Nachokoza mada.
Wadau mnaonaje kama Samia akiongezwa muda wa kukaa kwenye dhamana na mamlaka yake hadi 2035? Kwa kuwa Samia alichukuwa nafasi yake kufuatia mauti ya mtangulizi wake mwanzo wa safari na kwamba hakukuwa na utaratibu wa mila na desturi ya uchaguzi bali ilikuwa ni kutimiza matakwa ya katiba;
Kiuhalali na kwa haki kwake, anastahili kuwa wa pili nyuma ya Mwl Nyerere kwa kukaa ofisini kwa miaka 15 kwa maana ya miaka aliyopokea kijiti kwa sharti la katiba na ndipo sasa astahili utaratibu wa mila na desturi yetu ya uchaguzi ambapo anaruhusiwa awamu mbili 2025 – 2035?
Nini maarifa yako, tupe maoni kwa vigezo na ushahidi.
Kwanini asipige kazi ya ukweli kwa miaka hii minne, matokeo yake yatawashawishi wananchi kuhusu hiyo issue.
Huu unatakiwa uwe wakati wa kuchapa kazi, kampeni baadaye.
Matokeo chanya ya kazi zake yatampigia kampeni nzuri tu kama ajira kuongezeka, biashara, uwezekaji kushamiri, masoko kwa wakulima, bei rafiki za pembejeo, mbolea, vifaa vya umwagiliaji,mazingira rafiki ya biashara, kupunguza rushwa, urasimu, kuunganisha nchi iwe yenye umoja zaidi, kupunguza matumizi yasiyo na tija kwa serikali, kuondoa au kupunguza kodi/ tozo zinazoumiza wengi. Maji, umeme kwa kila familia, kukuza utalii.
Nguvu zake zote, focus yake yote zingeelekezwa kutatua hizi changamoto.
Muda ni mchache, inabidi utumike vizuri kwa kazi aliyopewa na Watanzania,kutatua changamoto zao, sio kupiga kampeni kutoka siku za mwanzo za utawala wake.