Ubavu
JF-Expert Member
- Jun 19, 2012
- 2,790
- 3,263
Hamna wa kujibu maswali hapa... Wengi wao ni mediocre. Walikuwa brainwashed kama walivyo wazazi wao.. Wanaimba nyimbo wasizojua maana yake..tujikite kwenye kujibu maswali naona mnaleta mahubiri tu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hamna wa kujibu maswali hapa... Wengi wao ni mediocre. Walikuwa brainwashed kama walivyo wazazi wao.. Wanaimba nyimbo wasizojua maana yake..tujikite kwenye kujibu maswali naona mnaleta mahubiri tu
Evidence ya kwanza ni the way mungu anavyojicontradict mwenyewe... Wakati anasema yeye ndiye mwenye nguvu kuliko wote anatokea shetani ambaye anaweza kupindisha maamuzi ya mungu..! (how comes?!)
Lakini pia yeye anasema anaroho nzur kuliko viumbe vyote wakati huo huo anaacha vichanga visivyo na hatia kupata madhara.. Najua utasema anataka kuwapima wazazi wa kichanga hicho imani zao, then tunakuja kujiuliza kama ana nguvu za kujua yaliyo moyoni mwetu basi hakuna ulazima wa kuleta majanga kwa mtoto yule kwani (kama ananguvu hizo) si angekuwa ameshajua imani za wazazi wale..?!
Kama kweli mungu yupo, angeshajitokeza ili kuondoa mauaji na maumivu wanayoyapata wanadamu kupitia mgongo wake...! Angetokea ili watu wajue ni mungu yupi wa ukweli..
Wahindi wa america walipata kumjua mungu wa kikristo mnamo karne za hivi karibuni, unataka kuniambia mababu zao waliokufa kabla ya kumjua kristo or Muhammad wataingia motoni kwakuwa ni makafiri or hawakubatizwa kwamaji??
Na mie nakuuliza swali. Kati ya miungu yote (mungu wa wakristo, waislamu, wayahudi, wahindu, nk.) yupi wa ukweli..?!Nipatie sababu, Usilete issue za kusema eti mungu ni mmoja..! Manaa hii kitu kwa kuangalia mifumo ya dini mbalimbali yaonyesha wazi kuwa haiwezekani.
Mkuu!Nyongeza, mungu hakuua watu tu hata mifugo jamani, halafu bado watu wanamuona ni mungu mzuri!!. Anyway hayupo hata hivo kama yupo basi hana muda na binadamu kabisa.
Kwani unavyojua wewe according to your religion, mungu ametuumba kwaajili ya nini?! Yaani ametuleta duniani ili yeye apate nini?Mkuu!
Inasikitisha sana kusoma hoja kama hii, inaonesha ni kiasi gani hamtafakari kwa umakini kile mnachokiamini. Hapa mnamaanisha ni 'kosa' kwa Mungu kuua mtu au mnyama.
Swali dogo ni hili, unafikiri ni kosa kwa mchoraji akifuta picha aliyoichora? Mpishi akimwaga chakula alichopika?
Ni kosa kwa mtu/shetani/malaika kumuua mtu mwingine, kwa sababu si mali yake. Huwezi kutumia hoja hiyo kwa Mungu, ni kichekesho. Ameweka pumzi ndani yako na ataitoa muda wowote anaotaka, kwa namna yoyote anayotaka. Mimi na wewe tu mali yake.
Heshima kwako mkuuKwani unavyojua wewe according to your religion, mungu ametuumba kwaajili ya nini?! Yaani ametuleta duniani ili yeye apate nini?
Kuna baadhi ya dini zinasema kuwa tumeletwa duniani ili tumuabudu. Je?, mungu hawezi kuishi bila ya ibada zetu? Kama anaweza, kwanini anatulazimisha..?! Kwanini isiwe maamuzi yetu kuja duniani...
Kama mungu ameweka free will kwanini akuadhibu baada ya kufanya chaguo lililotokana na yeye kukupa maamuzi.?
Wakati kuna free will, mungu anasema kuwa kila mtu kashampangia mwisho wake... Kwamba watu tulio duniani ni watekelezaji wa mipango yake tu ambayo alishaipanga. Sasa hapo free will ipo wapi?
Lakini pia, wakati kuna free will mungu anasema alishajua tutakachofanya kabla hajatuumba. Hivi ni nini kazi ya maombi, ikiwa mungu alishapanga kila kitu?
Unajuaje kuwa dini unayoiamini ndio dini sahihi na dini nyengine sio sahihi?!Heshima kwako mkuu
Nimetangulia kusema kwa kuikubali hoja yako kwamba haiwezekani dini zote zikawa sahihi. Kwani zinapingana kwenye mafundisho ya msingi, tunabakiwa na hitimisho kwamba ipo dini moja tu ambayo ni sahihi, zingine zinazopingana nayo ni dini za uongo. Zinaweza zikawa mbali au karibu na ukweli kulingana na vile zinavyoelezea mambo. Kwa hiyo majibu ya maswali kama kwa nini Mungu alituumba na mengineyo yatategemea usahihi wa dini yenyewe inayojibu. Usifanye kosa la kukana uwepo wa Mungu ati kwa sababu dini zimeelezea kwa namna isiyoridhisha, inawezekana si dini sahihi.
Kuhusu uhuru wa kuchagua tuliopewa na kwanini Mungu atuadhibu tukichagua maovu. Hii inahitaji kujua tu kuhusu uhalisia wa vitu ulivyo. Hakuna moto wa baridi, mwanga mweusi, maji makavu, mzee mtoto,.... unapochagua kitu umechagua na yale yote yanayoambatana na hicho kitu. kumbe mtu akichagua barafu, amechagua na baridi, akichagua giza amechagua na kutokuona... Unapochagua mambo yanayoitwa dhambi, umechagua na adhabu yake pia. Usijiulize kwa nini atuadhibu, kwani ndicho ulichochagua( huwezi kutenganisha dhambi na adhabu, wema na baraka) - hiyo ndio maana ya uhuru wa kuchagua... unachagua na kinachoambatana nacho.
Maswali yaliosalia yanahoji sifa na tabia za Mungu, nimejibu kwamba shida iko kwenye tafsiri ya neno 'kujua mambo yajayo, kupanga kuhusu maisha yetu ...' Ukiweza kuelewa vizuri maana za hayo mambo, hutaona shida yoyote hapo.
MkuuUnajuaje kuwa dini unayoiamini ndio dini sahihi na dini nyengine sio sahihi?!
Na unamzungumziaje yule aliyezaliwa katika uhindu (Hinduism) akakuwa katika dini hiyo mpaka anakufa bila ya kumjua mungu na dini ya ukweli, akifa ataenda motoni?
Kafiri katika ubora wakeNyie mnao amini uwepo wa Mungu, Wakristo na waislam, na madhehebu mengine Je kila mmoja wenu mnamaanisha Mungu Mmoja?
Yani unavyomfikiria wewe na mwezio ni hivyohivyo? Je unauhakika Kiongozi wako wa dini, Rafiki yako, na yeyote yule Jinsi anavyomuwaza huyu Mungu alivyo ndivyo unavyomuwaza wewe? Yani picha uliyojijengea kichwani mwako Jinsi alivyo, tabia zake ndivyo wenzio wanavyomuwaza hivyo? Kama mnatofautiana hatima yake nini?
Je huyu Mungu wenu alivyokusudia mumuwaze alivyo ndivyo ilivyo?
Je mpaka sasa unauhakika na dini yako ndio sahihi kumweleza huyo Mungu? Au tangu upokee kutoka kwa wazazi wako dini hiyo ndio umejidhihirisha wazi kwamba upo sahihi?
Je umejifunza dini nyingine kujihakikishia upo sahihi mpaka sasa kwamba Mungu anaikubali dini yako? na upo sahihi?
Je Ni biblia na quran ndio references kuthibitisha Mungu yupo, na jinsi alivyo?
Unajidhihirishaje kwamba vitabu hivyo si maandiko ya watu kwa utashi wao?
Je Maswali yangu hapo Unaweza kuyajibu????
Ww ni mweupe sana kichwani mkuu. Huna cha maana zaid ya kuwahi kukoment ili uonekane tu umewah kucoment ila unachoandika ni absolutely worthlessMpinga Mungu naona upo kazini
Kwanza kwa fikra zako zilizokutuma kuleta huu uzi je wajua Mungu ni nini au ni nani? Ili tukujibu kutokana na uwezo wa akili yako tusije kukupoteza kabisa. Pili kutokana na bandiko lako hili inaonyesha wewe huamini kuwa kuna Mungu, sasa kitu usichokiamini cha kukera nini? Si uwaache wenye imani zao waamini wanacho kiamini?
Njia nzuri ya kufanya mtu abadili anacho kiamni ili afate unacho kiamini ni kukizungumza kile unacho kiamini na jinsi gani kilivyo kusaidia na faida yake kwako kisha mtu mwenyewe alinganishe kile anacho kiamini na kile ukiaminicho wewe kisha kwa dhamira yake achague kukifata au kutokifata kile uaminicho wewe.
Ukimwambia mtu ubaya wa kile anachokiamini ili aamini kile unacho amini, akija huko akakuta mapungufu katika hicho unacho amini utakuwa umempoteza kabisa.
Hakuna imani isiyo na mapungufu kwamaana sisi binadamu pia tunamapungufu, kama jinsi tunavyo fundisha namna ya kuishi na mapungufu yetu ndivyo tunavyo fundishwa kukabiliana na mapungufu katika imani zetu.
Si kosa kujifunza imani nyingine, lakini hii haitakiwi kwa wale walio dhaifu kiimani kwamaana badala ya kuwajenga inaweza kuwapotosha kabisa.
Imani yenye mapungufu itakufikisha ktk utimilifu?Nadhani sihitaji kukupa tafsiri ya neno potofu kwamaana kwa umri wako nadhani wajua maana, kuhusu imani yangu ninauhakika sio potofu ila inamapungufu, kuhusu kujiridhisha sijui kujidhihirisha hilo ni la kiimani zaidi na kwa kuwa imani yangu haikuhusu hilo huna haja ya kulijua, kuhusu mimi kupotoka au la nishakujibu, sijapotoka kwamaana imani yangu sio potofu.