Mnaomshinikiza Rais Samia amuachie huru Sabaya acheni, Mwacheni Sabaya avune alichopanda!

Mnaomshinikiza Rais Samia amuachie huru Sabaya acheni, Mwacheni Sabaya avune alichopanda!

Kwahiyo wewe unafaidika nini kuna malipo unapata kutokana na mateso ya Sabaya yaani masikini mmejaa roho za chuki ndio maana umasikini hauishi wazungu wanatuponda kwa mawazo ya watu kama nyie kwamba waafrika wanachukiana wao kwa wao pasipo sababu ya msingi yoyote.
 
Kwangu mimi hao wakina mama wangefanya yafuatayo hapa chini ndio ningeona vilio vyao ni vya maana:-

1. Wangewatafuta wale wote wanaolalamika kutendewa uovu/dhuluma na Sabaya kwa njia moja au nyingine.

2. Wale wenye madai ambayo yapo ndani ya uwezo wa hao wakina mama wawaomba msamaha na wawalipe mara moja.

3. Wale ambao hawana uwezo wa kuwalipa wawaombe msamaha tu kwa dhati ya mioyo yao kwa niaba ya Sabaya.

Naamini wengi watakaoombwa msamaha hawatakuwa na mioyo migumu watasamehe tu hasa ikizingatiwa
kuwa watakaokuwa wanaomuombea msamaha Sabaya ni wakinamama tena watu wazima.

4. Baada ya hilo zoezi waende mahabusu wamweleze Sabaya hatua walizochukua na wamtake Sabaya na yeye akiri yale yote aliyoyatenda hata kama ni maovu kiasi gani na aombe msamaha kwa wahanga wote aliowaumiza kwa njia moja au nyingine kupitia barua ya wazi kwenye vyombo vya habari.

5. Baada ya hatua zote hizo waiachie mahakama ifanye kazi yake bila shinikizo. Maana mahakama ikiruhusiwa
kufanya maamuzi kwa shinikizo basi kila familia yenye mtu wao anayeshatakiwa watataka waende na wao
kulia mahakamani ili ndugu yao aachiwe.

6. Pia waache kumuingiza kiongozi wa nchi kwenye mtego kwani suala kama hilo lilishaleta sintofahamu kubwa
nchini pale raisi wa awamu ya pili alipoamuchia mtuhumiwa kepteni Aziz (kama nimekosea jina wahenga
watanisaidia)

Mwisho hao wakinamama wanapaswa wajue kuwa watu wengi walipitia maumivu makubwa sana ya kiakili,
kimwili, kisaikolojia na kiroho yaliyosababishwa na huyo Sabaya. Kwa hiyo maumivu anayoyapata sasa hivi Sabaya hayafiki hata robo tu ya aliyowapitisha wenzake kwani yeye mateso makubwa ni kukosa tu uhuru na wala sio maumivu ya kimwili. Lakini muhimu na kubwa ni msamaha tu kutoka kwa wahanga na wala sio kuachiwa huru. Kwani hata akiachiwa leo bado hatakuwa huru ikiwa wahanga bado hawajamsamehe. Lakini kukiwa na msamaha hata siku akiachiwa huru na mahakama basi atakuwa huru kuendelea na maisha yake kama kawaida bila matatizo yoyote.

Na kubwa la kujifunza ndugu zangu pale tunapoona watoto wetu au hata ndugu zetu wanawafanyia dhuluma watu wengine tuwakemee kwa nguvu zote hata kama wao ndio wanatuaptia mkate wa kila siku. Tusisubiri wakaharibikiwa ndio tutoke hadharani tena bila hata aibu badala ya kuomba msamaha kwa matendo yao maovu tunaomba mamlaka au viongozi wakubwa waingilie kati ili wawe huru.

Ni mtizamo tu.
 
Zimekuwepo kampeni za wazi mitandaoni za kumblackmail mhehimiwa rais kumtaka amuachie huru Sabaya. Wanaofanya haya wanatumia mbinu ya mashambulizi ya kisaikolojia ili kumfanya mheshimiwa rais ajisikie hatia kwa uwepo wa sababya ndani na hivyo kuchukua uamuzi wa kutumia ushawishi wake kumfutia mashitaka.

Baadhi ya hoja au mbinu wanazotumia wanaotaka Samia aingilie kesi za Sabaya ni hizi zifuatazo

1. Eti kwa kuwa Sabaya alikuwa kijana wa Magufuli basi kumuweka ndani ni kupambana na Magufuli
Hii ni hoja ya kisiasa yenye lengo la kumblackmail mheshimiwa rais Samia aogope mwenendo wa kesi kwa hofu kwamba kundi la waanchi na wanaCCM wanaomkubali Magufuli watachukizwa na hatua hii ya Sabaya kufikishwa katika vyombo vya sheria. Naamini hii hoja haina mashiko kwa sababu zifuatazo
a) Kufanya kazi katika serikali ya Magufuli au kupendwa na Magufuli si kinga ya udhalimu wako au uvunjaji wako wa sheria. Na kwa kuwa jinai haifi basi yeyote yule ambayo Jamhuri itajiridhisha kuwa ana kesi ya kujibu mahakamani atafikihwa mahakamani. Sabaya na watu wake wasijifiche katika ngao ya hayati
b) Hoja ni hii ni dhaifu kwa sababu ni matusi kwa hayati Magufuli, Kumtumia Magufuli kufunika udhalimu na jinai ni sawasawa na kusema kuwa hayati ndiye aliyemtuma Sabaya aonee watu, apore watu, anyanyase wanawake kijinsia na matendo mengine ya kinyama kabisa. Kwa hiyo mimi ninafikiri kwamba ili kulinda heshima ya hayati ni vyema watu wote waliofanya udhalimu chini ya kivuli chake wakashughulikiwa wao kama wao badala ya kuingiza jina la hayati

2. Hoja eti Sabaya ana mazuri yake kaitendea serikali na hivyo serikali isamehe tu mabaya yake
Hii ni hoja dhaifu zaidi, na imejaa ubinafsi mkubwa.

a)Sabaya kuwa mtumishi wa serikali, kutenda mazuri ni wajibu wake, maana hilo ndilo alilotumwa afanye na alikuwa akilipwa mshahara kwa hilo. Hata hivyo Sababya hakutumwa awe jambazi, mporaji, mnyanyasa wanawake kingono na matendo mengine ya kidhalimu. Jamhuri haimshitaki Sabaya kwa mazuri yake aliyoyafanya, bali inamshitaki kwa mabaya yake, na ni vyema haki itendeke
b) Sabaya si tu kwamba ameikosea Jamhuri lakini amewakosea watu ambao ni wahanga wa matendo yake ya kidhalimu, Kama mnataka Sabaya asamehewe, vipi kuhusu watu aliowafanyia kila aina ya uovu, mbona hawa hamuwaonei huruma?, Haki yao itapatkanaje?
d)Sabaya si kiongozi wa kwanza kukamtwa na kuwekwa ndani, Amewahi kukamatwa waziri wa Nyerere mzee Fundikira akatiwa bakora kwa rushwa, na akawekwa ndani. Amewa hikukamatwa waziri kiongozi wa zamani wa Zanzibar Seif Sharif Hamad, na waziri wa zamani wa serikali Juma Duni Haji na walikaa ndani takriban miaka minne, amewahi kukaa Jela mzee Mramba na Yona , SEMBUSE SABAYA?, Sheria ichukue mkondo wake!
c) Ni ubinafsi kumuomba msamaha rais Samia, ila usiombe msamaha kwa wale ambao Sabaya kawatendea unyama. Hii inaonyesha kuwa Sabaya bado hajajuta, na watu wake hawajali hata kidogo hisia za wahanga wa matendo ya Sabaya

3. Drama ya vilio vya akina mama na kauli yao eti Sabaya asamehewe keshajifunza
a) Tangu Sabaya akamatwe, haijafika hata miaka miwili. Huyu ni mtu ambaye mahakama moja nchini iliona anahitaji kukaa Jela kwa miaka 30 ili ajifunze kuachana na udhalimu wake, Japo mahakama ya juu ilitengua hukumu hii kwa "technicalities" lakini ukweli ni kwamba Makosa aliyotenda Sabaya si ya kukaa jela mwaka mmoja na akajifunza akarekebishika, ndiyo maana mahakama ya awali iliona miaka inayomtosha ni 30

b) Wakati Sabaya na watu wake wanaolia ili aachiwe huru wakiendelea na kampeni yao ya kibinafsi ya kumtoa Sabaya ndani, Kuna watu nchii hii wamekaa Jela miaka Lukuki na wakapambana mahakamani, Hatukuona familia zao zikikusanya watu ili walie mbele ya Camera. Kuna Mzee Lugemalira, alikaa ndani zaidi ya miaka Mitatu, Kuna Yusufu Manji alikaa ndani miezi mingi tu, Kuna Masheikh wa uamsho walikaa ndani kwa miaka nane huku kesi yao ikipigwa Kalenda SEMBUSE SABAYA ALIYEKAA GEREZANI KAMWAKA KAMOJA TU NDO WATU WANAMWAGA MCHOZI KUOMBA FAVOR?- Mimi nasema tuhuma Za Sabaya ni kubwa sana Sheria ichukua mkondo wake!

4. Ushauri kwa Rais Samia na Serikali
Tuhuma za Sabaya ni nzito sana, Kapora, Kajeruhi watu, Kabaka wanawake. Huyu mtamuachiaje hivihivi bila kuwa accountable kwa udhalimu wake?, Kama mkiamua kumuachia, mtakuwa mmefanya dhulma kubwa kwa wale aliowafanyia unyama. Msimuangalie Sabaya kama Victim, muangalieni Sabaya kama Perpetrator.
Msiingie katika mkumbo wa kumwachia Sabaya kwa visingizio eti ni mwanaCCM mwenzetu. Katiba ya CCM hakuna sehemu inayosema wananchama wake wavamie biashara za watu wapore fedha, au wabake wanawake, au wajeruhi watu, sasa mtajenga precedent mbaya ya entitlement kwamba ukiwa mwanaCCM na kiongozi kisha ukafanya udhalimu wa kutisha basi chama na serikali vitakulinda.

Ushauri wangu kwa mama Samia ni kuwa, Usione huruma kwa hivi vilio vya akina mama waliojipanga kufanya drama mbele ya Camera. Wanatumia mbinu ya kukushambulia kisaikolojia, kwa kutumia huruma ya mama ili kumwachia huru huyu kijana dhalimu. Ninachosahuri ni kuwa wacha HAKI ITENDEKE, USIMUONEE WALA USIMDHULUMU wacha sheria ichukue mkondo wake.

Mheshimiwa Rais, Siyo Sabaya peke yake mwenye mama mzazi anayemuonea huruma, au mwenye ndugu wenye kujali , au mwenye mchumba anayetegemea kumuoa. Kuna watu kibao wapo jela kwa kesi ya kuiba kuku, au vimakosa vidogovidogo na wanatumikia vifungo vyao, nao hao wanandugu zao, wana wazazi wao. JE NAO WAFANYE DRAMA KWENYE CAMERA YA KULIA ILI KUKUSHAWISHI UWAACHIE?
Mbona Mbowe kasamehewa na hajana aloyapanda?
 
Mashtaka anayoshtakiwa sasa hivi ndugu Sabaya yanamhusu mwenyewe. Magufuli hausiki hata kidogo. Wamwache mzee wa watu apumzike. Hata Sabaya mwenyewe sasa hivi asimsingizie Magufuli wala serikali ya Magufuli
 
Back
Top Bottom