Mnaobeza mafanikio ya Awamu ya Sita, zungukeni Tanzania muone mafanikio ya Serikali ya Rais Samia katika utekelezaji wa miundombinu


Tupe hela ya kuzunguka nchi nzima kwenye hiyo miradi, ili na sisi tuje tusifie kama ww.
 
Yaani wewe unaonekana kutumwa na ushapokea ujira tayari. Ni sawa hatukatai ila unaposema nchi mzima ni uongo. Mimi kule village kwangu barabara mvua ikinyesha hata bodaboda haziendi. Shule niliyosoma kwenye hizi pesa ya COVID hakuna Darasa hata tundu ya choo iliyojengwa Kwa kupata fungu Hilo.

Dar ninakoishi barabara ni mbovu haisemekani na Kuna Mbunge (Kawe) wakipewa mil. 500 hatuoni hata moramu yenyewe!
Sasa unapoleta hadithi za nchi mzima ni shida.
 
Unajua nyie chawa ni watu wasahaulifu sana. Baada ya JPM (rip) kufariki na watu kuanza kuelezea mafanikio yake, mliwaambia legasy haitetewi, bali hujitetea yenyewe! Well, sasa mko bize na uchawa wenu kutetea mafanikio ya awamu ya 6 (btw, sina tatizo na rais Samia), kwa nini msiyaache hayo mafanikio yakajionyesha yenyewe huko huko watu waliko? Kwa nini mnatumia nguvu nyingi hivyo kutaka kuwaaminisha watu?
Mwacheni Rais afanyekazi, uwezo na mafanikio yake vitaonekana kwa watu.
 
Watu wajinga kama wewe mpo wengi sn, Zanzibar wao wanaishi sayari gani au wao vita ya Ukraine haiwahusu?
 
Mpuuzi mkubwa, hata wakoloni walileta reli, shule, makanisa na barabara, mfumuko wa bei sisi ndiyo tatizo letu
Tofautisha mfumuko wa bei (inflation) na kupanda bei bidhaa (price hike). Baada ya hapo ndipo uje uandike humu siyo kutapika pumba kama Bata anakunya
 
Acha utoto UmkhontoweSizwe, Kama kuna mazuri waacheni watu waongee, mbona nyie mkikosoa watu hawalalamiki.
 
Watanzania wako huru, ndio maana hata wewe uko huru kutoa maoni yako bila shida
 
Mkuu Vyura99tu data haziongopi, wapi nimesema uongo hapo? Hakuna mtoto wa Kitanzania anayesomea chini ya mti kwa sasa, yawezekana Shule unayosema ni kweli haijapokea( Japo sina uhakika kuwa ikose fedha IMF, EP4R, Umaliziaji wa maboma, etc ) lakini pia Shule zinapewa kutokana na mahitaji, kuna shule zina excess ya madarasa na miundo mbinu ya vyoo..
 
Rais Samia ni mtu wa vitendo sana kuliko sifa, ni mpenda haki na siyo mtu wa DHULUMA. Kikubwa anafanya kazi zake vizuri kwa ajili ya wananchi wa Tanzania. Wala hafanyi kwa ajili ya kutaka abakie madarakani mwaka 2025.

Kama hatutamtaka mwaka 2025 naamini atakaa pembeni lakini hawezi kufanya ule UHAYAWANI wa Magufuli wa kuiba chaguzi za vitongoji za 2019 na uchaguzi Mkuu wa 2020. Tuko mikono salama na Rais SSH

Wakati ndiyo utasema tusubiri 2025
 
Unavyoweweseka kuikandia serikali ya Mama yetu SSH utadhani kama kweli ni mpinzani haswaa wa utawala huu kumbe ni kanyaboya lililo kwenye bahari kusubiri mpumbavu anasemo kisha kuzama naye majini [emoji16]
Hata wew ? Kumbe umekufa macho
 
Ukiitembelea Tanzania utashangaa nakubali. Na mshangao wenyewe ni wa ajabu kidogo...watu hawapewi kulingana na mahitaji yao bali kwa kujuana.
Vipo vituo vya afya vinazidi hospitali za wilaya nyingine. Zipo wilaya hazikugusa vituo vyake vya afya wala hospitali zake ila wamepewa mpyaaa..kubwaaaa.
Kuna sehemu hawana hospitali za wilaya ila wamelazimika kuomba kutumia hospitali za dini kuziba mapengo.
Mfano.
Mkoa wa kilimanjaro...
Rombo hospitali ya wilaya ni ya dini
Moshi vijijini...hawana...
Moshi mjini...hospitali ya wilaya ya dini
Siha?
Ukiona kinachoita kituo cha polisi cha wilaya...toka Rombo hadi siha utashangaa....
Na ni wila za muda mrefuuuu
Halmashauri hazi majengo yake nk

Kwa kifupi taasisi zote za serikali hazina majengo yanayofanana na wilaya nyingine...tena mpyaaa...

Sent from my SM-N986B using JamiiForums mobile app
 
Watanzania wako huru, ndio maana hata wewe uko huru kutoa maoni yako bila shida
Ni kweli wako huru ndio maana wanatumia ID feki ila walioshindwa kustahimili njaa kama wewe inabidi wajianike ile walau watupiwe hata ka-mfupa.
 
Hivi kumsifia kila Rais kila wakati, mara kwa mara haikuwepo wakati wa Nyerere, Mwinyi, Mkapa nafikiri hata Kikwete. Ilianza sana wakati wa Mgafufuli kwa sababu ya kuogopa kutunguliwa. Nafikiri walimsoma kwamba alipenda kusifiwa, hivyo ikawa kama gia ya kupata kibali kwake. Sasa hivi inasikitisha sana, kwamba kila jambo ni kumtaja Rais, yaani serikali anayoiongoza haina kazi. Tanzania uongozi ni kazi kweli kweli.
Tambua kongozi kwamba kibali chako si kutaja taja jina la Rais bali ni utendaji wako.
Rais usifunikwe na sifa zao, wengine wana unafiki ndani yao. Usilewe sifa za wapambe wako, wanajua wasipokusifia hawatabaki wanaogopa, mtu mwoga ni hatari sana, anaweza kufanya jambo lisliotarajiwa. Tambua kusifiwa sio kupendwa. Chunguza na watambue wenye moyo wa uzalendo hasa eneo la rushwa.
Kila mmoja anapenda kusifiwa lakini ikae kwa utaratibu na hekima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…