Evidence ya kwanza ni the way mungu anavyojicontradict mwenyewe... Wakati anasema yeye ndiye mwenye nguvu kuliko wote anatokea shetani ambaye anaweza kupindisha maamuzi ya mungu..! (how comes?!)
Lakini pia yeye anasema anaroho nzur kuliko viumbe vyote wakati huo huo anaacha vichanga visivyo na hatia kupata madhara.. Najua utasema anataka kuwapima wazazi wa kichanga hicho imani zao, then tunakuja kujiuliza kama ana nguvu za kujua yaliyo moyoni mwetu basi hakuna ulazima wa kuleta majanga kwa mtoto yule kwani (kama ananguvu hizo) si angekuwa ameshajua imani za wazazi wale..?!
Kama kweli mungu yupo, angeshajitokeza ili kuondoa mauaji na maumivu wanayoyapata wanadamu kupitia mgongo wake...! Angetokea ili watu wajue ni mungu yupi wa ukweli..
Wahindi wa america walipata kumjua mungu wa kikristo mnamo karne za hivi karibuni, unataka kuniambia mababu zao waliokufa kabla ya kumjua kristo or Muhammad wataingia motoni kwakuwa ni makafiri or hawakubatizwa kwamaji??
Na mie nakuuliza swali. Kati ya miungu yote (mungu wa wakristo, waislamu, wayahudi, wahindu, nk.) yupi wa ukweli..?!Nipatie sababu, Usilete issue za kusema eti mungu ni mmoja..! Manaa hii kitu kwa kuangalia mifumo ya dini mbalimbali yaonyesha wazi kuwa haiwezekani.