Mnaoamini Mungu, kwenye vichwa vyenu mna "imagine" sawa jinsi alivyo?

Mnaoamini Mungu, kwenye vichwa vyenu mna "imagine" sawa jinsi alivyo?

Evidence ya kwanza ni the way mungu anavyojicontradict mwenyewe... Wakati anasema yeye ndiye mwenye nguvu kuliko wote anatokea shetani ambaye anaweza kupindisha maamuzi ya mungu..! (how comes?!)
Lakini pia yeye anasema anaroho nzur kuliko viumbe vyote wakati huo huo anaacha vichanga visivyo na hatia kupata madhara.. Najua utasema anataka kuwapima wazazi wa kichanga hicho imani zao, then tunakuja kujiuliza kama ana nguvu za kujua yaliyo moyoni mwetu basi hakuna ulazima wa kuleta majanga kwa mtoto yule kwani (kama ananguvu hizo) si angekuwa ameshajua imani za wazazi wale..?!
Kama kweli mungu yupo, angeshajitokeza ili kuondoa mauaji na maumivu wanayoyapata wanadamu kupitia mgongo wake...! Angetokea ili watu wajue ni mungu yupi wa ukweli..
Wahindi wa america walipata kumjua mungu wa kikristo mnamo karne za hivi karibuni, unataka kuniambia mababu zao waliokufa kabla ya kumjua kristo or Muhammad wataingia motoni kwakuwa ni makafiri or hawakubatizwa kwamaji??
Na mie nakuuliza swali. Kati ya miungu yote (mungu wa wakristo, waislamu, wayahudi, wahindu, nk.) yupi wa ukweli..?!Nipatie sababu, Usilete issue za kusema eti mungu ni mmoja..! Manaa hii kitu kwa kuangalia mifumo ya dini mbalimbali yaonyesha wazi kuwa haiwezekani.

Heshima kwako mkuu.
Mifano uliyotoa ni dhaifu sana ikiwa hiyo ndio uthibitisho wako kwamba 'Mungu hayupo' ni 'fact'. Lakini kwa kifupi unamaanisha kwamba Mungu hayupo kwa sababu unaona sifa na tabia za Mungu zinapingana na unavyoona mambo yanaendelea katika huu ulimwengu. Hoja hii si sahihi kwa sababu kadhaa.

1. Inashindwa kutambua maana sahihi ya tabia na sifa za Mungu. Ukisikia Mungu ana Upendo wote, haimaanishi 'Upendo' utatafsiriwa kama unavyotaka wewe. Ukimwambia mtoto wako unampenda, halafu akifanya kosa ukamchapa fimbo, haimaanishi unajipinga kuhusu upendo... shida iko kwenye tafsiri ya neno upendo. Ni muhimu kutafsiri sifa za Mungu ukizingatia uhusiano uliopo kati yetu na Yeye.

2. Inashindwa kujumuisha sifa zote za Mungu
Mungu hana sifa moja tu, mara nyingi watu wanafanya makosa kujaribu kuelezea jambo fulani kwa kuzingatia sifa moja tu ya Mungu. Upendo, Haki, Utakatifu, Wema, Uweza, Upole, Wivu, Mamlaka, Hekima , Enzi, Huruma.... vyote vinatakiwa kuzingatiwa unapoelezea jambo lolote kumhusu Mungu. Ulimwengu upo kama ulivyo kutokana na mjumuisho wa sifa zote za Mungu. Tumia vizuri muda wako kumfahamu Mungu kwa ufasaha kabla hujaanza kupinga uwepo wake.

3. Kuhusu swali lako, nakubaliana na wewe KABISA kwamba haiwezekani dini zote zikawa sahihi, Mungu ameelezwa tofautitofauti kwenye hizi dini, mafundisho ya muhimu yanapingana kati ya dini tofauti. Na hii ndio sababu nimeeleza hapo juu kwamba anayeamini uwepo wa Mungu amepatia kujibu swali la msingi, lakini haimaanishi amemaliza maswali. Swali linalofuata ni Mungu yupi kati ya wote wanaotajwa katika dini hizi ama zingine ni Mungu wa kweli. Lakini kabla hatujaanza huko, tujikite kwenye swali la msingi kuhusu uwepo wa Mungu.

Mungu yupo, kila kitu kinathibitisha uwepo wa Mungu. Unapoanza kuchunguza uthibitisho wa uwepo wa Mungu, hakikisha uko tayari ndani yako kukubali kuufuata ukweli popote utakapokupeleka.
 
Nyongeza, mungu hakuua watu tu hata mifugo jamani, halafu bado watu wanamuona ni mungu mzuri!!. Anyway hayupo hata hivo kama yupo basi hana muda na binadamu kabisa.
Mkuu!

Inasikitisha sana kusoma hoja kama hii, inaonesha ni kiasi gani hamtafakari kwa umakini kile mnachokiamini. Hapa mnamaanisha ni 'kosa' kwa Mungu kuua mtu au mnyama.

Swali dogo ni hili, unafikiri ni kosa kwa mchoraji akifuta picha aliyoichora? Mpishi akimwaga chakula alichopika?
Ni kosa kwa mtu/shetani/malaika kumuua mtu mwingine, kwa sababu si mali yake. Huwezi kutumia hoja hiyo kwa Mungu, ni kichekesho. Ameweka pumzi ndani yako na ataitoa muda wowote anaotaka, kwa namna yoyote anayotaka. Mimi na wewe tu mali yake.
 
Kwani unavyojua wewe according to your religion, mungu ametuumba kwaajili ya nini?! Yaani ametuleta duniani ili yeye apate nini?

Kuna baadhi ya dini zinasema kuwa tumeletwa duniani ili tumuabudu. Je?, mungu hawezi kuishi bila ya ibada zetu? Kama anaweza, kwanini anatulazimisha..?! Kwanini isiwe maamuzi yetu kuja duniani...

Kama mungu ameweka free will kwanini akuadhibu baada ya kufanya chaguo lililotokana na yeye kukupa maamuzi.?

Wakati kuna free will, mungu anasema kuwa kila mtu kashampangia mwisho wake... Kwamba watu tulio duniani ni watekelezaji wa mipango yake tu ambayo alishaipanga. Sasa hapo free will ipo wapi?

Lakini pia, wakati kuna free will mungu anasema alishajua tutakachofanya kabla hajatuumba. Hivi ni nini kazi ya maombi, ikiwa mungu alishapanga kila kitu?
 
Heshima kwako mkuu

Nimetangulia kusema kwa kuikubali hoja yako kwamba haiwezekani dini zote zikawa sahihi. Kwani zinapingana kwenye mafundisho ya msingi, tunabakiwa na hitimisho kwamba ipo dini moja tu ambayo ni sahihi, zingine zinazopingana nayo ni dini za uongo. Zinaweza zikawa mbali au karibu na ukweli kulingana na vile zinavyoelezea mambo. Kwa hiyo majibu ya maswali kama kwa nini Mungu alituumba na mengineyo yatategemea usahihi wa dini yenyewe inayojibu. Usifanye kosa la kukana uwepo wa Mungu ati kwa sababu dini zimeelezea kwa namna isiyoridhisha, inawezekana si dini sahihi.

Kuhusu uhuru wa kuchagua tuliopewa na kwanini Mungu atuadhibu tukichagua maovu. Hii inahitaji kujua tu kuhusu uhalisia wa vitu ulivyo. Hakuna moto wa baridi, mwanga mweusi, maji makavu, mzee mtoto,.... unapochagua kitu umechagua na yale yote yanayoambatana na hicho kitu. kumbe mtu akichagua barafu, amechagua na baridi, akichagua giza amechagua na kutokuona... Unapochagua mambo yanayoitwa dhambi, umechagua na adhabu yake pia. Usijiulize kwa nini atuadhibu, kwani ndicho ulichochagua( huwezi kutenganisha dhambi na adhabu, wema na baraka) - hiyo ndio maana ya uhuru wa kuchagua... unachagua na kinachoambatana nacho.

Maswali yaliosalia yanahoji sifa na tabia za Mungu, nimejibu kwamba shida iko kwenye tafsiri ya neno 'kujua mambo yajayo, kupanga kuhusu maisha yetu ...' Ukiweza kuelewa vizuri maana za hayo mambo, hutaona shida yoyote hapo.
 
Unajuaje kuwa dini unayoiamini ndio dini sahihi na dini nyengine sio sahihi?!
Na unamzungumziaje yule aliyezaliwa katika uhindu (Hinduism) akakuwa katika dini hiyo mpaka anakufa bila ya kumjua mungu na dini ya ukweli, akifa ataenda motoni?
 
Mkuu

Unajua kwa kuuchunguza ushaidi uliopo katika dini husika. Mafundisho ya dini yoyote yanahusisha mambo ambayo hatuwezi kuyathibitisha kirahisi ( mambo ya kiroho sana, siku ya mwisho, asili ya vitu,...) na pia mambo ambayo tunaweza kuyathibitisha kabisa/kwa kiwango fulani (inapogusia mambo ya kisayansi, kihistoria, kihisia...) Kwa kutumia mambo ambayo tunaweza kuthibitisha, unapokuta maelezo ya dini husika si ya kweli kila wakati- si kosa tukifikia hitimisho kwamba dini husika si ya kuaminika. Na unapoipima kwa hayo mambo na ukakuta iko sahihi kila wakati, unakua angalau na sababu ya kuiweka katika kundi la dini ya kuaminika. Huu hauwi mwisho wa uchunguzi wako, labda tuiite hatua mojawapo muhimu. ANGALIZO hapa ni kuwa sharti tutumie vyanzo vya kuaminika vya hiyo dini, tuulize kwa waliobobea kabisa kwenye dini husika (si tu cheo chake ), tutumie utaratibu wa kufafanua mambo unaotumiwa na dini husika, tusiwe na misimamo kabla....

IKIWA Uhindu si dini ya kweli ( hatujatoa ushahidi wowote, tutumie kama mfano tu). Tunajua kuwa sifa mojawapo ya Mungu ni haki. Ikiwa atahukumu watu, hatutegemei atatenda kinyume na jinsi alivyo- hukumu yake itakuwa ya haki. Hii inamaanisha vitu kama kutokujua, kutokudhamilia,...(watoto wadogo, wagonjwa wa akili, wasiowahi kusikia hizo habari n.k ) vitafikiliwa kwenye hukumu. Mwisho wa siku ni kuwa kila mtu atatendewa haki.

Ni bora tuanze kuzichunguza dini tulizowahi kuzisikia, ikiwa zote si sahihi, tutakuwa na cha kujitetea. Ikiwepo sahihi, hatuna udhuru. Kwa hali zote, uvivu, mizaha, kiburi, utani,matusi dhidi ya Mungu au dini ni hatari sana Ikiwa vitazingatiwa kwenye hukumu ya haki.
 
Hilo siyo swali complex. Hivi ulivyokuwa unaiwaza Dar es salaam kabla haujafika, ni sawa na alivyokuwa akiiwaza rafiki yako ambaye mlitoka naye maguguni kuja kutafuta vibarua?
 
Nyie mnao amini uwepo wa Mungu, Wakristo na waislam, na madhehebu mengine Je kila mmoja wenu mnamaanisha Mungu Mmoja?

Yani unavyomfikiria wewe na mwezio ni hivyohivyo? Je unauhakika Kiongozi wako wa dini, Rafiki yako, na yeyote yule Jinsi anavyomuwaza huyu Mungu alivyo ndivyo unavyomuwaza wewe? Yani picha uliyojijengea kichwani mwako Jinsi alivyo, tabia zake ndivyo wenzio wanavyomuwaza hivyo? Kama mnatofautiana hatima yake nini?

Je huyu Mungu wenu alivyokusudia mumuwaze alivyo ndivyo ilivyo?
Je mpaka sasa unauhakika na dini yako ndio sahihi kumweleza huyo Mungu? Au tangu upokee kutoka kwa wazazi wako dini hiyo ndio umejidhihirisha wazi kwamba upo sahihi?

Je umejifunza dini nyingine kujihakikishia upo sahihi mpaka sasa kwamba Mungu anaikubali dini yako? na upo sahihi?

Je Ni biblia na quran ndio references kuthibitisha Mungu yupo, na jinsi alivyo?
Unajidhihirishaje kwamba vitabu hivyo si maandiko ya watu kwa utashi wao?

Je Maswali yangu hapo Unaweza kuyajibu????
Kafiri katika ubora wake
 
Akili fupi haiwezi kutafakari na kuona taswira ya Mungu wangu ninae mwamini
 
Mpinga Mungu naona upo kazini
Ww ni mweupe sana kichwani mkuu. Huna cha maana zaid ya kuwahi kukoment ili uonekane tu umewah kucoment ila unachoandika ni absolutely worthless
Kwanza kwa fikra zako zilizokutuma kuleta huu uzi je wajua Mungu ni nini au ni nani? Ili tukujibu kutokana na uwezo wa akili yako tusije kukupoteza kabisa. Pili kutokana na bandiko lako hili inaonyesha wewe huamini kuwa kuna Mungu, sasa kitu usichokiamini cha kukera nini? Si uwaache wenye imani zao waamini wanacho kiamini?

Njia nzuri ya kufanya mtu abadili anacho kiamni ili afate unacho kiamini ni kukizungumza kile unacho kiamini na jinsi gani kilivyo kusaidia na faida yake kwako kisha mtu mwenyewe alinganishe kile anacho kiamini na kile ukiaminicho wewe kisha kwa dhamira yake achague kukifata au kutokifata kile uaminicho wewe.

Ukimwambia mtu ubaya wa kile anachokiamini ili aamini kile unacho amini, akija huko akakuta mapungufu katika hicho unacho amini utakuwa umempoteza kabisa.

Hakuna imani isiyo na mapungufu kwamaana sisi binadamu pia tunamapungufu, kama jinsi tunavyo fundisha namna ya kuishi na mapungufu yetu ndivyo tunavyo fundishwa kukabiliana na mapungufu katika imani zetu.

Si kosa kujifunza imani nyingine, lakini hii haitakiwi kwa wale walio dhaifu kiimani kwamaana badala ya kuwajenga inaweza kuwapotosha kabisa.
 
Nadhani sihitaji kukupa tafsiri ya neno potofu kwamaana kwa umri wako nadhani wajua maana, kuhusu imani yangu ninauhakika sio potofu ila inamapungufu, kuhusu kujiridhisha sijui kujidhihirisha hilo ni la kiimani zaidi na kwa kuwa imani yangu haikuhusu hilo huna haja ya kulijua, kuhusu mimi kupotoka au la nishakujibu, sijapotoka kwamaana imani yangu sio potofu.
Imani yenye mapungufu itakufikisha ktk utimilifu?
 
Back
Top Bottom