Mnaongeleaje wizi wa mafuta sheli, yaani kujaza upepo?

Mnaongeleaje wizi wa mafuta sheli, yaani kujaza upepo?

hawajajipndoa Bali bp iliuzwa kwa puma energy! usitoe taarifa za uongo kama hauna data
Kampuni huwa zinauzwa baada ya kufilisika au kupungukiwa uwezo wa kujiendesha, je ilikuwa hivyo kwa BP?
 
Kwa taarifa yako BP waliuza biashara zake kwa Puma ili kupata pesa ya kulipia FINE kubwa waliopigwa na serikari ya marekani baada ya mabomba yao kupasuka na kuchafua bahari ya eneo la Gulf of Mexico. Na biashara walizo uza ni za nchi nyingi za kusini mwa Afrika, huku wakiiacha Afrika Kusini kama sijakosea.
Ukiendelea kuamini hivi ni sawa lakini ni hatari kwako. Hebu google annual turnover ya BP kuelewa wana mtaji kiasi gani then linganisha kiasi walichotakiwa kufidia Gulf of Mexico na unachosema au kiasi walichopata kwenye hiyo 'biashara' ya tz.
 
Mmmh hichi kituo cha mafuta kinachoitwa shell kipo maeneo gani kwa dar
Shell nao walishafunga biashara zao Tanzania kabla hata kikwete hajaingia madarakani. Ila wabongo ukitaka kuongea kuhusu hivi vituo vya mafuta ili wakuelewe kwa haraka zaidi sema shell utaeleweka ila ukisema sijui petrol station utawaacha njia panda wengi sana.
 
Kuna wizi wa aina nyingi mi naoujua ni huu. Let's say umefika kwa mhudumu ukapaki gari na kumwambia akuwekee mafuta ya 30,000 bila kuangalia kwenye mita yake kabla yako alikuja mtu akaweka mafuta ya 5,000 na haku reset pale kwenye display kwa haraka haraka anaendelea pale alikoishia ya 5,000 na ili usimstukie anakuja kukusemesha ili kukuondolea attention yako kwa hiyo hapo utakuwa ushakamatwa na umewekewa mafuta ya 25000 badala ya 30000. Nishawakamata kama watatu wakifanya hivyo na waliniongezea haki ya yangu
 
Petrol station yoyote ukikuta kuna waudumu wa jinsia ya kiume, wamenyoa mapank fahamu hapo lazima upigwe. Oil com karibu na Airport ni noma, usijaribu usiguse. Pump moja ina waudumu 3!! Na wote wamekaa kiwizi wizi.
 
Hii inaonekana sana.kuna wizi mkubwa sana kwenye mafuta ya sheli apa mjini
Adi inafikia mda mtu unatamani uichome sheli moto
Na pia ni sheli gani hazina wizi huu na nini kifanyike

Karibuni kwa mahojiano mazurmazur

Hii imeshanitokea mara tatu Shell za OIL COM!
Mara ya kwanza ilikuwa OIL COM ya Njia ya Chini kule kawe karibu na Uchumi supermarket,
Mara ya Pili ni OIL COM ya Magomeni ukiwa umetokea njia ya Tandale
Mara ya tatu hii imenitokea Juzi kabisa weeknd hii maeneo ya Mbezi Tank Bovu ukitoka kanisa la KKT kwa mbele ukiwa unaelekea mwenge,Jamaa kaweka upepo kanipa na risiti Gauge haikusoma, Iliniuma sana! Ikabidi nikaweke tena VICTORIA mpaka leo nipo full

I swear ni Bora Gari Izime lakini sitaweka tena Mafuta ktk shell za OIL COM.

**Kama unadhani nawaharibia biashara, subiri yakukute****
 
Kuna wizi wa aina nyingi mi naoujua ni huu. Let's say umefika kwa mhudumu ukapaki gari na kumwambia akuwekee mafuta ya 30,000 bila kuangalia kwenye mita yake kabla yako alikuja mtu akaweka mafuta ya 5,000 na haku reset pale kwenye display kwa haraka haraka anaendelea pale alikoishia ya 5,000 na ili usimstukie anakuja kukusemesha ili kukuondolea attention yako kwa hiyo hapo utakuwa ushakamatwa na umewekewa mafuta ya 25000 badala ya 30000. Nishawakamata kama watatu wakifanya hivyo na waliniongezea haki ya yangu
Thanks
 
Kwa dar es salaam vituo vya ENGEN huwa havina ujanjaujanja kabisa,mafuta yao huwa yanadumu kwa muda mrefu kwenye tank ukilinganisha na mafuta ya kwenye vituo vingine,binafsi sijawahi kuwa na experience mbaya na hawa jamaa,licha ya kwamba vituo vyao ni vichache sana.
 
Hii imeshanitokea mara tatu Shell za OIL COM!
Mara ya kwanza ilikuwa OIL COM ya Njia ya Chini kule kawe karibu na Uchumi supermarket,
Mara ya Pili ni OIL COM ya Magomeni ukiwa umetokea njia ya Tandale
Mara ya tatu hii imenitokea Juzi kabisa weeknd hii maeneo ya Mbezi Tank Bovu ukitoka kanisa la KKT kwa mbele ukiwa unaelekea mwenge,Jamaa kaweka upepo kanipa na risiti Gauge haikusoma, Iliniuma sana! Ikabidi nikaweke tena VICTORIA mpaka leo nipo full

I swear ni Bora Gari Izime lakini sitaweka tena Mafuta ktk shell za OIL COM.

**Kama unadhani nawaharibia biashara, subiri yakukute****
Bila kuwasahau oilcom tabata segerea ni nomaaaa, mi niliweka mafuta ya 20000 nkakiwasha kuelekea kinyerezi ile nafika magereza pale darajani taa ikawaka nlitukana njia nzima
 
Ina maana hawa wahusika hawalijui hili tatizo au ndio kwamba wananufaika, hili tatizo lipo miaka na miaka ila kila nikisikia naambiwa wanadeal na wafanyakazi hewa. .. ambao fedha inayookolewa haizidi robo ya wizi huu wa mafuta
 
Utaratibu ni kujaza fully tank mpk iishe ndio najaza tena, ishu za kuweka vibaba ndio huwezi hata kutrace kituo gani ni poa na gani ni vby.
Dah..kwa ishu ya ujazo wa mafuta kuathirika kwa mabadiliko ya joto ni kama haipo...kwa sababu hesabu za vimiminika hupimwa kwenye nyuzi joto 20 za sentigredi ndiyo maana matenki hufukiwa chini ya ardhi ambako mara nyingi joto huwa kwenye nyuzi joto 20 - 22 za sentigredi...... kwa mfano lita 1000 za mafuta ya petrol huongezeka kiasi cha lita 0.93 kwa kila nyuzi 10 za sentigredi zinavyoongezeka....🙂🙂
 
Siku moja sheli moja ya Oil com hapa hapa Dar, nimeenda kujaza full tank, sasa sijui jamaa hakuwa mjuzi wa kuiba maana hadi tank linajaa mita inasoma lita 87, na nikiangalia gari yangu tank lake mwisho lita 70. Nilimuangalia afu nikamwambia we mwizi, akamind akaja juu akasema hajawahi kuiba toka azaliwe, nikasema niitie manager wako, akasema hayupo. Nikamwita mwenzake na jamaa flani alikuwa anapita nikasema naomba tu-drain mafuta yote kwenye tank afu tuangalie ni lita ngapi yamo pamoja na yaliyokuwamo karibu nusu tank. Nikawaambia kama mafuta yatafika hata lita 80 then nitalipa mara mbili kwa ajili ya usumbufu, jamaa ndo akashtuka ikabidi aanze kuniomba tuyamalize. Nikamkomalia mimi nilikuja na nusu tank, hivo nitalipia nusu tank ambayo ni lita 35 jamaa akawa anaomba kuwa pamoja na kuwa walinipiga lakini mafuta waliyoweka ni zaidi ya hapo, nikakomalia lita 35 kwa kuwa ni muongo na nikalipia hiyo nikachapa lapa. Lakini kiuhalisia taa ya mafuta ilishawaka, niliamua tu kuwakomesha na wao.
 
Hii inaonekana sana.kuna wizi mkubwa sana kwenye mafuta ya sheli apa mjini
Adi inafikia mda mtu unatamani uichome sheli moto
Na pia ni sheli gani hazina wizi huu na nini kifanyike

Karibuni kwa mahojiano mazurmazur
Mkuu hii kitu nimeshuhudia jana, iliniuzi sana lakini nilishindwa la kufanya.Usijaze nusunusu, jaza fulltank ikipungua ongeza kiasi kilichupungua, hautaibiwa.Kwasababu utakuwa unajua matumizi mathalani toka nyumbani hadi ofisini lita ngapi?? na ndizo utakazokuwa unajaza kila siku.
 
Watanzania tuwe na tabia ya kudadisi au kutoa taarifa kwa taasisi husika pale inapotokea jambo ambalo si la kawaida. KAMA sikosei taasisi inayohusika na masuala ya Vipimo ni WAKALA WA VIPIMO. Ukiona unahisi umepunjwa mafuta toa taarifa ofisi ya Wakala wa Vipimo iliyopo karibu yako. Ili kupunguza tatizo kama lipo toeni taarifa kwa wahusika. Kwa DSM ofisi zao zipo Jengo la NSSF Ilala Boma.

Hivi unataka kumaanisha kuwa wao hawajui hili tatizo? Ukweli tatizo hili wanalijua vzr sana maana na wao ni watanzania na wanatumia huduma hizi. Nikwambieni kuwa suala la vipimo na mizani hata kwenye mabucha na masoko tunakonunua vyakula kote tunaibiwa sana na wao wanajua kuwa kuna ttz hili. Mfano tu, nunua nyama kwenye duka la serikali kaipime kwenye mzani wa bucha za mtaani utakuta nyama inazidi uzito. Sbb ni kwamba mizani mingi kama siyo yote huko mtaani na masokoni imechezewa ili mteja aibiwe watu wapate faida zaidi. Suluhisho ni gumu kuliko kutoa taarifa kwa watu wa mizani na vipimo
 
chunga sana wale wanaokwambia SOGEA MBELE hawa wanataka usione ile mita inavyosoma kueni makini nao au mmoja anachukua hela mmoja anakujazia mafuta kuwa makini huyu anayechukuwa hela anakuwa anakuziba au kukufanya usiwe makini na mita ingawa sio wote lakini tahadhari muhimu.
Yeah kweli kabisa unachosema mkuuu, ilishanitokea live bila chenga, wankuelekeza kwenye pump ambako wanapigia upepo nusu mafutaa nusu....
 
Mkuu hii kitu nimeshuhudia jana, iliniuzi sana lakini nilishindwa la kufanya.Usijaze nusunusu, jaza fulltank ikipungua ongeza kiasi kilichupungua, hautaibiwa.Kwasababu utakuwa unajua matumizi mathalani toka nyumbani hadi ofisini lita ngapi?? na ndizo utakazokuwa unajaza kila siku.
Unachosema mkuu ni sahihi kabisa lakini kwa mkuu wa kaya wa sahivi...🙄😡😕😵 na mwendo kasi bila kusahau mnyoosho uliopo kila kona na sekata zote za uchumi/........NI SHIDA bRO
 
Back
Top Bottom