Sura ya Pili, Sehemu ya Kwanza, Ibara za 38, 39 na 40.
Ibara ya 40 (1) na (2)
Kifungu (1)
"Bila kuathiri masharti ya mengineyo yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote ambaye ni Rais anaweza kuchaguliwa tena kushika kiti hicho" Siyo kuteuliwa na Katiba.
Kifungu (2)
"Hakuna mtu atakayechaguliwa zaidi ya mara mbili kushika kiti cha Rais"
Mhe. Rais Samia hajachaguliwa, atachaguliwa kwa mara ya kwanza 2025 na hivyo kwa mara ya pili kama atagombea na kushinda 2030 na hivyo kuhitimisha awamu zake 2035.
Bado tunaye sana tu!