Mnaojenga nyumba, kuweni makini na watu mnaowaomba wawalindie nyumba zenu

Wakati mwingine ni uvivu tu wa kutingwa na majukumu ya kila siku......na kwa bahati mbaya siku unayotaka kwenda ndio siku ya kupumzika na mwili umechoka........


Uvivu au uchovu huo uwe kuanzia Januari hadi December? Mwaka wa kwanza, wa pili, tatu na kuendelea?

Cha ajabu unaweza kuta kama una eneo lingine la mbali ambalo hujarogwa utajikuta kule mbali unaendaga lakini hapo karibu unaparuka!
 
Wengine wanamashamba makubwa makubwa bagamoyo na mikoani wamepanda mazao kama vile nazi na maembe lakini hawafaidiki nayo wenyewe wananunua nazi kama wengine mtaani na maembe kama wengine wasokuwa na mashamba[emoji108][emoji108]

Waangalizi wa hayo mashamba wanapiga hela ile mbaya!
 
Atakua na nyumba nyingi huyo jamaa.

Masikini/choka mbovu mwenye kuishi kwny ka-banda ka-mbwa ka kupanga huko uswazi hawezi kusahau nyumba yake anayoijenga kamwe.
Shukuru kwamba hujawah kurogwa.dunia ina mengi Zaid ya uyajuayo
 

Mkuu tunaomba mrejesho wa safari yako kama ulifanikiwa kwenda
 
Bagamoyo mwisho[emoji16][emoji16][emoji16].
Kila dalali ana mganga wake..
Unaweza ukauziwa makaburi na ukatoa hela

[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]mkuu umenichekesha sana

Kunywa moja apo nakuja kulipia
 

Hii kiboko
 
TruthLover anasema

Hapo umakini wa kibinadamu hautasaidia lolote.Yesu hakuja duniani kuzurura. Alikuja akijua fika tunamuhitaji sana,hasa kwa mambo yaliyo nje ya uwezo wetu wa kibinadamu kama haya.

Haya sio maneno ya kupuuza hata kidogo. Ima unaamini uchawi ima lah!
 
Nimechekaa sana, yaani usahau nyumba yako? Basi jamaa mambo yalikuwa super au alikuwa chizi

huwa wanarogwa, mother yangu pia amewahi kunisimulia story kama hii ilitokea Kanda ya ziwa, ila utofauti ni kidogo
yule bwana alikuwa anakumbushwa na mkewe kuhusu nyumba ila anamshushia mkewe kichapo hatari,kumbe alirogwa asahau nyumba yake ambayo ilikuwa imeshakamilika kila kitu mpaka umeme na maji
 
nina jambo langu vikindu na makulunge bagamoyo, sijaenda mwaka wa pili unaenda huu, ngoja nijitahidi kufika isje kuwa kijini msahaulifu kaniingia...
 
Hayo mambo ni huko kwenu tu bara ambako hakuna ubinadamu, hapa kwetu ni shwari hakuna kitu namna hiyo
 
Hapo hapahitaji umakini! Utakaaje miaka yote hiyo bila kwenda kutembelea eneo lako?
 
yaani nimesoma hii habari yako mwisho nimekuona mjingasana, unajaribu kuleta wazo lako hapa lakini tatizo unalo mwenyewe halafu unasingizia kurogwa sijuw upumbav gani yaani watu kama nyinyi wenye theory mgando kama hii mimi nawakwepa sana, wewe endelea bora endelea na mawazo yako finyu ukiamini kuna jambo baya umefanyiwa. poor thinker
 
Imenitokea hii kitu mkuu Maisha sometimes usipokuwa makini umekwisha.... Kipindi nasoma o-level 2009 mzee alinipanga ameanza kunishushia mjengo mungu ni mwema mpaka 2012 akanipeleka kweli kitu kimesimama nakumbuka kauli yake akaniambia nategemea hapa ndipo utapokuja kuanzia maisha yako sasa katika harakati za finishing kuna jamaa(mmoja wa mafundi) alikuwa na familia mke na watoto wawili waliomba kukaa pale kwa muda huku finishing ikimaliziwa kiufupi huwezi amini since 2013 nyumba ilisahaulika kiujumla tukawa tunawekeza kwenye mambo mengine nimekuja kushtuka mwaka jana ndio kupambana namaliza huu mwaka nikiwa nahamia kwenye jengo langu lililotelekezwa katika harakati ya safari ya maisha.Binadamu Ishi Naye Kwa Akili. Asante Sana Mzee Wangu Mungu ni Mwema[emoji120]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…