Mnaolalamika na kubeza Mbowe kwenda kuonana na Rais, Mlitaka afanye nini?

Sidhani kama alipokuwa gerezani akili iliacha kufanya kazi na isitoshe mara zote tulizomuona akiwa mahakamani alikuwa ameshika kitabu kwa maana akili haikuwa dormant. Kwenda moja kwa moja Ikulu kunaonyesha yupo fit!
 
Si huyo unaemuita ndie kasema hawez kua mpinzani tena au ni pacha ake?[emoji16]
Kwani alikuwa mpinzani mwaka gani? Huyo Kila siku anajiita CCM Damu halafu aseme ameacha kuwa mpinzani? Hebu Wenye kujua maana ya upinzani waachwe wawe Wapinzani. Siyo Mtu unakaosana na kiongozi Fulani wa CCM halafu unakuja kujiita mpinzani. Wapinzani ndani ya JF wanajulikana, wawe upande wa CDM, CUF au ACT wanajulikana tena Kwa ID zào.
 

Small mind!! Ni mtu gani anaweza kuamriwa kwenda Ikulu na huku akiwa chini ya mhimili huo akakataa?? Mbowe aliandaliwa toka mapema kwa kisingizio cha kuumwa. Hakimu pia alijua ni siku hiyo hiyo alitakiwa kwenda ikulu na ndio maana ya amri “washitakiwa waachiwe huru leo bila kukosa”. Jambo hili zima halikuwa la bahati mbaya - kwenda ikulu sio jambo la ghafla!!! Hakutoka nyumbani kwenda ikulu - uamuzi wake haukuwa huru!!

Lakini kama Mbowe hakutaka kushitakiwa tena kwa kufungua kesi. Akashindwa. Na akatakiwa kujitetea. Yote hayo yalikuwa na lengo la kumwachia huru. Sasa imekuja njia ya mtesi kufuta kesi - ni nini tena ni kikubwa kuliko uhuru??

Watu wa aina yako wangemlaumu hata kama angekwenda nyumbani kwanza. Hata kama angekwenda ofisini kwanza! Watu wa aina yako ni wale wasiojua art of making choices. Wasiojua uwezo wao na mipaka ya uwezo huo!

Ni bahati mbaya umempa uwezo na machaguo mengi Mbowe pia kujali ANGEWEZA au ASINGEWEZA kufanya yapi.
 
Vijana wengi wa CHADEMA wanadhani siasa ni kutanguliza "TUG OF WAR" katika kila jambo.....

#Siempre JMT[emoji120]
Acha unafiki, nioneshe andiko moja tu la Mwanachadema anayejulika humu ambaye amelaumu Mbowe kuitwa Ikulu. Yaani Nyani Ngabu na Gentamycine ni CHADEMA tangu lini?
 
Sasa ngoja ukamatwe wewe hata kwa kutokuwa na ushahidi halafu tuone kama kutakuwa na wakushinikiza uachiwe huru kisa hakuna ushahidi.
Huko Jela Mbowe kawakuta kibao walishikiliwa bila ushahidi ila kawaacha wanaendelea kusota hawana mtu wa kuwaombea kwa rais.
 
Na huu ndio ukweli ni watu wasioelewa tu wanashindwa kufumbua haka kamtego hii plan ilikuepo tu.
 
Tanzania ina vyama zaidi 10 vya upinzani, kwanini CDM mnateseka nayo kuliko vyama vingine?! Kama unaona Mbowe is not your choice opt kwingine. Hata ACT -wazalendo.
Anza wewe.
 
Lkn at the end watatoka tu jela sio mwisho wa maisha.
Afrika jela unakaa kwa sababu mbili.
1.Wewe ni masikini huna pesa ya kuhonga kununua UHURU wako.
2.Unaweza ukawa na pesa lakini umekosana na wanasiasa au wenye mamlaka nature ya mswahili ni visasi so unawekwa jela kukomolewa.
Nadra Sana kumkuta tajiri jela afrika nje ya point hizo mbili
 
Alichofanya Mbowe kukutana na Rais ni ukomavu wa kisiasa Ila Kwa wenye akili za kuku ndo wanashangaa. Nchi inapozungumza lugha moja ya kuleta amani hatunabudi kupongeza. Rais na Mbowe wameonesha njia ya kisiasa. Poleni kwa wasaka tonge
 
Mwenyekiti kaunga juhudi za ccm.
 
Hapo ndiyo inaleta taswila kwamba tuhuma hiyo ya ugaidi ina chembechembe ya ukweli.
 
Sidhani kama alipokuwa gerezani akili iliacha kufanya kazi na isitoshe mara zote tulizomuona akiwa mahakamani alikuwa ameshika kitabu kwa maana akili haikuwa dormant. Kwenda moja kwa moja Ikulu kunaonyesha yupo fit!

Simaanishi ufit wa afya ama akili, yeye ni kiongozi wa taasisi, ni vyema angekaa na wenzake kwanza kisha wawe na msimamo wa pamoja. Sina shaka kabisa na afya yake maana nilikuwa namuona, labda kama alienda kama Freeman Mbowe na sio kama mwenyekiti wa cdm.
 
Kajiangalia yeye binafsi acha aendelee kwa mchaga haishangazi Sacco's ataingalia kwa ukaribu Chadema ni Utopolo kama utopolo mwingine
Mbowe kuonana na Rais imewaumiza mnoo CCM haswa waleee. Wapo CCM hawakupenda hata kesi ya Mbowe ya kubambika,lakini vipo vigagula ambavyo havijui lolote!! Mtoa mada umeongea points,hata Mandela kutoka jela ilikuwa ni hatua ya mwisho baada ya vikao vingi kati yake na De Clerk na Ni officials wachache Sana wa ANC walijua.
Na kwa taarifa ni makaburu zaidi waliokasirika Mandela alipotoka jela.
 
Hii kesi ilikuwa ya kutengenezwa ila tu walishindwa kujua kwamba Mungu ni mkuu kuliko kitu chochote.Mashahidi wao wote hakuna hata mmoja aliyetoa ushahidi wa kuweza kuthibitisha kosa lolote la ugaidi.Yule jaji amebaka taaluma yake kwa kufanya kazi kwa maelekezo toka juu.Mahali alipo huenda.anachofurahia ni yale mapesa aliyokuwa analipwa kwa kukubali kuendesha kesi ya mchongo.
 
Safiiiii .wakumbushe pia kuwa .Sera ya Sasa ni no hate no fear
 
Sawa kabisa na hilo ni la muhimu sana, lakini nadhani walikwisha weka msimamo kitambo labda kama kuna haja ya update.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…