Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,211
- 3,611
- Thread starter
- #161
Mkuu, shida ni tafsiri ya Katiba, labda tunahitaji marekebisho madogo ya Katiba kwenye Ibara hizi ili kujipanga na uzoefu tulioupata wa kuondokewa na kiongozi akiwa madarakani.Kama angekuwa ametumikia miaka pungufu ya mitatu, then sawa ila kwa bahati mbaya magufuri amefariki na kumuachia zaidi ya miaka minne so kikatiba haruhusiwi kugombea zaidi ya mara mbili. Yaani hapa akiingia uchaguzi wa 2025 ndio mwisho wake kugombea hata kama CCM watapendekeza aendelee katiba inakataa kabisa.
Sura ya Pili, Sehemu ya Kwanza, Ibara za 38, 39 na 40.
Ibara ya 40 (1) na (2)
Kifungu (1)
"Bila kuathiri masharti ya mengineyo yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote ambaye ni Rais anaweza kuchaguliwa tena kushika kiti hicho" Siyo kuteuliwa na Katiba.
Kifungu (2)
"Hakuna mtu atakayechaguliwa zaidi ya mara mbili kushika kiti cha Rais"
Mhe. Rais Samia hajachaguliwa, atachaguliwa kwa mara ya kwanza 2025 na hivyo kwa mara ya pili kama atagombea na kushinda 2030 na hivyo kuhitimisha awamu zake 2035.
Bado tunaye sana tu!