Mnaoamini kuwa uchawi upo mnatumia vigezo gani?

Mnaoamini kuwa uchawi upo mnatumia vigezo gani?

Kumbe chuma tayari kishafika 😹😹
Nilitaka nikuite bro unichapie watu fimbo za ubongo
Kuna watu hapa leo hii hawana tofauti na wale walioamini risasi zitageuka maji kwa supernatural powers.

Ingawa wale waliishi zaidi ya miaka 100 iliyopita, enzi ambazo hakukuwa na upatikanaji wa habari kirahisi.

Na hawa wanaishi enzi za internet, kila habari iko online.
 
Mchawi anapewa nguvu ya uchawi na jini ndie umuwezesha kupaa, kupenya kwenye ukuta kubadilika kitu chochote sasa jini hana shida na pesa hizi za kibinadamu
 
Kuna watu hapa hawana tofauti na wale walioamini risasi zitageuka maji kwa supernatural powers.

Ingawa wale waliishi zaidi ya miaka 100 iliyopita, enzi ambazo hakukuwa na upatikanaji wa habari kirahisi.

Na hawa wanaishi enzi za internet, kila habari iko online.
Lakini dawa za kuzuia risasi zipo wauze majambazi au police watakuambia dunia ina mengi usiyoyajua
 
Uchawi upo kwa sababu vitabu vilivyotuambia kuwa kuna Mungu na sisi tumeumbwa na huyo,vitabu hivyo vinasema wazi wazi kuwa (WACHAWI,WAZINZI NA WAONGO WOTE MOTONI)kuna mahala Katika maaandiko Mungu anasema nami nitakuwa shahidi mwaminifu juu ya wazinzi ,wrong,waabuduo sana na wachawi siku ya HUKUMU , HIVYO KAMA HAUMINI VITABU VYA DINI UPO SAHIHI ILA KAMA unaviamini na unaamini Mungu yupo basi wewe ni MPUMBAVU kwani kitabu kichokwambia kuna Mungu ndo hicho hicho kinatoa ushuhuda juu ya uwepo wa uchawi
 
Katika miaka niliyo nayo mpaka sasa sijawahi kukubali kuwa eti kuna uchawi sijui mtu anaweza kuloga sijiui mambo yako yasiende.

Kama kweli uchawi upo kwanini hao wachawi wasiende benki wakaloga wakachukua pesa.

Kama kuna mtu humu ndani alishawahi kulogwa njoo utupe mrejesho ilikuwaje.

Pia, kama kuna mtu anajiamini anaweza kuniloga njoo uniloge we taja unachotaka kutoka kwangu nitakupa we niloge kama kweli unaweza😂😂

Mwisho hakuna uchawi ni dhana za kufikilika tu.
Wachawi na pesa ni mbali mbali
Wao kazi yao ni kulisha watu misumari, nyembe na mijusi
 
Nilitaka kuthibitisha uchawi hamna
Hapana ulichokuwa unafanya ni kutaka kuthibitisha kuwa hakuna wa kukuroga, na huo uchunguzi wako hausemi kuwa wapo watu waliyojaribu kukuroga na hakuna kilichotokea au kwamba uliongea tu na hao watu wakakusikiliza na hawakufanya kitu.

Sasa nashindwa kuelewa kwa hali hiyo ulifikia vp hitimisho la kuwa hakuna uchawi?
 
Hakuna uchawi ni uoga tu wa watu 😹
Halafu ukitaka kujua waganga jau siku hizi wanachukua kuku mpk wa kisasa
Sasa uoga kvp? We umekariri kwamba uchawi ni kurogana tu ndio maana unasema ni uoga wa watu. Ina maana haujawahi kusikia visa vyenye kuhusishwa na uchawi mbali na kurogana?
 
Unaweza kwanza ukaelezea kwa unavyoelewa wewe huo uchawi ni nini hasa na kwanini unasema haupo?
Uchawi ni hisia na fikra haribifu zisizo na maana yoyote, zilizopo miongoni mwa baadhi ya jamii fulani, ambazo zinaweza kuleta matatizo makubwa kwenye jamii, fikra hizi zilipaswa kutokuaminiwa kabisa kwa gharama yoyote, kwani zinaua fikra chanya na ari kubwa ya maendeleo na mabadiliko ya kijamii.

Mtu kapatwa na ugonjwa fulani tu ,badala ya kufanya uchunguzi wa kina watu wanaamua kusema rahisi tu ni uchawi ,hii inaua nguvu ya utafiti na kupata tiba stahiki .

Mtu ananunua kajigari tu ka mil 10 na kanyumba labla na biashara ya kawaida tu watu, wanasema kaenda kwa waganga na hii inaua ile ari ya watu kuamini kwenye kazi na kutafuta.

Uchawi ni fikra potofu ambazo hazipaswi kupewa kipaumbele kabisa.
 
Sasa kama huo ndio uchawi kama ulivyoeeleza je hapo unataka uthibitishiwe nini sasa? Unataka nikuthibitishie hizo fikra na hisia ambazo mwenyewe umekiri zipo kwenye jamii? Au hukuelewa swali?
 
Wewe una akili kuliko mtume paulo aliyemkemea mchawi hadharani?
Au wewe una akili kuliko Musa aliyepambana na wachawi mbele ya Farao? Au wewe una akili kuliko Darius mfalme wa Babeli aliyekua akiwatumia waganga na wachawi kuwapumbaza wengine ili aendelee kutawala au wewe una akili kuliko Wafalme wa ulaya walioamua kuagiza wachawi wote kwenye tawala zao wakamatwe na kuuawa (season of witch)
Ungejua hao wanaokutawala au watu Maarufu unaowasifia mitandaoni wanatumia nini usingeandika uzi kama huu.

Acheni kuwapumbaza wengine ili muwatese wasitafute solution ya matatizo yao
UCHAWI UPO.
Kwa tulipofikia katika kujenga hoja, vitabu vya mila za watu na stori zao[biblia, quran, torati n.k.] si reference tena. Jitoe katika huo mtaro ulete hoja nje ya hayo maandishi na kusadikika tutakuelewa tu!
 
Sasa kama huo ndio uchawi kama ulivyoeeleza je hapo unataka uthibitishiwe nini sasa? Unataka nikuthibitishie hizo fikra na hisia ambazo mwenyewe umekiri zipo kwenye jamii? Au hukuelewa swali?
Sawa apo tumeenenda vizuri sana , ndio maana nikakuambia hizo fikra zipo lakini haimaanishi kwamba ni fikra sahihi , ni kama imani tu zipo lakini hazina uthibitisho.
 
Uchawi ni kufanya mambo yasiyo ya kawaida
Kwa hiyo uchawi upo na unatofautiana na mazingira na tamaduni
 
Watu wanashindwa kuelewa utofauti kati ya imani potofu za ushirikina katika jamii na uwepo wa uchawi?

Katika hizo nchi ambazo zimeendelea ambako hakuna sana imani za uchawi, uelewa wao kuhusu uchawi kwa wenye kuamini ni tofauti kabisa na sisi huku ambako mtu anakwambia kama uchawi upo niroge.
 
Watu wanashindwa kuelewa utofauti kati ya imani potofu za imani ya uchawi katika jamii na uwepo wa uchawi?

Katika hizo nchi ambazo zimeendelea ambako hakuna sana imani za uchawi, uelewa wao kuhusu uchawi kwa wenye kuamini ni tofauti kabisa na sisi huku ambako mtu anakwambia kama uchawi upo niroge.
Unawezaje kuthibitisha uwepo wa uchawi?
 
Back
Top Bottom