Mnaomiliki na kutumia Volkswagen 'chuma ya mjerumani' ni gereji zipi mnafanyia service & repair? Popote pale nchini

Mnaomiliki na kutumia Volkswagen 'chuma ya mjerumani' ni gereji zipi mnafanyia service & repair? Popote pale nchini

Kuna duka linaitwa morogoro spare lipo makutano ya barabara ya morogoro na jamhur Dsm, hapo utapata spare zote za magari ya German.

Upo sawa 100% , hilo duka niliwahi fika pale nikitafuta parts za Landrover na ndipo nilipokutana na mmoja wa wateja ambaye kifaa alichokuwa anakitafta hakikuwepo then akaambiwa asubirie kidogo, Mhindi yule akazama kwenye email na baada ya muda kidogo yule bwana alipewa gharama zote na akaambiwa within 7 days atapokea spare part husika NB: gharama ilikuwa imechangamka kidogo kulingana na aina ya gari kwa wakati ule
 
Mkuu Nukta5 , VW yako bado ipo kwa hewa? Share nasi uzoefu wako ni wapi unapata spea na kufanya services.
 
Kuna duka linaitwa morogoro spare lipo makutano ya barabara ya morogoro na jamhur Dsm, hapo utapata spare zote za magari ya German.

Thanks mkuu for sharing such location. Wahitaji itawasaidia.
 
Kuna Jerry Spare Parts and Service.

Yupo hapo Victoria karibu na Kairuki....

Safi sana mkuu. Umeutendea haki Uzi huu.

Ahsante kwa kushea hiyo repair location. Wahitaji watasoma na itawasaidia.
 
Kuna jamaa mwingine anaitwa Temu, yupo maeneo ya hapo Victoria pia.

Ila yeye ni fundi umeme tu.

Good. Fundi wa umeme tu kwa Europe cars..

Anapatikanaje hapo Victoria, jina lake maarufu? ama jina la gereji yake?
 
Nimejaribu kupitia coment zote lakini sioni gereji wala duka linalouzwa spare parts za magari tajwa na kibaya zaidi binafsi nikienda gereji zetu mtaani nazikuta VW Polo (Nazipenda sana) zikiwa zimepaki kwa kukosa vipuri mmojawapo ilikuwa imepasua sample tu?

anyway je hatuna agent wa magari hayo ya ulaya pamoja na kwamba wakiwepo wanakuwa na bei ghali sana kuliko maduka ya watu binafsi mfano pale Kariakoo Toyota wana duka lao na wanauza vitu Genuine tu na nikatafuta Genuine hiyo hiyo kwa part number hiyo hiyo Kisutu nilikuja kushangaa jamaa wa Kisutu alikuwa anauza bei ya chini kuliko agent alivyokuwa anauza

Wadau wanataja mkuu, pitia comments vizuri.
 
Ndugu nishauri jambo nkitaka kubadili engine ya VW T3 niweke engine ya Foresta unaweza nishauri vipi hapa na je engine gani naweza weka kwenye hii gari?
unaweza sana ukaweka hiyo ya ej20 au ej22 lakin hyo t3 yako iwe ni ile ya watercool na sio ya air. pil unaweza ukaweka engine ya toyota noah 3s. ukafanya modification kidogo ambapo ikashakaa sawa hutokaa usumbuke kama mm nilivyofanya.
 
Anaitwa fundi temu tu.

Namba yake ukitaka ntakupatia.

So kwa umeme wa magari ya Ulaya, kuna fundi aitwaye Temu, anapatikana pale maeneo ya Victoria. Fundi umeme tu wa magari.

Mkuu, thanks for sharing such info.
 
Upande wa Mwanza vipi???? na Kahama???

Pande hizo hakuna wanaomiliki gari za mjerumani?
 
Kwa kuzingatia viwango vya safety, stability, comfortability, inaonekana wazi kabisa kuwa watu wengi wanatamani sana kumiliki magari ya Ulaya. Lakini wanaogopa kuyamiliki kwasababu kuu tatu:

- Uhaba wa mafundi/garage for European cars...
Moshi maeneo ya Mbuyuni ndio mafundi bora kabisa hapa Tanzania
 
Moshi maeneo ya Mbuyuni ndio mafundi bora kabisa hapa Tanzania

Kwanza heshima yako Madam Jaji mfawidhi.

Back to topic... pale Moshi mbuyuni, kuna mafundi wa magari ya Mjerumani?

Ma'am hatuzungumzii Toyota. Tunazungumzia vyuma vya Ulaya, specifically Volkswagen ya mjerumani.
 
unaweza sana ukaweka hiyo ya ej20 au ej22 lakin hyo t3 yako iwe ni ile ya watercool na sio ya air. pil unaweza ukaweka engine ya toyota noah 3s. ukafanya modification kidogo ambapo ikashakaa sawa hutokaa usumbuke kama mm nilivyofanya.

Shukrani mkuu dah sikuiwaza noah kabisa
 
Back
Top Bottom