Mnaolalamika na kubeza Mbowe kwenda kuonana na Rais, Mlitaka afanye nini?

Mnaolalamika na kubeza Mbowe kwenda kuonana na Rais, Mlitaka afanye nini?

Kwa mtazamo wangu Mbowe alistahili kujipa muda wa kuonana na rais, na sio chini ya 24hrs toka atoke gerezani. Maadam alishakwenda hakuna namna ya kuzuia hilo tena. Cha muhimu kwa sasa ni kufuatilia mwenendo wake wa kisiasa baada ya kukutana na rais. Na akianza siasa za kujikomba tu ajue hatakuwa na nafasi kwetu.
Sidhani kama alipokuwa gerezani akili iliacha kufanya kazi na isitoshe mara zote tulizomuona akiwa mahakamani alikuwa ameshika kitabu kwa maana akili haikuwa dormant. Kwenda moja kwa moja Ikulu kunaonyesha yupo fit!
 
Si huyo unaemuita ndie kasema hawez kua mpinzani tena au ni pacha ake?[emoji16]
Kwani alikuwa mpinzani mwaka gani? Huyo Kila siku anajiita CCM Damu halafu aseme ameacha kuwa mpinzani? Hebu Wenye kujua maana ya upinzani waachwe wawe Wapinzani. Siyo Mtu unakaosana na kiongozi Fulani wa CCM halafu unakuja kujiita mpinzani. Wapinzani ndani ya JF wanajulikana, wawe upande wa CDM, CUF au ACT wanajulikana tena Kwa ID zào.
 
Alitakiwa akutane na wanachama kwanza. Au leo angetoa taarifa kwa umma nini aliongea na Rais, na nini msimamo wa chama.
Ukimya wake una maana alitolewa kwa masharti akapelekwa kulishwa maneno na mtesi wake.
Lissu arudi aongoze mapambano Mbowe kafika bei.

Small mind!! Ni mtu gani anaweza kuamriwa kwenda Ikulu na huku akiwa chini ya mhimili huo akakataa?? Mbowe aliandaliwa toka mapema kwa kisingizio cha kuumwa. Hakimu pia alijua ni siku hiyo hiyo alitakiwa kwenda ikulu na ndio maana ya amri “washitakiwa waachiwe huru leo bila kukosa”. Jambo hili zima halikuwa la bahati mbaya - kwenda ikulu sio jambo la ghafla!!! Hakutoka nyumbani kwenda ikulu - uamuzi wake haukuwa huru!!

Lakini kama Mbowe hakutaka kushitakiwa tena kwa kufungua kesi. Akashindwa. Na akatakiwa kujitetea. Yote hayo yalikuwa na lengo la kumwachia huru. Sasa imekuja njia ya mtesi kufuta kesi - ni nini tena ni kikubwa kuliko uhuru??

Watu wa aina yako wangemlaumu hata kama angekwenda nyumbani kwanza. Hata kama angekwenda ofisini kwanza! Watu wa aina yako ni wale wasiojua art of making choices. Wasiojua uwezo wao na mipaka ya uwezo huo!

Ni bahati mbaya umempa uwezo na machaguo mengi Mbowe pia kujali ANGEWEZA au ASINGEWEZA kufanya yapi.
 
Vijana wengi wa CHADEMA wanadhani siasa ni kutanguliza "TUG OF WAR" katika kila jambo.....

#Siempre JMT[emoji120]
Acha unafiki, nioneshe andiko moja tu la Mwanachadema anayejulika humu ambaye amelaumu Mbowe kuitwa Ikulu. Yaani Nyani Ngabu na Gentamycine ni CHADEMA tangu lini?
 
Huo utu huo waupate wapi,kama waliweza waweka ndani mashehe wa uhamsho na wazee wa uhamsho bila ushahidi just kuwakomoa tu sababu Hakuna nguvu za kuwawajibisha kipi washindwe.
Uliona wapi kesi mashahidi wote ni police na police hao wote ni wakaazi wa dar na wengine wamekuwepo kwenye magenge ya wasiojulikana.
Sasa ngoja ukamatwe wewe hata kwa kutokuwa na ushahidi halafu tuone kama kutakuwa na wakushinikiza uachiwe huru kisa hakuna ushahidi.
Huko Jela Mbowe kawakuta kibao walishikiliwa bila ushahidi ila kawaacha wanaendelea kusota hawana mtu wa kuwaombea kwa rais.
 
Small mind!! Ni mtu gani anaweza kuamriwa kwenda Ikulu na huku akiwa chini ya mhimili huo akakataa?? Mbowe aliandaliwa toka mapema kwa kisingizio cha kuumwa. Hakimu pia alijua ni siku hiyo hiyo alitakiwa kwenda ikulu na ndio maana ya amri “washitakiwa waachiwe huru leo bila kukosa”. Jambo hili zima halikuwa la bahati mbaya - kwenda ikulu sio jambo la ghafla!!! Hakutoka nyumbani kwenda ikulu - uamuzi wake haukuwa huru!!

Lakini kama Mbowe hakutaka kushitakiwa tena kwa kufungua kesi. Akashindwa. Na akatakiwa kujitetea. Yote hayo yalikuwa na lengo la kumwachia huru. Sasa imekuja njia ya mtesi kufuta kesi - ni nini tena ni kikubwa kuliko uhuru??

Watu wa aina yako wangemlaumu hata kama angekwenda nyumbani kwanza. Hata kama angekwenda ofisini kwanza! Watu wa aina yako ni wale wasiojua art of making choices. Wasiojua uwezo wao na mipaka ya uwezo huo!

Ni bahati mbaya umempa uwezo na machaguo mengi Mbowe pia kujali ANGEWEZA au ASINGEWEZA kufanya yapi.
Na huu ndio ukweli ni watu wasioelewa tu wanashindwa kufumbua haka kamtego hii plan ilikuepo tu.
 
Sasa ngoja ukamatwe wewe hata kwa kutokuwa na ushahidi halafu tuone kama kutakuwa na wakushinikiza uachiwe huru kisa hakuna ushahidi.
Huko Jela Mbowe kawakuta kibao walishikiliwa bila ushahidi ila kawaacha wanaendelea kusota hawana mtu wa kuwaombea kwa rais.
Lkn at the end watatoka tu jela sio mwisho wa maisha.
Afrika jela unakaa kwa sababu mbili.
1.Wewe ni masikini huna pesa ya kuhonga kununua UHURU wako.
2.Unaweza ukawa na pesa lakini umekosana na wanasiasa au wenye mamlaka nature ya mswahili ni visasi so unawekwa jela kukomolewa.
Nadra Sana kumkuta tajiri jela afrika nje ya point hizo mbili
 
Amani Itawale kwenu Nyote!

Jana nahisi ilikua moja ya siku atakazozikumbuka Mwamba FAM kwenye Maisha yake hasa juu ya kesi iliyokua inamkabili yeye na wenzake ambapo DPP jana Aliamua kuifuta kesi hio au aliamua kutokuendelea nayo.

Baada ya taarifa ile shangwe nyingi zilikuepo niseme hata Mimi hapa nilifurahi sanaaaa kupita kiasi.

Sasa watu wakiwa na Furaha Mara Taarifa na picha zikatoka na ni Official zikimuonyesha Mbowe akiwa na Rais wa JMT hapo kila kitu kikaanza kunenwa tofauti hata humu kunawengine wameapia CCM itawale Milele kisa tu Eti Mwamba FAM kaonyesha Uzwazwa sa NAJIULIZA Ule ni Uzwazwa kweli? Au watu hatuelewi SIASA?

Mbowe kila siku Mi nasema na niseme hapa He is A Pure POLITICIAN anaelewa misingi ya Siasa yote sio mpuuzi kwenda Ikulu ni ulize tu Mtu ulikua na Kesi ya Ugaidi inafutwa halaf GAIDI unaitwa Ikulu unakataa sa unakataa vipi, si unaenda ili watu wenye kujiuliza wajiulize na wapate majibu ni Kweli huyu alikua GAIDI yani GAIDI aitwe Ikulu? Hili ndio swali Mlitakiwa kujiuliza jana kesi imefutwa ila inatakiwa tuendelee kufuata mambo madogomadogo ili tuelewe zaidi tusiiishe kwenye kusema Angesusa alichofanya FAM ni ukomavu wa Akili Mkubwa ndani ya SIASA.

Ni malize kwa kuuliza mlitaka Afanye Nini labda Nyie Waungwana?
Alichofanya Mbowe kukutana na Rais ni ukomavu wa kisiasa Ila Kwa wenye akili za kuku ndo wanashangaa. Nchi inapozungumza lugha moja ya kuleta amani hatunabudi kupongeza. Rais na Mbowe wameonesha njia ya kisiasa. Poleni kwa wasaka tonge
 
Alitakiwa akutane na wanachama kwanza. Au leo angetoa taarifa kwa umma nini aliongea na Rais, na nini msimamo wa chama.
Ukimya wake una maana alitolewa kwa masharti akapelekwa kulishwa maneno na mtesi wake.
Lissu arudi aongoze mapambano Mbowe kafika bei.
Hapo ndiyo inaleta taswila kwamba tuhuma hiyo ya ugaidi ina chembechembe ya ukweli.
 
Sidhani kama alipokuwa gerezani akili iliacha kufanya kazi na isitoshe mara zote tulizomuona akiwa mahakamani alikuwa ameshika kitabu kwa maana akili haikuwa dormant. Kwenda moja kwa moja Ikulu kunaonyesha yupo fit!

Simaanishi ufit wa afya ama akili, yeye ni kiongozi wa taasisi, ni vyema angekaa na wenzake kwanza kisha wawe na msimamo wa pamoja. Sina shaka kabisa na afya yake maana nilikuwa namuona, labda kama alienda kama Freeman Mbowe na sio kama mwenyekiti wa cdm.
 
Kajiangalia yeye binafsi acha aendelee kwa mchaga haishangazi Sacco's ataingalia kwa ukaribu Chadema ni Utopolo kama utopolo mwingine
Mbowe kuonana na Rais imewaumiza mnoo CCM haswa waleee. Wapo CCM hawakupenda hata kesi ya Mbowe ya kubambika,lakini vipo vigagula ambavyo havijui lolote!! Mtoa mada umeongea points,hata Mandela kutoka jela ilikuwa ni hatua ya mwisho baada ya vikao vingi kati yake na De Clerk na Ni officials wachache Sana wa ANC walijua.
Na kwa taarifa ni makaburu zaidi waliokasirika Mandela alipotoka jela.
 
Hii kesi ilikuwa ya kutengenezwa ila tu walishindwa kujua kwamba Mungu ni mkuu kuliko kitu chochote.Mashahidi wao wote hakuna hata mmoja aliyetoa ushahidi wa kuweza kuthibitisha kosa lolote la ugaidi.Yule jaji amebaka taaluma yake kwa kufanya kazi kwa maelekezo toka juu.Mahali alipo huenda.anachofurahia ni yale mapesa aliyokuwa analipwa kwa kukubali kuendesha kesi ya mchongo.
 
Ni kukosa uelewa
Mkulu alienda Belgium akakutana na aliyepigwa risasi 16 lakini Mungu alimuokoa huku hamkupiga kelele eboooh
.
Ameonana na Mwenyekiti Mbowe baada ya kukaa gerezani siku zaidi ya 200

Hii ndio Tz Mwl Nyerere aliitengeneza Umoja wetu ndio nguzo
Wanaomlaumu Mwenyekiti ni kuwaacha kwani mioyo yao ni migumu na ya visasi...

Mbowe ni mwenye utu
Safiiiii .wakumbushe pia kuwa .Sera ya Sasa ni no hate no fear
 
Simaanishi ufit wa afya ama akili, yeye ni kiongozi wa taasisi, ni vyema angekaa na wenzake kwanza kisha wawe na msimamo wa pamoja. Sina shaka kabisa na afya yake maana nilikuwa namuona, labda kama alienda kama Freeman Mbowe na sio kama mwenyekiti wa cdm.
Sawa kabisa na hilo ni la muhimu sana, lakini nadhani walikwisha weka msimamo kitambo labda kama kuna haja ya update.
 
Back
Top Bottom