Mnaipa asilimia ngapi hii ramani ya Bangaloo?

Hv lango kuu lipo wap
Screenshot_20230312-101351_Gallery.jpg

Lango lipo kwenye njano. Ila nitaliweka kwenye nyekundu. Ili njano iwe ni mlango mdogo wa mkulungwa kama hataki kupita sebureni
 
Oyaa Unazingua...
1. Mtu kwenda Study Room mpaka apite Master Bedroom?
2. Hakuna Privacy kati ya Public WC na Sitting room (Re-arrange hapo)
3. Bedroom close na Kitchen ipe dirisha la Pili kama unajenga Dar utanishukuru majira ya Joto
4. Sitting inapaswa iwe ventilated vya kutosha na natural light ya kumwaga. Mbona umeipendelea Dinning ambako watu hawakai sana? Unazingua
5. Pay attention to roof Plan - Hapo kwenye entrance hapo usione raha hiyo mistari mingi mingi kwenye kujenga haitakuwa hivyo
6. Arrangement ya jiko "U~ Shape" ni perfect
7. Mpe kazi Mtaalam adesign usichukue tu kwenye mtandao ukampa Fundi Samweli ajenge, utazingua zaidi
Fact
 
Niliona kama nyumba ya nje haiepukiki kwa ajili ya vijana na wageni wa kiume. Ukiungana na vyoo vya nje na stoo ya mazaga. Zaidi kwa ajili ya mpangaji huko mbeleni wa kunikimbiza hospitali nikizeeka
Bila shaka Wageni wa Kiume watakuwa ni Wanachama, Wapenzi, Mashabiki na Wachezaji wa Simba!
 
View attachment 2538313

Baada ya kuupima mziki wa ghorofa na kuona ni kina kirefu sasa nahamia rasmi kwenye mabangaloo aka Freemason.
Kuna floor plan ya huyo mwamba hapo. Naombeni maoni yenu na kukosoa kwingi kabla sijamchek
Hii hapana. Vyoo vya public vinasngalia sting room , ukijamba tu ni shida.
Hilo limzunguko kwenye sting room linamaliza space tu . Mwishoe wife agongane na wageni kwenye kona za korido.
 
Niliona kama nyumba ya nje haiepukiki kwa ajili ya vijana na wageni wa kiume. Ukiungana na vyoo vya nje na stoo ya mazaga. Zaidi kwa ajili ya mpangaji huko mbeleni wa kunikimbiza hospitali nikizeeka
Mkuu iliposimama nyumba kama hiyo uchanganye humo na nyumba za wapangaji?

Labda kama kutakuwa na option ya kutenganisha nyumba kwa nyumba na fence otherwise sishauri uwaze kuishi na mpangaji eneo lako.
 
Mkuu nadhani hukusoma vizuri ukaelewa. Nimesema ni kama ikilazimu. Fikiria huko uzeeni watu wakakukimbia. Ukabaki na mama na binti wa kazi, huko atakaa nani. Kwa nini usiweke hata single akatia joto nyumba?
 
View attachment 2538313

Baada ya kuupima mziki wa ghorofa na kuona ni kina kirefu sasa nahamia rasmi kwenye mabangaloo aka Freemason.
Kuna floor plan ya huyo mwamba hapo. Naombeni maoni yenu na kukosoa kwingi kabla sijamchek
Ramani inavutia kwa macho lakini ki uhalisia pia kiuchumi ni mbovu sana,

1.kuna haja gani ya kuweka ukuta na mtango dinning room?

2.kuna haja gani ya huo mlango katikati ya korido yani kazi yake ni nini hapo,

3.hiyo store mlango wake uwekwe jikoni iwe kitchen store,

4.pia kuna umuhimu wa dirisha kati ya jiko na dinning kuepusha kuzurula na mapoti koridoni

5.sitting room umeibana sana kwa ndani gharama ya ac inahusika kama unaishi dsm pia arrangement yamakochi kuzunguka meza na kublock TV site kaijakaa sawa

6. Pia sijaona sababu ya mtu kuingia koridoni kwanza ndio aingie sitting room tofauti na hayo design ni nzuri
 
Weka sawa basics:
1. Bathrooms ziwe na nafasi ya shower
2. Mimi si mpenzi wa macorridor kibao. Inawezekana kuondoa hizo corridors na kubadili entry za vyumbani ili Kuta za vyumba ndizo ziwe za living room
3. Bedrooms zizingatie makabati ya nguo, meza za watoto kusomea, nk. Kwa zilivyochorwa sasa inaonekana Bado hazijafikiriwa practically
4. Kitchen inahitaji kudesigniwa vizuri pia. Fridge isikae dining room.

Mengine ni kama walivyoshauri wengine (kitchen store, study room, nk)

Ps. Hiyo entry way siyo mbaya ikibaki hapo ila iongeze ukubwa na tengeneza foyer hata ndogo tu. Na weka mlango wa study Kwa upande huo wanao au wageni waweze kupata ukawahidumia bila wao kuingia chumbani kwako.

Kama ni shamba, hapo jikoni/ store area angalia uwezekano wa kupata mud room.
 
1. Upo sahihi
2. Sijakuelewa, unaweza ku screen shot?
3. Upo sahihi
4. Upo sahihi
5. Nitaweka dirisha kubwa hapo kushoto. 6.Mlango utakuwa hapo kwenye sofa kubwa
 
Hii hapana. Vyoo vya public vinasngalia sting room , ukijamba tu ni shida.
Hilo limzunguko kwenye sting room linamaliza space tu . Mwishoe wife agongane na wageni kwenye kona za korido.
1.Hiyo public toilet haitokuwepo. Itakuwa toilet ya room ya kulia
2. Kwenye mzunguko kuna kona za kuficha milango ya vyumba na ukuta wa TV. Huo ukuta wa dinning utatoka
 
Weka sawa basics:
1. Bathrooms ziwe na nafasi ya shower
2. Mimi si mpenzi wa macorridor kibao. Inawezekana kuondoa hizo corridors na kubadili entry za vyumbani ili Kuta za vyumba ndizo ziwe za living room
3. Bedrooms zizingatie makabati ya nguo, meza za watoto kusomea, nk. Kwa zilivyochorwa sasa inaonekana Bado hazijafikiriwa practically
4. Kitchen inahitaji kudesigniwa vizuri pia. Fridge isikae dining room.

Mengine ni kama walivyoshauri wengine (kitchen store, study room, nk)

Ps. Hiyo entry way siyo mbaya ikibaki hapo ila iongeze ukubwa na tengeneza foyer hata ndogo tu. Na weka mlango wa study Kwa upande huo wanao au wageni waweze kupata ukawahidumia bila wao kuingia chumbani kwako.

Kama ni shamba, hapo jikoni/ store area angalia uwezekano wa kupata mud room.
1. Bila shaka
2. Naomba mapendekezo yako hata mimi naona corridor ni nyingi
3. Sawa sawa
4. Sawa kabisa ila fridge acha ikae hapo mkuu
PS. Sawa kabisa
 
1. Fridge inatakiwa kuhusiana na sink na jiko Kwa ajili ya matumizi ya mpishi mkuu. Kama wewe ndiye mpishi mkuu wa nyumbani na unapenda hivyo sawa ila kama wapishi ni wengine itakuwa kero kwao. Vimigogoro na minuno vya rejareja vyaweza kutokea Kwa kitu simple tu kama hichi 😄😄

2. Corridor nimejaribu kudoodle kwenye simu naona nashindwa ila unaweza vuta Kuta kidogo na kuweka makabati na milango iwekwe Kwa kuingilia pembeni. Unaweza refer kwenye Ile plan yangu kwenye post yangu...

Screenshot_20230316-040910.jpg
 
2. Corridor nimejaribu kudoodle kwenye simu naona nashindwa ila unaweza vuta Kuta kidogo na kuweka makabati na milango iwekwe Kwa kuingilia pembeni. Unaweza refer kwenye Ile plan yangu kwenye post yangu...
img_1_1678031072251.jpg

Nimefikiria hapo red kuwe na milango ya hizo rooms. Halafu nitoe hiyo kuta kwenye njano
 
Back
Top Bottom