Mnaofurahia kuporomoka kwa Dolla ya Marekani hamjui mchezo wa thamani ya fedha na ni nani anayechezesha mchezo huo.

Mnaofurahia kuporomoka kwa Dolla ya Marekani hamjui mchezo wa thamani ya fedha na ni nani anayechezesha mchezo huo.

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Hata kwa maneno ya Governor wa Benki Kuu ya Tanzania kuwa dola itaanza kupanda tena kuanzia February 2025 unaweza kujua tu kwamba kila kitu kipo kwenye control. Wasilolijua watu wengi ni nani hasa huyo yupo kwenye control ya haya mambo. Si mwingie ni Mmarekani mwenyewe!

Kuna wakati nchi inaamua kushusha thamani ya fedha yake kwa makusudi maalumu kulingana na financial projections zao, kuna kitu wanakuwa wamekiona mbeleni na wanafanya hivyo kimkakati na kwa faida kubwa baadaye.

Kumbukeni kwamba fedha ni commodity pia inaweza kuuzwa na kununuliwa; ukiwa unauza mahindi yako kwa bei kubwa sana watu wanaweza kuacha kununua mahindi yako na kwenda kwingineko, sasa unafanyaje? Unashusha bei ili watu wanunue kwa wingi na utapata faida zaidi sio?

Hata Governor wa BOT anaweza kufanya kitu kushusha dola mpaka ikawa USD 1=TZS 100 lakini ajue anafanya nini na atafaidika vipi na hilo jambo.

Ukitaka kuruka juu unaanzia mbali kuvuta kasi. Ndivyo wanavyofanya wataalamu wa fedha wa Marekani. Mtu asikudanganye eti ni utalii umekua, au sijui ni uchumi wetu umesitawi, sijui et Mama anaupiga, la hasha. Kuna wakati Italia hela yao iitwayo LIRE ilikuwa ya kutupa, TZS 1 ilikuwa LIRE 2000, walichofanya ni kuachana nayo na kuamua kufanya EURO kuwa ndio fedha yao, hadi leo! Lakini je ungeweza kufananisha uchumi wa Italia na wa Tanzania? Hata kidogo.

Sana sana kabla ya 2025 kuisha tujiandae kuona figure kama hizi; USD 1=TZS 3,800.
 
Back
Top Bottom