Mtu akiwa mtoto mdogo, anaamini kuwa baba yake ana uwezo sana, likipita gari utasikia watoto wanaimba ''gari ya baba''.
Anaamini hakuna mtu anaeweza kumpiga baba yake, baba yake anajua yote na hakuna kitu kinamshinda.
Akikua anagundua kuwa kumbe siyo kweli.
Kwa bahati mbaya kabisa bado kwny ubongo wake kuna ile hulka ya kutaka kuwa na mtu au kiumbe anayeweza yote, anayejua yote.
Hapo ndipo ubongo wa binadamu ukaamua kujitungia na kujiaminisha kuwa yupo Mungu baba muweza wa yote, anayejua yote.
Ukisoma kitabu cha Edward Craig, THE MIND OF GOD AND THE WORKS OF MAN, utagundua kuwa anajaribu kuraise swali, kwamba kati ya Mungu na binadamu nani alimuumba mwenzake?
Lakini mwishoni, ni kama anahitimisha kuwa ubongo wa binadamu ndio uliomuumba Mungu.