Uthibitisho wa kwanza kwamba Mungu yupo ni uwepo wako na uwezo wa kuhoji kwamba Mungu yupo au la. fikiria nguo iulize kama wapo washonaji au gari ya NISSAN iulize kama kampuni ya NISSAN ipo au la. Unatakiwa kijiangalia mwenyewe: ulitoka wapi, unaweza kujijua mwenyewe asilimia 100, unaweza tatua matatizo yote yanayokuja mbele zako?
Tafakari na mimi kitu kidogo: ulishawahi jiuliza kuhusu vyakula unavyokula, vilitoka wapi, kwa nini ukivila havikupi shida. Turudi kwa gari; gari inaenda kwa mafuta au gas au umeme, gari iliyotengenezwa iende kwa mafuta haiwezi kwenda kwa umeme. inamaana aliyebunu na kutengeneza gari alifanya hivyo akijua itaenda kwa kutumia nini tena bila shida.
Rafiki yangu na ndugu yangu kwako wewe ukila maharage ukashiba hushangai: nani alinibuni, akanitengeneza - haiyumkuni ndiye aliye buni na kutengeneza maharage. Sidhani kama UNAAMINI wewe na maharage mlikuja kwa bahati (chance) na kama ndivyo hiyo nayo ni DINI maana msingi wake ni imani tuu, nini tofauti na dini basi?