Mnaopakia watoto seat za mbele za gari, tafadhali airbag zinaua

JituMirabaMinne

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2020
Posts
3,381
Reaction score
9,744
View attachment IMG_20210911_114533.jpg

Watu wengi wanaendesha gari za kijapani. Hivyo hiyo sticker huwa inakuwa na maandishi ya kijapani. Lakini kwa gari za wazungu, hiyo sticker inakuwa kwa kiingereza.

Umewekewa tahadhari kwamba kifo au majeraha makubwa yanaweza kutokea.

1. Watoto wa miaka 12 au chini ya hapo wanaweza kuuawa na airbag. Hivyo siyo salama kabisa kuwaweka siti za mbele.

2. Siti za nyuma ndio sehemu salama kwa watoto.

3. Usitumie siti ya mtoto ambayo inaangalia nyuma kwenye siti za mbele. Hizi child seat sijaziona sana huku Tz.

4. Kaa mbali kadri inavyowezekana kutoka kwenye airbag.

5. Penda kutumia Seat belts.

Na kwa kuongezea.

1. Usipende kuweka miguu kwenye dashboard. Kuna siku utageuka kilema in just a second. Airbag ina nguvu sana, ni kama bomu.

2. Usipende kuweka kitu chochote in between wewe na airbag,

Siku njema
 
2923964_IMG_20210911_114533.jpg
 
Sorry wakuu naomba kueleweshwa zaidi, hiyo precaution ni kwa watoto wanokaa mbele na wazee vipi kwa wakubwa kawaida na hata dereva hatari kwao hamna ama? Why watoto tu?, afu hiyo airbag lengo lake hasa la kuwepo wakati ni kitu hatari ni nini? Afu ni ile kama puto ikifunguka siyo?
 
Airbag ipo kwa ajili ya kukupunguzia au kukukinga majeraha au hata kifo wakati ukipata ajali. Ila tu kama utakuwa umefunga mkanda na pia hautakuwa kwenye speed kubwa sana. Japo factor ni nyingi, inategemea na nature ya ajali.

Kwa wazee nashindwa kuzungjmza as sifahamu chochote.

Ila kwa watoto wadogo nadhani sababu kubwa ni kwa sababu mtoto hafiti kwenye ile mikanda ya kawaida ya gari hivyo akipata ajali airbag inaweza kumuua badala ya kumkinga.

Hata kwako wewe mtu mzima airbag siyo salama. Ndio maana nimesisitiza suala la kuweka miguu kwenye dashboard, wadada ndio hasa mna tabia hiyo. Kaa mbali na airbag as you can.

Pia kuvuta sigara huku unaendesha gari ukipata majanga airbag ikadeploy hiyo gari yote itawaka moto as airbag huwa inadeploy kuja maeneo ya usoni na kifuani.

Ngoja nitafuta video za airbag nizipandishe humu uone, huwa inalipuka kama bomu.
 
Unaweza kuangalia hii video. Mara ya kwanza hii video alituonesha Mwalimu wetu class wakati Tunajifunza Crash Investigation.

Its a short video ila pia ni kipande cha movie ya Final Destination.

Mwisho mwa hiyo video kuna dada amesalimika ajali lakini katika kuokolewa bado alikuwa kwenye mazingira hatarishi. Iangalie.

Duh nimeicheki! So hiyo airbag ilivofumuka ndiyo imemsababishia umauti🤔 inaogopesha
 
Airbag ipo kwa ajili ya kukupunguzia au kukukinga majeraha au hata kifo wakati ukipata ajali. Ila tu kama utakuwa umefunga mkanda na pia hautakuwa kwenye speed kubwa sana. Japo factor ni nyingi, inategemea na nature ya ajali.

Kwa wazee nashindwa kuzungjmza as sifahamu chochote.

Ila kwa watoto wadogo nadhani sababu kubwa ni kwa sababu mtoto hafiti kwenye ile mikanda ya kawaida ya gari hivyo akipata ajali airbag inaweza kumuua badala ya kumkinga.

Hata kwako wewe mtu mzima airbag siyo salama. Ndio maana nimesisitiza suala la kuweka miguu kwenye dashboard, wadada ndio hasa mna tabia hiyo. Kaa mbali na airbag as you can.

Pia kuvuta sigara huku unaendesha gari ukipata majanga airbag ikadeploy hiyo gari yote itawaka moto as airbag huwa inadeploy kuja maeneo ya usoni na kifuani.

Ngoja nitafuta video za airbag nizipandishe humu uone, huwa inalipuka kama bomu.
Aisee ahsante mkuu! Kiukweli elimu kama hii ni muhimu sana, mimi sijawahi kufahamu hatari yake, so inakukingaje ni vile ikideploy inakua kama mto so ukipata ajali means hutohit machuma ya mbele eeh?
 
Airbag hasa hizi frontal airbag inakukinga usijibamize kwenye kioo cha mbele unapopata ajali.

Ukipata ajali hasa frontal collision, kama hujafunga mkanda una chance kubwa ya kujibamiza kwenye kioo cha mbele.

Kazi ya mkanda ni kukuzuia ubaki palepale once inapotokea ajali, hivyo airbag ikideploy itakukuta palepale kwenye kiti.

Kusipokuwa na airbag ukipata frontal collision una chance kubwa ya kupata matatizo kwenye shingo as mwili utazuiwa kwenye kiti ila shingo italazimishwa kuja mbele. Unaweza hata kuvunjika shingo.

Ndio maana tunashauri watu kuhakikisha airbag zinafanya kazi vizuri kwenye magari yao. Pia tunasisitiza matumizi ya seat belts.
 
Nitajuaje kama airbag inafanya kazi vizuri ?
Screenshot_20210912-142754~2.jpg
 
Sorry wakuu naomba kueleweshwa zaidi, hiyo precaution ni kwa watoto wanokaa mbele na wazee vipi kwa wakubwa kawaida na hata dereva hatari kwao hamna ama? Why watoto tu?, afu hiyo airbag lengo lake hasa la kuwepo wakati ni kitu hatari ni nini? Afu ni ile kama puto ikifunguka siyo?

Kama unamiliki Gari na unaendesha halafu unauliza maswali haya aibu sana.

Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
 
Mbona mwenye uzi kanijibu vizuri tu mkuu bila kejeli kama wewe?, tunatofautiana uelewa unaweza kuwa unajua kitu fulani na mwingine hajui so busara ni kumuelekeza mtu kwani inakugharimu nini ama unakatika pumbu ukinijibu? Haya similiki gari na siendeshi so did i deserves to ask that question?.. watu wengine bana🤔
 
Mbona mwenye uzi kanijibu vizuri tu mkuu bila kejeli kama wewe?, tunatofautiana uelewa unaweza kuwa unajua kitu fulani na mwingine hajui so busara ni kumuelekeza mtu kwani inakugharimu nini ama unakatika pumbu ukinijibu? Haya similiki gari na siendeshi so did i deserves to ask that question?.. watu wengine bana[emoji848]

Pole sana kwa kuumiza hisia zako sio lengo langu kwa hilo, sababu kuu kusema kama unamiliki Gari au kuendesha halafu hujui hio maana yake. Kwasababu Hio warning ipo juu ya seat ya dereva. Narejea tena kama nimekukera kwa comments yangu ya kwanza samahani sana.

Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
 
Afadhali ya hao, kuna akina mama na Baba junior unamkuta anaendesha huku kampakata junior katikati yake na steering wheel! Hapo unakuta junior kalilia kuendesha. Huwa natamani niwakate makofi sema wengine mbavu nene wanaweza kunigeuzia kibao!
 
Back
Top Bottom