Mnaopekua simu za wapenzi/waume/wake zenu huwa mnataka nini kifuate?

Ni matani tu ya kazini hayo,alichotakiwa kufanya ni kumwuliza tu kwanini huyo mtu anakuita hivyo, kwanini achati nae sasa,itamsaidiaje zaidi yakumfanya apaniki na kujipa misongo ya mawazo bila sababu.
Utani inabidi uzingatie wewe ni nani kwa wakati huo, yaani ni mke au mume wa mtu utani usivuke mipaka. Mimi naamini hata huyo mwanamke angekuta sms ya namna hiyo kwa jamaa ndani pangekuwa pa moto pia, hata wewe ungekuta sidhani kama usingefikiria mengine. Ni bora utani wa hivyo uishie kwenye kuongea tu, sio hadi kwenye kuchat huku unajua huo ni ushahidi endapo mume/mke ataona hamtaelewana na iko wazi kabisa hata kwa akili ya kawaida tu
 
Akina sisi simu ya mtu ikiita hata niulizwe nani huyo anapiga huwa namjibu njoo mwenywe na kama yupo bafuni eti niletee simu namwambia oga wewe mtatafutana ukitoka 😂😂😂

Niliwahi mfuma anafunua yangu eti ngoja niangalie kama kuna mtu atanipa presha ya kushuka 😂😂

Majina yangu mengi ni fundi spare temeke, fundi interior design, engineering 4D33, mchonga bush temeke, fundi rejeta mbagala, fundi tension spring leaf, "aliyepigwa chai Schiphol" 😂 😂😂😂
Mshangazi dot com
 
Ni sawa mkuu,nilichoandika hapo, tatizo liko kwa approach ya mwanaume,why aanze kuchati na dume jenzake,badala yakumuoji mkewe!??,.ni nini hii kama si wivu wa ovyo?
 
Kinachosababisha simu inakaguliwa ni muhusika kuonyesha simu yake ni special. Unafikili wanaokagua wanaanza tu!?Huwa Kuna viashilia vya kimsukumo, ndoa inayovunjika Huwa Ina dalili(keys), anachofanya muhusika ni kutembea na hizo keys,.


Niliwahi kuwa na uhusiano wa namna hiyo, siku niliyoongozwa kukagua simu, ndio siku nilikuwa nimejiandaa kuachana, and I was comfortable for that,


Angalizo tu,kama una amani usikague,ila ukiwa na hisia mbaya ,just kagua, ukikaa kimya utakuja kulishwa ARV bila sababu ya msingi


Bora uteseke miezi kadhaa, kuliko kuumia maisha,
 
Muda mwinginee unaweza ukawa huna idea ya kupekua lakini ukaazima simu yake ufanye mawasiliano labda, mara paaap text inaingia kwa juu pale "mpenzii nimemiss Ile ya Jana" na Wala hujatuma wewe hiyo text lazima utataka kujua zaidi ni nani anayetuma mesejii za hivoooo ndo kukutana na maajabu🥶🥶🥶
 
Ni sawa mkuu,nilichoandika hapo, tatizo liko kwa approach ya mwanaume,why aanze kuchati na dume jenzake,badala yakumuoji mkewe!??,.ni nini hii kama si wivu wa ovyo?
Yeah hapo ilibidi amalizane na mke wake, Nakumbuka kuna staff mwenzetu kipindi ndo kaoa tu ndoa bado changa ilikuwa mke wake akitongozwa tu,jamaa anamfata mwanaume aliyemtongozea mke wake na kuanzisha magomvi.


Jamaa aligombana karibu na kila mwanaume pale mtaani kumbe mke wake ni kicheche balaa anamchora tu. Alipokuja kugundua mke wake ndo chanzo na anagongwa mbaya saizi kapoa hamfatilii tena na kulichopo wanashindana tu mwanaume kaamua nae kuwa kiwembe
 
Hiyo tabia anayo mke wangu. Yani dakika moja ya kupoteza, simu imepekuliwa kila engo. Why kuyatafuta mambo yatakayokuumiza? umekuta mawasilano tata, vipi utavunja ndoa?
wazee wetu hawakutaka shida kabisa, wakiwa wanatoka safari walitanguliza koti au mzigo nyumbani wao wakibaki vijiweni kwa muda. Hii ni kumfanya mke ajiandae, kama alikuwa na makandokando yake ayaondoe ili maisha yaendelee
 
Kwa baadhi ya wasomaji watakua wanajisikia kuvurugigwa ubongo,wakisikia kuwa kuna wazee walikuwa hivyo,wanaona kama walikuwa hamnazo kichwani au limbwata liliwatawala,,kumbe wangejua ilikuwa ni hekima ya hali ya juu na walidumu kwa mda mrefu kwenye ndoa zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…