Mnaobeza mafanikio ya Awamu ya Sita, zungukeni Tanzania muone mafanikio ya Serikali ya Rais Samia katika utekelezaji wa miundombinu

Mafanikio ya wananchi ni kuwa huru ktk Nchi Yao.

Wananchi wawe huru kuchagua viongozi wawatakao, Sanduku la kura lililoibwa 2020 ndo lilimweka alipo sasa, Je amefanikiwa kuondoa wizi huo?

Maendeleo ni Uwezo wa wananchi kuwawajibishwa Viongozi wabovu wawatakao, Leo wanatutukana hadharani wakisema tuhamie Burundi na hatuna la kuwafanya.

KATIBA mpya ndo italeta maendeleo ya Kweli.

Ameeeen
 
Tulishakubaliana maendeleo ya watu sio vitu! Vip leo?
 
Hao ni waganga njaa waomekane ili wapewe vyeo.
But Mama Samia anafa nanya vizuri ingawa wapo wako chawa wanaomzunguka.
 
Kuna watu kazi yao wamekuwa ni kupinga na kubeza mafanikio ya Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Samia Suluh Hassan, yawezekana wanatumia
Mafanikio huwa yanatangazwa kwani watanzania hawana macho ya kutofautisha nyeupe na nyeusi?
Mmeona njia rahisi ya kupata teuzi ni kujitoa ufahamu na kuwa chawa.
 
Kuna watu kazi yao wamekuwa ni kupinga na kubeza mafanikio ya Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Samia Suluh Hassan...
Achana na Hawa wanaoshinda mitandaoni ,watakupotosha bure..

Hawa hata kura zikipigwa lazima waongoze kwa mafuriko humu mitandaoni ila huko kwa Wananchi hakuna hata anaewaelewa na wao huwa wako busy humu humu huwezi wakuta mtaani kupinga.
 
Achana na Hawa wanaoshinda mitandaoni ,watakupotosha bure..

Hawa hata kura zikipigwa lazima waongoze kwa mafuriko humu mitandaoni ila huko kwa Wananchi hakuna hata anaewaelewa na wao huwa wako busy humu humu huwezi wakuta mtaani kupinga.
Kabisa mkuu The Sunk Cost Fallacy nashanga wanajifanya hawaoni kazi zinazofanyika, wamebaki kupiga kelele kwenye mitandao, miradi yote ya Maendeleo inayotekelezwa kwao wanaona bute
 
Mafanikio huwa yanatangazwa kwani watanzania hawana macho ya kutofautisha nyeupe na nyeusi?
Mmeona njia rahisi ya kupata teuzi ni kujitoa ufahamu na kuwa chawa.
Watanzania wanaona, wala hakuna anayetangaza, lakini ukweli lazima usemwe, kumpongeza Rais akifanya vizuri sio dhambi, hata wewe ukifanya vizuri watu watakupongeza, ukifanya vibaya watakusema kwa ubaya
 
Chini ya Uongozi wa Rais Samia Baadhi ya mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya elimu hadi Aprili 2022; -Kurejesha wanafunzi wa kike 3,333 masomoni kupitia mpango wa kurejesha wanafunzi; -Kuendelea na ujenzi na ukarabati wa vyuo vya VETA katika mikoa 25 ya Tz
 
Kabisa, kazi inafanywa kubwa saana Nyabukika
 
M
Mpuuzi mkubwa, hata wakoloni walileta reli, shule, makanisa na barabara, mfumuko wa bei sisi ndiyo tatizo letu
Mfumuko wa Bei haujaletwa na mh Rais Bali umetokana na Vita vya huko ukrein, Na katika kulikabili Hilo ili kuleta unafuu katika maisha ya mtanzania mh Rais anatoa Ruzuku katika secta muhimu ambazo zinagusa maisha ya watanzania wengi na Ni injini ya uchumi wetu, Kama alivyofanya kwenye mafuta na mbolea.
 
Endelea kujipendekeza utaonekana tu ila moyoni unaujua ukweli!! ,huku mwanza biashara nyingi zinafungwa bora hata kipindi cha magufuli,umeme unakatika kila siku tanesco wanaogopa kutangaza rasmi kuwa kuna mgao,pesa haina thamani elfu 10 ya sasa haina tofauti na elfu 5 pesa nyingi iko mtaani lakini haina thamani,mitaa ni michafu watu wanatiririsha maji ya chooni kwenye mitaro na hakuna anayefuatilia yaani kifupi watendaji wa serikali wako usingizini na hii yote inachangiwa na rais asiye chukua hatua,yupo kama pambo ikulu.TUMERUDI KWENYE ZAMA ZA KUJICHOTEA UNACHOKIONA MBELE YAKO ILIMRADI UKO KWENYE NAFASI.Maisha ni magumu kifupi hatuna rais mwenye uwezo wa kukemea maovu kwenye hii nchi kwa sasa
 
Kabisa mkuu ibanezafrica, Tanzania inafunguka, Wafanyabiashara wengi sasa wanasafiri, hotel na kumbi zilizokuwa zimefungwa kwa kukosa wateja sasa zinafunguliwa
Watanzania ni wepesi sana kusahau...
Wote tulikua tunalia mtaani hela hakuna!
Mara wasiojulikana!
Uhuru wa habari....
Bunge likakata matangazo live....
Wakulima wa korosho...ufuta...tumbaku...chai...pamba...dengu...hoi
Viongozi wa upinzani na vyama vyao walikuwa wanashinda mahakamani ..
Watu tukashindwa somesha watoto int school...
Biashara kutoka ikawa mbinde
Madalali wakapoteza ajira..
Meli zikapungua bandarini....
Matajiri wakabanwa na wengine kukimbia....
Hakika Vyuma vilikaza kweri kweri..


Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…