Atakua na nyumba nyingi huyo jamaa.
Masikini/choka mbovu mwenye kuishi kwny ka-banda ka-mbwa ka kupanga huko uswazi hawezi kusahau nyumba yake anayoijenga kamwe.
Mkuu usipende kubisha jambo ambalo hujawahi kukutana nalo ktk maisha ya duniani. Pengine mtoa post ameshindwa kueleza vizuri tukio lilivyo Lakini ni kweli baadhi ya watu wanaokabidhiwa nyumba kulinda sio watu wazuri. Zipo nyumba nyingi hadi leo zinamilikiwa na walinzi wa kimakonde na wenye nyumba zile hawajulikani walipo. Na wao kujimilikisha kama ni zao.
Ipo nyumba moja Magomeni nyuma ya police Magomeni, Ile nyumba tangu miaka ya 1980 hadi leo ipo vile vile, Ilikuwa inaishi family fulani ya Mzee wakimakonde. kila mtu alijuwa kama ni mlinzi na wenyewe hajulikani. Ilikuwa nyumba nzr sana na mjengo wa kizungu na bati fulani za design ya pekee kabisa, inaonyesha mwenye nyumba ile alikuwa na nguvu sana kipindi kile.
Lakini hakuna ambaye aliyekuwa anamjuwa mwenyewe zaidi ya yule babu mlinzi pekee. Tangu 1980 mwenyewe hajawahi kukanyaga pale kwenye nyumba hata yule mlinzi alipokufa miaka ya 2000 bado mwenyewe hakutokea. Mzee alipokufa, wakaibuka watu wanaojuwa history ya nyumba ile wakiwa na documents fake.
wakawatingisha family ile ya mlinzi na kusema nyumba ni yao. Walipoulizwa miaka yote mlikuwa wapi? Jamaa akasema
kwamba miaka yote alikuwa ng'ambo kakimbia uhujumu uchumi kipindi cha nyerere. Miaka ile ilikuwa mambo ya azimio la arusha na mafisadi kupokonywa mali. Sasa amerudi anataka nyumba yake.
Jamaa akiwa na documents zote za nyumba.
Ile family ikalipwa kiasi cha pesa fulani kama malipo ya baba yao kulinda nyumba hiyo kwa miaka yote. wakahamishiwa kinondoni Moscow, Jamaa wakaanza ukarabati wa nyumba. Baada ya mwezi nyumba ikapigwa stop na serikali. Hilo ni baada ya kugunduwa kuna utapeli wa umiliki halali wa nyumba ile. Hadi leo nyumba imezungushiwa mabati ipo vile vile bado mwenyewe halisi hajulikani.
Aliyekuwa anamjuwa mwenyewe ni yule mzee mlinzi wa kimakonde pekee. Haya mambo ya uchawi na ulozi wa sahau nyumba au shamba yapo mkuu. Kinachofanyika ni mlinzi kukupiga kijini sahau au unapigwa kijini usingizi, Kukufanya uipuuze nyumba yako, hata usiimalizie tena na yeye aendelee kukaa maisha yote kwenye nyumba ile.
Kila ukikumbuka kwenda kwenye nyumba unasema utaenda kesho, kila siku utakwenda kesho na hufiki wala hufanyi chochote cha maendeleo pale ndani, miaka inakatika tu. Na hata siku ukikumbuka kufika pale,,zile gharama za kumtoa mle ndani ni kumjengea mlinzi nyumba ingine aishi.
Dunia ina mambo mengi sana usiyoyajuwa.
Kama bado hujakutana na jambo basi usikatae lolote jipya unalosikia.