Mnaofurahia Mikopo, Sri Lanka pia iIianza kama sisi

Mnaofurahia Mikopo, Sri Lanka pia iIianza kama sisi

Huo ndio Ukweli mchungu kuumeza, lakini usiokwepeka.

Sio ujasiri wala ushujaa kwa viongozi kutembea mkifurahia mikopo na kujipiga kifua mbele ya wananchi majukwaani,kama vile ni jambo la kheri na kishujaa kukopa kopa bila Dira ya kitaifa.

Mnapaswa pia kutoa elimu kwa wananchi, juu ya madhara ya mikopo hiyo kwa uchumi wa nchi.
Ili wananchi waweze kujiandaa kisaikolojia huko mbeleni.

Kwa sababu nyinyi viongozi mnakwenda kukopa huko,lakini walipaji wakuu ni wananchi na vizazi vyao.

Kwa nchi iliyojaaliwa raslimali kama hii ya Tanzania.

Hatukupaswa na hatustahili kushinda mguu na njia kwenda kutembeza mabakuli huko Duniani,sambamba na nchi maskini wa kweli ambazo zipo Africa na kwingineko.

Wakati huo tukiziacha mali zetu zikichotwa kwa mkono mwingine na hao hao wakopeshaji,kwa msaada wa baadhi ya wenzetu wachache kwa manufaa binafsi.

Kwani mifano hai ya mikopo hiyo na madhara yake kwa ushamiri wa taifa tunao.

Mfano wa karibuni kabisa ni huu unaoendelea huko Sri Lanka [emoji1224].

Walikopa hadi wakanyanganywa Bandari yao kuu.

Na sasa wanaelekea kupoteza uhuru wao kama taifa.

Ni baada ya hao hao IMF watalapoitangaza Sri Lanka kama nchi iliyofilisika.

Bado mfano mwingine wa madhara ya mikopo uko Lebanon [emoji1146].

Kwa hiyo CCM wakati mkisifia ukopaji muelewe jinsi mnavyoelekea kulitumbukiza taifa hili tajiri la raslimali,mikononi mwa wakopeshaji.
View attachment 2297136
Bibi yuko busy kukopa, mzigo ukija huku wajanja wanakula kwa urefu wa kamba zao na kujipimia mpaka kuvimbiwa. Ee Mola tuepushie mbali na hili janga.
 
  • Thanks
Reactions: nao
"Af" "hawamu" "Samahia" "hualisia"

Kama hayo tu yanakutatiza kuandika basi huwezi jua ninachokimaanisha.
Wewe endelea kushikiwa akili.

Halafu kwako na wenzako mliozowea kutumwa mnadhani kila mtu humu ni mtumwa?

Change your Mindset Please!
Change your mindset,...Tena hapo ndio umempoteza kabisa, hawa ni "Ndiyooooooooo...." WAMEJAZANA bungeni na mitaani ambao utafiti wa TWAWEZA ukionyesha asilimia kubwa ya wafuasi wa chama hicho ni wazee, masikini na mbumbumbu. Mada yako hii muhimu hatakaa aielewe.
 
Hii ndiyo pointi ya muhimu kufanyiwa kazi.

Mkuu kuwa na miradi mingi Ndio maana kunakuwa na upigaji mwingi na hata miradi kutelekezwa kisa hela Hakuna kumbe wameiba hao hao wanaojiita wazalendo na viongozi wenye kelele

Tunataka kila kitu kwa wakati mmoja tukafanywa mazuzu toka awamu ya nne wakiimba Kigoma itakuwa kama Dubai

Mara Moro itakuwa sijui nini Yaani kujivisha vitu tusivyoweza ( sio kuwa hatuwezi) Bali wanaiba zote kabla hata ya foundation
Hata tuimbe kuwa tuna utajiri ila bila kuacha wizi utajiri tutausikia nje tu
 
hii mikopo imezidi.
tunajisifia kukopa aibu sana!

iwapo wakiitumia mikopo hii kimkakati kujenga miundombinu ya reli (SGR) na kununua vichwa vipya vya treni na kumaliza Bwawa la umeme la Nyerere ni sawa ila wakiifisadi tu bongo itakuwa next SrI Lanka! hilo liko wazi kabisa wala haihitaji digrii kuliona!

Wabongo nao wanasubiri kwenda Magogoni kuogelea na kubanika tausi!

Mama anapaswa kufuatilia binafsi matumizi ya hii mikopo kwa kwenda field kuona kwa macho matumizi yake na sio kusubiri kuletewa ripoti mezani na Singida Big Stars aka Yanga B guy (Magulu)

Nina hakika Bimkubwa anajua wabongo tuna digrii za wizi na ufisadi!

Nina hakika Bimkubwa anajua kupitia ripoti za CAG kuwa watumishi wengi wa serikali yake hawana aibu wala huruma na pesa ya serikali, Bimkubwa akiwachekea watamuangusha na kumkana siku wazungu wakifuata pesa zao!! Asisejesema hatukumwambia!!

Kukopa siku zote ni sherehe kubwa ya harusi ila kulipa ni matanga na unyonge!!
Unayoyasema au kushauri yalimpiga knock out Ndugai.
 
Kama pesa zinazokopwa zikitumika kwa uangalifu mkubwa bila ubadhirifu wowote tija ya hiyo mikopo itaonekana, lakini kwa uzoefu wa hapa bongo pesa huwa zinafanyiwa hesabu chafu ! Na kibaya ni kile kitu kinaitwa Kazi na Bata !! Pesa ya serikali huwa wengine wanaona kama vile ni halali yake kuliwa tu !!
Huwezi kukopa ukaingiza kwenye barabara ni mara mia uingize kwenye kilimo kuboresha uzalishaji na tija
 
yani nye ningewaona wa maana sana ka kuhoji kwenu kungeanzia kwenye 1.5 trilion na makrokocho mengi ya awamu ya Tano kinyume na hapo mnaonekana wahuni tu na chuki zenu kwa samia
Hatutaki kulinganisha Nani kafanya makosa zaidi na Nani kafanya makosa kidogo !! Tunachotaka ni kujitahidi makosa yanayoweza kuepukwa yaepukwe !! Sio kwamba kwa kuwa Fulani alifanya hivi basi ni lazima na mwingine afanye vile vile!! Hatutaki mashindano ya ya kufanya makosa !!
 
Ww kwa akili yako unahisi ivyo vyote vinaweza kuendesha nchi iwatengenezee miundombinu ilipe mishahara na hapohapo iwapunguzie gharama za maisha na kulipa Kodi mataki muwe mnafikilia kabla ya kusema

Wanaokukopesha wao wanatoa wapi acha kulemaza akili yako broo aah samahani nimejikuta nimeguswa na pumba zako una negativu thinking
 
Back
Top Bottom