Mnaolalamika na kubeza Mbowe kwenda kuonana na Rais, Mlitaka afanye nini?

Jubilani!

Kwani hukusikia walichoongea!
 
Sabaya naye asamehewe na kufutiwa mashataka yoote, kisha na yeye akaribishwe ikulu kwa mazungumzo na SSH
 
Kutoka kwa Mbowe kumeharibu dili la michango
 
Mna kelele tu.

Mbowe kaachiwa huru, katoka nje ya mahakama amefuatwa na vyombo vya habari akawaambia kuna muda wa kuongea na muda wa kunyamaza, akatoa na kifungu cha maneno ya biblia toka kitabu cha muhubiri.

Hii ndio hekima ya Mbowe ambayo wengi wenu na mnaowaunga mkono hawana, mmezoea kupelekwa kwa mihemko halafu mwisho wa siku hata mkiambiwa muandamane na hao mnaowapenda bado hamuonekani barabarani, mnajificha jf na kujitutumua kwa kila aina ya maneno ya kujimwambafy kumbe kiuhalisia mko weupe tu, hamna kitu.

Mbowe anajua kucheza na akili zenu, ameshajua anaongoza wanachama wa aina gani, ndio maana huwa anachanganya mbinu zake ili kuendana na hali ya mambo iliyoko mbele.

Ngoja aje yule atakaewaambia muandamane tuone kama kuna siku mtathubutu kuingia barabarani, hawa viongozi kimsingi wanachoka kwa kuongoza wajuaji wa sampuli yenu wasiojua washike lipi, kama mngekuwa na misimamo hii mnayoionesha huku jf kule field CCM leo ingekuwa historia, wengi wenu vitendo sifuri.
 
Tatizo amewahi mno kwenda ikulu ilibidi apimzike na kujipa muda kutafakari ndio aende. Kwa sasa bado ana wenge la magereza na akili bado haijakaa sawa.
 
Kwa mtazamo wangu Mbowe alistahili kujipa muda wa kuonana na rais, na sio chini ya 24hrs toka atoke gerezani. Maadam alishakwenda hakuna namna ya kuzuia hilo tena. Cha muhimu kwa sasa ni kufuatilia mwenendo wake wa kisiasa baada ya kukutana na rais. Na akianza siasa za kujikomba tu ajue hatakuwa na nafasi kwetu.
 

Akiahidiwa upatikanaji wa hiyo katiba atakuwa na sababu gani ya kuandamana? Kumbuka hii ndio mara ya kwanza kukutana na rais face to face toka Samia awe rais, tena wakawa na kikao cha faragha. Uzuri tuna uwezo wa kuusoma mchezo na kujua nini kinaendelea.
 
Kusema kweli na nisiwe mnafiki Mimi amenikera Sana na nimechukia.

Sina mengi ya kuandika ila huo ndio ukweli wangu.

Sitakuja kufuatilia wala kuchangia siasa au wanasiasa wa Tanzania tena!
 
Mkuu, hao wanaopinga ni kama washabiki tu wa timu za mpira hawaendi mbali katika kuchambua mambo.
Faida ni hizi;
Ameandaa njia ya amani katika harakati zake kisisa. Sababu watu wote wanaotesa wapinzani wako chini ya raisi ambaye amepatana na Mbowe
Pili kitendo cha raisi kuonana na Mbowe kinamhakikishia mbowe usalama wake na chama chake
Tatu waliomtesa Mbowe hawataweza tena kirahisi kurudia uovu wao kwani watajua kuwa yuko level nyingine, wataogopa na hivi Mbowe na chama chake watajiimarisha bila hofu kubwa
Nne machoni mwa raia Mbowe na rais wataonekana watu wa amani wasiopenda visasi sio watu wa jino kwa jino na itaifanya siasa ziwe za kistaarabu zaidi na kuifanya Tanzania iwe mahali salama zaidi kuiishi na maendeleo yatashuhudiwa
Na faida nyingine lukuki....
 
Hao atakutana nao siku zote. Kwa rais ni awal kul
 
Sidhani kama Mbowe alikuwa na choice nyingine. Infact inaonekana aliyeomba audience ni Mbowe mwenyewe.

Wengi wa wanaobwabwaja humu bila shaka wangefanya alichofanya Mbowe ma wasingeweza kuhimili hata 20% tu ya madhira aliyopitia. Give this gentleman a break..
 
Hii ni uthibisho kesi ya kubumba Ingekuwa na ushahidi wasingeifuta uliona wapi kesi mashahidi wote ni police
Hata kama wana ushahidi ila kama kuifuta inaleta faida kwao kwanini wasiifute? si umeona wamefuta kesi na kumwita ikulu wamechukua points zao, labda wewe usiyejulikana na si mwanasiasa na hauna mtu wa kwenda kukuombea kwa rais ukikamatwa ndio hawawezi kukuachia hata kama hawana ushahidi.
 
Underboss, kuna mambo hupaswi kuyachukulia kama akili yako ilivyo tuuu. Kukutana na wanachama hakuna shida, nafasi hiyo iko tu muda wowote.
Kukutana na Rais ni nafasi adimu, na Mbowe alichofanya ni cha maana Sana, maana changamoto zote pale ndiyo pa kuzisema, na kilichojadiliwa matunda yake yataonekana soon.
Siyo kila mtu ni mwanasiasa bali wengine ni uchwara(probably na wewe ukiwemo).
 
Wewe akili huna.

Rais aliekufunga na kudhalilisha na kukufanyia kila baya halafu unaona kukutana nae ni nafasi adimu?

Unatumia kichwa kufikiri ama makalio?
 
Ndio mpunguze shobo kupigania masilahi ya wanasiasa kuliko masilahi yenu, jitu linatokwa na mishipa ya shingo kisa mwanasiasa Mbowe kafungwa ila wananchi wanzake wamejaa kibao huko jela kwa uonevu pia ila hajawahi kutokwa na mishipa ya shingo, lini mwanasiasa ataenda kuongea na rais kwa ajiri ya masilahi yenu au kuomba tu wale ndugu zetu kule jela waliyowekwa kwa uonevu watendewe haki?
 
Kusema kweli na nisiwe mnafiki Mimi amenikera Sana na nimechukia.

Sina mengi ya kuandika ila huo ndio ukweli wangu.

Sitakuja kufuatilia wala kuchangia siasa au wanasiasa wa Tanzania tena!
Akiba ya maneno ni muhimu mkuu. Siasa zina hesabu zake na hazitaki kujihukumu.
 
Kuwa mkweli mkuu, kulala kote sero unasema hivi. Hii ni afya ya taifa zima.
mi ninechokoza fikra tu ukiangalia mbali Samia hana upeo huo, Mbowe ni nguvu na ushawishi wa viongozi wa dini vimemtoa pamoja na mbinyo wa kimataifa hasa maswala ya mkwamo kiuchumi wa Chifu ombaomba, Cheo kinamzidi hakuwa na namna, michadema wsifurahie Udikteta upo wazi sana.

Hivi shushushu wa kule Rondo Lindi kajificha wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…