Mnaokaa Uswahilini (Wilaya ya Temeke) Mungu awafanyie wepesi ndugu zangu. Jana machozi yalinitoka

Mnaokaa Uswahilini (Wilaya ya Temeke) Mungu awafanyie wepesi ndugu zangu. Jana machozi yalinitoka

Nimelia sana kujiita wa ilala wakati unamiliki buku benga tu.......ila umaskini wa wananchi hasa wa kawaida unazidi kuwa wa kutisha huku watu fulani wanaojiita wanasihasa wakizidi kuwa na ukwasi wa kufuru.
Ulitaka nijitangaze kuwa niliwasaidia wale watoto??..
 
No matter unakaa TMK au Ilala ila kitendo cha OP kukosa hata 500 ya ziada mfukoni kulikuwa hamna haja ya kuanzisha huu uzi 😅🚮🚮

Wait, una uhakika hayo machozi yalikutoka kwaajili ya hao watoto kweli?? 😂
Punguza makasiriko mtoto wa Temeke..
 
Uswahilini vyakula Virgi mia 500 inawatosha watoto. Sasa ulitaka wapewe bakuli la ugali na maharagwe siyo.
 
Kuna ukweli ila naona kama hakukua na haja ya hiko kichwa Cha habari kwenye neno Temeke, asilimia kubwa kila wilaya uswahilini maisha ni hayohayo mkuu
 
Mimi ninakaa Wilaya ya Ilala. Jana nilikuwa Wilaya ya Temeke (mtoni kwa Aziz Ally) nilishuhudia mida ya mchana badala ya mama kuwapikia watoto (watoto walitoka kucheza wakaja kulalamika njaa inawauma) akawapa 500 wote wawili wakanunue bagia na askrimu (ice cream) na ndio imetoka hiyo mpaka Usiku, kulingana na maelezo ya mwenyeji wangu. Sema na mimi nilikuwa majalala, nilibakiwa na nauli tu 2,000, laiti kama ningekuwa na kitu chochote ningeweza kuwaongezea hata 500 nyingine aisee.

Kama hauna pesa ya kumsaidia mtoto masikini, basi mkumbuke hata wakati wa sala au swala.

Daah, uswahilini panatisha wadau, hususan kwa watoto wadogo.

UPDATE LEO JANUARY 28, 2025 SAA 15:50
======
Nimegundua watanzania wengi wanapenda sana kusaidia wenye uhitaji kisha kujitangaza.

Laiti kama ningesema niliwasaidia wale watoto, mngenirushia tena mawe "KWA HIYO NDIO UMEKUJA KIJITANGAZA JF ILI UONEKANE UNA ROHO NZURI??" Hahahahaa wabongo wengi jau sana..
Watu hawa hawa Miaka mitatu iliyopita waliambiwa "fyatueni tu" kila kitu bure!

Huku Temeke, Mbagala Gongo la Mboto , mwanamke wa miaka 23 unakuta tayari ana watoto zaidi ya wattatu.
Kama tunataka wajihudumie, basi tuwaambie kipindi cha kampeni wakiwa wamekusanyika kuwa sera ni:-
1. Elimu si bure.
2. kujifungua ni hela.
 
Polee sana mkuu nakuelewa ulivyo jisikia ili urudi tena ukasaidie hao vijana.... mtaani kwenu na washkaji zako azisha kampeni ya michango then mnaenda kusidia hao vijana! Bdo unaweza kuwa msaada kwao
Nauli yake tu ilikuwa mbwembwe, itakuwa kusaidia wengine..!!
 
Back
Top Bottom