Mnaonaje tubadili katiba yetu ili Rais Samia aendelee kuongoza Taifa letu baada ya kumaliza muhula wake 2030?

Mnaonaje tubadili katiba yetu ili Rais Samia aendelee kuongoza Taifa letu baada ya kumaliza muhula wake 2030?

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Katiba siyo msaafu wala siyo Biblia. Katiba yetu ilitungwa na wanadamu ambao ni watanzania kwa lengo la kuwa kama muongozo wa masuala mbalimbali ya kuongoza Nchi yetu. Katiba Ni karatasi tu zilizojaa maneno ya namna gani ya jambo fulani lifanyike na hatua zipi zifanyike na kufuatwa katika kufikia hitimisho la jambo fulani.

Katiba yetu ipo kwa ajili yetu watanzania na ni kwa ajili ya ustawi wetu pamoja na Taifa letu kwa ujumla wake. Ni muongozo wa mambo yetu wenyewe.

Nilikuwa napenda kuwaambieni watanzania Wenzangu ya kuwa tufike wakati tutambue ya kuwa viongozi aina ya Rais Samia hawazaliwi kila siku na wala hawapatikani kila Nchi na wala siyo Rahisi kuwatengeneza .

Huyu Rais ni Mchapa kazi kwelikweli,ni mzalendo aliyetukuka na ambaye huwezi kumtilia shaka juu ya uzalendo wake,ni kiongozi mwenye maono,akili kubwa,upeo mkubwa na Karama ya uongozi. Ni kiongozi ambaye amejitoa na kujitolea Maisha yake Kama Sadaka kuwatumikia watanzania.

Ameyatoa Maisha yake kama Zawadi kwa Watanzania. Sasa kwanini tusithamini na kutambua Moyo huo wa upendo wa kipekee wa Rais wetu? Kwanini tusibadilishe katiba yetu ili Mama aendelee kuongoza Taifa letu.

Uzuri wa Mama yetu ni kuwa bado yupo imara kimwili na kiakili. Akili yake inachemka Muda wote na hapa unaweza kuona kupitia mipango yake na mambo makubwa aliyoyafanya na anayoendelea kuyafanya hapa Nchini.

Jiulizeni Angela Merkel aliiongoza Ujerumani kwa miaka mingapi.Kumbukeni ya kuwa Ujerumani ndio Taifa lenye uchumi mkubwa sana barani Ulaya. Na ni yeye aliyefanya kazi kubwa ya kuhakikisha kuwa Ujerumani inaendelea kuwa imara kiuchumi.

Sasa kwanini tusimpatie Mama yetu Muda zaidi wa kuongoza Taifa letu ili tufaidi vyema kazi ya mikono yake ? Mnafikiri ni Nchi gani hapa Afrika mashariki na ukanda huu wa kusini Mwa jangwa la Sahara itakayotufikia kiuchumi?

Huyu Hapa Mama wa Shoka Jasiri Muongoza Njia👎
IMG-20250204-WA0073.jpg
IMG-20250204-WA0071.jpg
Screenshot_20240901-150630_1.jpg
Screenshot_20241025-191457_1.jpg


Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Hilo ndo hitaji la wananchi wengi kwa sasa. Inabidi wabunge wafanye kitu pale kwenye katiba ili Mama aendelee kuongoza angalau hadi 2035.
Kwa sasa watanzania wanataka Mama aendelee kuongoza Taifa letu. Maana chini ya uongozi wake wameona mafanikio makubwa yaliyopatikana na namna Maisha ya watanzania yalivyo badilika na kuwa yenye Matumaini makubwa sana .
 
Haraka ya nini wakati bado hajaanza muhula wa pili? Haya ya kubadili katiba anaweza akitaka akae na wapinzani waone watabadilije
 
Back
Top Bottom