Mnaofanya mazoezi ya kukimbia kuna mambo mnadanganya

Mnaofanya mazoezi ya kukimbia kuna mambo mnadanganya

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Kuna jambo nimekuwa nikilifikiria na kubaki kushangaa sana. Ni hii tabia ya wafanya mazoezi ya kukimbia. Unakuta mtu anapost kaenda mazoezi ya kukimbia na kudai kamaliza labda 13km kwa kukimbia.

Kumaliza 13km sio tatizo kwa watu wenye mazoezi ila kukuta mtu kibonge na minyama ya kutosha kapost kumaliza 13km kwa kukimbia inaleta ukakasi sana.

Kwa msiojua ni kuwa mazoezi ya kukimbia sio kitu cha mchezo mchezo. Yaani hata kumaliza 1km bila kusimama wala kutembea inastahili pongezi.

Tuache kudanganyana kwenye mambo serious. Cha kushangaza wengi wanaojidanganya huwa hawapungui!

Inauma sana kuona unamaliza 2km huku roho ikikaribia kuacha mwili mara ghafla unaona kibonge kapost kamaliza 13km. Huu sio uungwana na ni kukatishana tamaa.
 
Mkuu mtu akikwambia kaenda km 13 bila ushahidi (GPS or any fitness app) au kufanya makadirio ya km tu hapo anakuwa anajidanganya mwenyewe

Wakimbiaji wengi hasa wazoefu wanatumia saa zenye GPS au simu (smartphone) etc.

Saa zenye GPS ziko more accurate kwa umbali kupima kuliko saa ambazo hazina GPS , pia simu baadhi kama infinix etc huwa zinatabia ya kuvuruga umbali uliokimbia..unaweza kuta mtu huyo amekimbia km 5 inamwandikia 13 ..Ni suala la uelewa kwa mtumiaji.

Wakimbiaji wengi wazoefu wanatumia APP zenye ufanisi kama STRAVA hii ni common worldwide it's like social network...kuna app zingine sio nzuri kwenye kurekodi

Pia kuna matatizo ya GPS kuvuruga km na route ya mtu anayofanyia mazoezi..maybe hayo maeneo sio mazuri

Pia kuna suala la uelewa mdogo kwa mtu mgeni ambaye anaanza kukimbia na kutumia hivi virecord mwendo.

Mwisho kabisa.mtu kukimbia pekee
Haimfanyi kupungua mwili..kuna mambo mengi yanayokwamisha hasa ulaji wa chakula.
 
Kuna jambo nimekuwa nikilifikiria na kubaki kushangaa sana. Ni hii tabia ya wafanya mazoezi ya kukimbia. Unakuta mtu anapost kaenda mazoezi ya kukimbia na kudai kamaliza labda 13km kwa kukimbia.

Kumaliza 13km sio tatizo kwa watu wenye mazoezi ila kukuta mtu kibonge na minyama ya kutosha kapost kumaliza 13km kwa kukimbia inaleta ukakasi sana.

Kwa msiojua ni kuwa mazoezi ya kukimbia sio kitu cha mchezo mchezo. Yaani hata kumaliza 1km bila kusimama wala kutembea inastahili pongezi.

Tuache kudanganyana kwenye mambo serious. Cha kushangaza wengi wanaojidanganya huwa hawapungui!
Mm nimepungua
 
Back
Top Bottom