Mnaonaje Rais Samia akiongezwa muda wa kukaa kwenye dhamana na mamlaka yake hadi 2035?

Mnaonaje Rais Samia akiongezwa muda wa kukaa kwenye dhamana na mamlaka yake hadi 2035?

Mmeanza,mnataka na huyu afe kabla ya kumaliza mihula yake 2?Uchuro huu sasa.
 
Kama unasema nipigie mstari jibu kwamba uelewa wako ni mkubwa kuwa Ikulu iko juu ya katiba kwamba haiwezi kukaguliwa na CAG basi kumbe Rais ambaye ndiye Mkuu wa taasisi ya Ikulu aongoze milele kwa kutumia uelewa wako kwamba yuko juu ya katiba.

Tunapotaka katiba mpya hatuitaki kwa bahati mbaya. Tunajua fika madaraka ya rais yanamfanya kuwa juu ya sheria na katiba, matokeo yake ile sheria yenye nguvu kuliko katiba iitwayo amri kutoka juu ndio inapoanzia. Udhaifu wote wa Mihimili na taasisi mbalimbali za kimamlaka unatokana na mamlaka ya urais yanayotumika vibaya. Na yote hayo ni kutokana na kifungu kinachozuia rais kushitakiwa kawa makosa atakayofanya akiwa madarakani, au akiwa ametoka. Hapa ndio uchafu wote wa kiutawala ndani ya nchi hii unapooanzia, kwani hufanya tabia binafsi za raisi aliye madarakani na genge lake kufanya watakavyo na mifano halisi ipo.
 
Nachokoza mada.

Wadau mnaonaje kama Rais Samia akiongezwa muda wa kukaa kwenye dhamana na mamlaka yake hadi 2035? Kwa kuwa Rais Samia alichukuwa nafasi yake kufuatia mauti ya mtangulizi wake mwanzo wa safari na kwamba hakukuwa na utaratibu wa mila na desturi ya uchaguzi bali ilikuwa ni kutimiza matakwa ya katiba.

Kiuhalali na kwa haki kwake, anastahili kuwa wa pili nyuma ya Mwl Nyerere kwa kukaa ofisini kwa miaka 15 kwa maana ya miaka aliyopokea kijiti kwa sharti la katiba na ndipo sasa astahili utaratibu wa mila na desturi yetu ya uchaguzi ambapo anaruhusiwa awamu mbili 2025 – 2035?

Nini maarifa yako, tupe maoni kwa vigezo na ushahidi.

789CD657-ABB8-4E3F-8D64-431FAA661E79.jpeg
 
Historia huwa ina archive evidence, ziweke hapa tufaidike nazo.
Si uende KIUTA kwenye archive Za magazeti utaona au waulize wazee wako wa CCM watakuambia. Pia hio ni historia bado iko vichwani mwa watu , kaulize mtu yeyote mwenye umri wa at least 64 yrs atakuambia kwa huku kwetu Zanzibar
 
KIUTA haifanyi archiving, inachapa nyaraka za serikali tu. Archiving inafanywa na idara ya kuhifadhi nyaraka za serikali. Kwa magazeti yanachapwa na viwanda binafsi vya uchapaji na archiving zake zinafanywa na Shirika la Maktaba ya Taifa. KIUTA pekee ndiyo inachapa gazeti la serikali (government gazette).
 
Nachokoza mada.

Wadau mnaonaje kama Rais Samia akiongezwa muda wa kukaa kwenye dhamana na mamlaka yake hadi 2035? Kwa kuwa Rais Samia alichukuwa nafasi yake kufuatia mauti ya mtangulizi wake mwanzo wa safari na kwamba hakukuwa na utaratibu wa mila na desturi ya uchaguzi bali ilikuwa ni kutimiza matakwa ya katiba.

Kiuhalali na kwa haki kwake, anastahili kuwa wa pili nyuma ya Mwl Nyerere kwa kukaa ofisini kwa miaka 15 kwa maana ya miaka aliyopokea kijiti kwa sharti la katiba na ndipo sasa astahili utaratibu wa mila na desturi yetu ya uchaguzi ambapo anaruhusiwa awamu mbili 2025 – 2035?

Nini maarifa yako, tupe maoni kwa vigezo na ushahidi.
Huu ni ufinyi na ukosefu wa oksijeni kwenye ubongo
 
Tulishakataa haya mambo ya kipumbavu

Hana kipingamizi aombe kwa kwenye sanduku la kura sio kwa njia zenu zenye hila

Nyinyi ndio mnaogeuza watu miungu watu hadi wanakengeuka tuache hii tabia

Mama yenu Hana kipingamizi anaruhusiwa kikatiba kugombea one term
 
Ukweli mnakera na kutuchosha na hivyo vikampeni vyenu wakat wake bado kila mala eti rais Samia aongoze miaka miaka miaka n.k

Kwann hamjiamin? Nan anamkataa au Nan anamchukia na kwssb gan? Muda ukifika zitaanza tu!! Mnawashwaaaa!!!

Kwanza jueni hv vikampen vyenu mna mtia mkos tu mama yetu, si mlisema Magufuri atawale milele nyie! na badala yake akaenda kutawala malaika japo sijui ni malaika wa Mungu au wa shetani!!!

Hii nchi kwa wakati huu inavitu vya msingi vya kujadili Pengine ata kumshauri kupitia JF. Mfano; Kukuza uchumi utakaopelekea wafanyakaz kuongezwa mishahara. Wewe unafikiri kwss hv ata wakimshangilia wanatoa moyoni 100%?

Kila kukicha shilingi inashuka, tunatumia shs nyingi kununua dola, hili tuagize bidhaa nje

mafuta ya kula mpaka leo hayashkk, petrol na dezel balaa tupu, tozo ndo usiseme, corona na chanjo pasua kichwaaa. Katiba mpya changamoto kwake. Kwa upande wa Democrasia mataifa mengi yanatusema vibaya n.k

Mnademkaaaaa na miaka, tumieni muda mwingi kumshauri rais mambo yakae sawa tu, mengine ni automatic
 
Mnaanza kumtilia uchuro na hiyo mitatu asimalize… Shauri zenu,

nasikia Arusha huko kaanza kutoa speech za mniombee…Muombeeni amalize hii mitatu kwanza, hamjifunzi ?
 
Kwamba alieapa ni mabeyo?
Ndio, Mabeyo anajua kinachoendelea kuliko Samia.

Kwenye mazishi ya Magu Mabeyo alimwambia Samia ukitulia njoo nikupe siri za nchi.

Yani Vice President Samia alikuwa kikaragosi tu haambiwi siri za nchi!

Mhimili wa Mabeyo unapingana na mhimili wa Kikwete.
 
Back
Top Bottom