Mnaonaje Rais Samia akiongezwa muda wa kukaa kwenye dhamana na mamlaka yake hadi 2035?

Mkuu, shida ni tafsiri ya Katiba, labda tunahitaji marekebisho madogo ya Katiba kwenye Ibara hizi ili kujipanga na uzoefu tulioupata wa kuondokewa na kiongozi akiwa madarakani.

Sura ya Pili, Sehemu ya Kwanza, Ibara za 38, 39 na 40.

Ibara ya 40 (1) na (2)

Kifungu (1)
"Bila kuathiri masharti ya mengineyo yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote ambaye ni Rais anaweza kuchaguliwa tena kushika kiti hicho" Siyo kuteuliwa na Katiba.

Kifungu (2)
"Hakuna mtu atakayechaguliwa zaidi ya mara mbili kushika kiti cha Rais"

Mhe. Rais Samia hajachaguliwa, atachaguliwa kwa mara ya kwanza 2025 na hivyo kwa mara ya pili kama atagombea na kushinda 2030 na hivyo kuhitimisha awamu zake 2035.

Bado tunaye sana tu!
 
Dawa yenu ni katiba mpya - maana CCM sasa hivi mnapangiana miaka awamu kwa awamu as if Tanzania mnaimiliki nyie.. usishangae mwingine akasema mama akitoka January anakamata 2035 - 2045.
Kama ana vigezo na sifa anakamata tu, ni haki yake kama ilivyo kwa mwingine, mbona dynasty inafanyakazi duniani?
 
Kama amepata hicho cheo kwa mujibu wa katiba..... Sasa kwa nini katiba hiyo hiyo ipinfishwe.
 
Hata yule mlimuombea hivi hivi
Shida MUNGU nae anapanga yake.
Dakika yako 1 ya mbele haujui itakuwaje vipi hyo miaka.?.
 
Kama amepata hicho cheo kwa mujibu wa katiba..... Sasa kwa nini katiba hiyo hiyo ipinfishwe.
Sura ya Pili, Sehemu ya Kwanza, Ibara za 38, 39 na 40.

Ibara ya 40 (1) na (2)

Kifungu (1)
"Bila kuathiri masharti ya mengineyo yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote ambaye ni Rais anaweza kuchaguliwa tena kushika kiti hicho" Siyo kuteuliwa na Katiba.

Kifungu (2)
"Hakuna mtu atakayechaguliwa zaidi ya mara mbili kushika kiti cha Rais"

Mhe. Rais Samia hajachaguliwa, atachaguliwa kwa mara ya kwanza 2025 na hivyo kwa mara ya pili kama atagombea na kushinda 2030 na hivyo kuhitimisha awamu zake 2035.

Bado tunaye sana tu!
 
Sio kipande hicho.

Soma hapa......
 
Wewe bado haujaelewa. Katiba inasema ikatokea raisi aliyepo, akapatwa na umauti, then makamo wake akikaimu nafasi hiyo kulingana na maelekezo ya katiba katika kipindi kinachopungua miaka mitatu hadi mwisho wa awamu husika then huyu mkaimu ataweza kuingia katika chaguzi kugombea mara mbili zaidi, na ikatokea akamekaimu miaka zaidi ya mitatu kama samia kwa sasa then ataruhusiwa kikatiba kugombea mara moja tu na si zaidi.

Wapi haujaelewa bwana mdogo?!
 
Alichaguliwa 2020 kwa mujibu wa katiba. Unapokuwa unamchagua Rais kwenye uchaguzi mkuu kwa mujibu wa katiba unakuwa unawachagua kwa pamoja wafuatao (siyo unawateua):
1. Unakuwa unamchagua Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
2. Umakuwa unamchagua makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
3. Unakuwa unamchagua Rais wa Jamhuri ya Tanzania atakayeshika nafasi endapo ndani ya miaka mitano Rais aliyepo madarakani atakosa uwezo wa kuwa Rais kwa sababu yohote ile au akifariki.
Kwa hiyo kwa mujibu wa katiba SSH tulishamchagua kwa kura hapo october 2020.
Achilia mbali ukweli huo, katiba inaainisha wazi kuwa endapo makamu atachukua nafasi ya urais kwa zaidi ya miaka 3, basi atsweza kugombea kwa mara moja nyingine na si zaid.i
 
Naunga mkono hoja tena mimi nataka apewe hata miaka 40.
 
Tanganyika ipo imelivaa kitu la muungano.

Kuhusu invasion of Zanzibar
Msikilize Lukuvi anaongea nini kanisani


Hamza alitakiwa amwanzie huyu kwanza anaechukia waislamu na wazanzibari kwa ujumla, i wish mheshimiwa rais aione hii clip. Na kama ameiona atakuwa anakosea sana kumwacha aendelee kuwa waziri. Ni mdini na mbaguzi sana
 

 
Kuna mtu walimpamba hivyo hata miaka 6 hakufika, acha kumchulia mama wa kipemba [emoji849]
 
Sio kipande hicho.

Soma hapa...... View attachment 1978195
Mkuu unajuwa tatizo liko kwenye tafsiri, hasa ya neno "uchaguzi" kifungu hiki cha 4 cha ibara ya 40 ebu kisome sambamba na kifungu cha 1 ibara ya 41, kuhusu:-
1. Uwasilishaji wa majina ya wagombea,
2. Inachopaswa kufanya Tume ya Uchaguzi,
Hapa ndipo hata wapinzani wanapata shida. Sasa basi Mhe. SSH alitambuliwa lini na Tume ipi ya Uchaguzi? Jina lake litawasilishwa kwa mara ya kwanza kwa NEC 2025 (rekodi za NEC hazitasoma kwamba SSH aliwahikugombea 2021). Tunaweza tukakwama mbeleni mkuu...
 
Aendelee mpaka 2040
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…