na baada ya kuanza kupii .

solution mama kabisa ni ustaarabu ,hakikisha choo kina maji ya kutosha na kiflashiwe na maji ya kutosha ili kuhakikisha mzigo wote umetolewa nje.
 
Back
Top Bottom