Mnahangaika kuzungukazunguka bila ya sababu, zikeni maisha yaendelee

Mnahangaika kuzungukazunguka bila ya sababu, zikeni maisha yaendelee

Kati ya vitu vyenye utata duniani KIFO ni kimojawapo. Mpaka sasa duniani kuna mabishano juu ya uhai ni nini ili ikijulikana watu wazuie KIFO.

Na utata juu ya kifo umekuja kwa kuwa watu hawajui uhai ni nini. Je uhai ni pumzi, ubongo, moyo, au nini? Watu wa falsafa nao hawapo nyuma, wanadai uhai unaweza kuwa ni nafsi au roho.

Mtu akifa mwili wake hubakia, na maendeleo ya binadamu yamewezesha kuhifadhi miili ya marehemu. Mtu kafa lakini mwili upo. Jee mwili si sehemu ya uhai wa mwanadamu?

Kwa mtazamo wangu kumbe mwili huifadhi uhai lakini wenyewe si sehemu ya uhai. Mwili unaweza kuwepo lakini uhai usiwepo. Na hapo ndipo dhana ya mwili kuitwa mzoga inapoanzia.

Christopher Mtikila alishitakiwa kwa kuleta dhana ya mzoga wakati wa msiba wa Mwalimu Julius Nyerere. Na akafungwa mwaka mmoja.

Hapa Tanzania Kuna chama cha siasa kimekufa lakini wenye chama chao na wanandugu wa chama hicho, akili zao hazikubali kuwa wanaishi na chama mfu!

Wanazunguka kila mahali kutafuta jinsi ya kukifufua lakini mfu ni mfu tu. Badala ya kuzunguka zunguka na kutangatanga, wakubali kuwa chama chao kimekufa wakizike ili maisha mengine yaendelee.

Na ajabu watu wengine wanapata madhara kwa kuteswa na kudhalilishwa kisa wanasema ukweli kuwa chama hicho kimekufa. Kutesa wengine ndiko kutakakobadili ukweli kuwa chama chenu kimekufa?

Zikeni ili maisha mengine yaendelee!
Oktober itatoa majibu.
 
Sawa!

Wenye msiba wao wanajijua! Wengine wanatamani wafanye "Cryonics" lakini wanagundua muda haupo upande wao!

Wazike tu. Au kama wanaweza waigeuze maiti yao mzukule!
Kwahiyo kwakua tumezuiwa kufanya siasa na tunakosa watu kwenye mikutano basi CHADEMA imekufa? Bado tupo sana
 
Kifupi CCM Ife maisha yaendelee, TANZANIA ipone.

Binafsi naamini CCM ni jina tu, ila CCM inaendeshwa na watu, watu wale wale walioko CCM leo hii wakihamia CDM wote na CDM ikashika Dola mambo yatakuwa yale yale.

Lakini pia siku ikitokea CCM ikatekwa na watu wema na waliopo wote wakatoka naamini kupitia CCM hiyo hiyo mambo yanaweza kubadirika.
CCM ife, waingie watu wenye nia thabiti ya kuweka misingi na mifumo imara ya kuongoza nchi. Tunatembea na Katiba mfu, mifumo ipo corrupt sana, imeoza.

Tunahitaji mambo mengi yawe overhauled, baada ya hapo tuendelee kuitengeneza nchi. Huwezi kuishi nchi ambayo Rais ni kila kitu, anateua kila mtu, anatengua anavyojisikia. Raisi ambaye ni mgombea anateua Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, umeona wapi hii. Wateule wa raisi hawawi responsible kwa yoyote zaidi ya raisi, hawawezi hata kuitwa bungeni kuhojiwa kwa kukiuka sheria.

We need reforms going forward, without reforms tena kubwa hatutafika.
 
Mtu wao alishakufa, kinachosumbua sasa ni "Ghost CCM"

Hatuwezi kupambana na mzuka (ghost) kimwili. Hii inapaswa kupambana ktk ulimwengu wa kiroho kwa kutumia silaha za kiroho..

Askofu Josephat Gwajima ameshaanzisha vita. Lilishitiliwa kidogo, reaction yake ikawa very positive kuelekea machinjioni...

Na sisi twendeni vitani tuungane na Askofu Gwajima, CHADEMA ya Tundu Lissu. Ushindi uko wazi mno..!
 
Back
Top Bottom