Mimi ninakaa Wilaya ya Ilala. Jana nilikuwa Wilaya ya Temeke nilishuhudua mida ya mchana badala ya mama kuwapikia watoto (watoto walitoka kucheza wakaja kulalamika njaa) akawapa 500 wote wawili wakanunue bagia na askrimu (ice cream) na ndio imetoka hiyo mpaka Usiku, kulingana na maelezo ya mwenyeji wangu. Sema na mimi nilikuwa majalala, nilibakiwa na nauli tu, laiti kama ningekuwa na kitu chochote ningeweza kuwaongezea hata 500 nyingine aisee.
Kama hauna pesa ya kumsaidia mtoto masikini, basi mkumbuke hata wakati wa sala au swala.
Daah, uswahilini panatisha wadau, hususan kwa watoto wadogo.