kuna taasisi isiyokaguliwa na CAG. Ebu ona hii kama labda ulikuwa hujazaliwa:-
Mnamo tarehe 26/04/2003 kampuni ya Net Group Solutions (NGS) ya Afrika Kusini ilipata baraka za serikali kupewa kandarasi ya kuendesha menejimenti ya Tanesco. Kwa taarifa za ukaguzi wa Tanesco hata Ikulu na jeshi zilikuwa wadaiwa wakubwa wa ankara za umeme, Rais Mkapa (Big Ben) alitoa kibali kwa Net Group Solutions kukusanya madeni yote na Ikulu pamoja na jeshi zikalipa madeni yao baada ya NGS kutishia kukata huduma na kuwapeleka wadaiwa sugu Mahakamani. CAG ana mamlaka ya kukagua taasisi zote. Je, taasisi ya Ikulu si ni ile ile inayotambuliwa na Katiba? Nikusahihishe kwamba CAG ana weledi (professionalism) wa kitaaluma na kitendaji, ni taasisi ya wataalam waliobobea, hakuna mwanaharakati pale CAG anayekagua mahesabu ya taasisi.