Mnaopiga wake zenu huwa mnakuwa mmetumia vilevi? Mke hapigwi!

Kazoea shida na hana pa kwenda ukizingatia kwao alipotoka nako hakueleweki lazima awe mpole🤣🤣🤣 umaskini mbaya👌
Si Kweli kuwa Umaskini ndo chanzo Cha wanawake kupigwa na kukosa pa kwenda.

Upendo wa mke ndo humbakiza pale.

Chanzo ni POMBE,

POMBE ipigwe BAN 🙏
 
Mshukuru Mungu. Yakikukuta utapaona tu kupiga na ndio utajua kwann watu hupiga wake zao.

NB
Usipige mwanamke. Mpe hela feki wahuni wakampige mbele ya safari
 
Kuna jamaa amemramba kichwa mke wake mpaka akampopoa Meno ya mbele lakini mwanamke hataki kuondoka kwa msela...
Kuna wanawake wagumu nyiee me nimehudhuria
Sasa aende wapi na mapengo/mwanya wa kufosi ?
 
Siku atakapo nyanduliwa na kidume chengine huko utajua kwanini wanapigwa😂
 
Kazoea shida na hana pa kwenda ukizingatia kwao alipotoka nako hakueleweki lazima awe mpole🤣🤣🤣 umaskini mbaya👌
Watoto wa matajiri wanachezea kichapo na sio kwamba hawana pa kwenda au kwao ni masikini.

Jitahidini kupunguza magubu, wanaume hatupendi kujibishwa jibishwa bila adabu tena mbele hata watoto sometimes, wanawake kuna time mnakua kama watoto akili kisoda, ugomviiiiiiiii..
mwanaume anajikuta tu kasakurushia kibao.
 
Sasa zikipigwa ban si watu wote tutaokoka? HALAFU SASA ILI???!!!

Sent from my HUAWEI NMO-L31 using JamiiForums mobile app
Pombe ndo zimesababisha ulemavu na mateso Kwa mama zetu,

Wengine wameshindwa kupata Elimu Bora sababu ya baba kunywa Pombe.

Pombe zipigwe BAN 🙏
 
Salaam, Shalom,

Ilikuwa yapata kama majira ya saa tatu hivi usiku, tulikuwa tumemaliza kupata chakula Cha usiku, tulikuwa tukijiandaa kufanya Ibada kabla ya kwenda kulala. Wakati huo nilikuwa na umri wa miaka 10.

Tukiwa katika kusubiri kuanza Kwa Ibada, nilisikia kishindo kikubwa, yaani nilisikia mlio mkubwa wa kitu kama ubao ukitua sehemu Fulani, mlio Ule ulitufanya wote kutahamaki kusikilizia Ule mlio na kishindo kile kilitokana na nini,

Baada ya sekunde kadhaa, tulisikia sauti kubwa ya KILIO Cha mwanamke aliyekuwa akilia KILIO Cha uchungu mkubwa, Kwa kuwa mshindo na kelele Ile ya ubao flat uliotua juu ya kitu tusichokijua ulifuatana na sauti ya kulia mwanamke yule, wote tulijua kuwa mwanamke yule ndiye aliyeangukiwa na kitu kile kizito.

Tukiwa katika kuhamaki nini kimetokea, yalisikika maneno ya mwanamke akimlalamikia mumewe kwanini amempiga vile, Mwanaume alisikika akisema nitakuonyesha, Rudi hapa.

Kumbe, Jirani yetu Mhaya, aliyekuwa amemuoa mwanamke wa Kikurya alikuwa akitoa somo la kawaida Kwa mkewe. Nilijiuliza hivi Kweli mwanamke anaweza kupigwa vile na mtu aitwaye mume na maisha yakiendelea?

Mwanamke yule Jirani alikimbilia kwao, na baada ya siku kadhaa ya kuuguza maumivu, alirudi Kwa mumewe na waliendelea na maisha kama kawaida, na vipigo havikukoma ndani ya familia Ile.

Leo Mimi ni mtu mzima, nimeshavuka umri wa Ujana, Bado najiuliza,

Wanaume mnaopiga wake zenu Huwa mnawapiga wapi?

Huwa mnakuwa mmetumia kilevi Gani?

Maana Kwa Utafiti nilioufanya, sijaona sehemu yoyote katika mwili wa mke wangu inayofaa kupigwa.

Kumpiga mke ni kukosa kujiamini, ni kushindwa kuongoza Kwa akili na BUSARA.

Mungu atusaidie.

Karibuni [emoji120]
Je Mimi Sio falsafa zangu kupigawanamke..Ila Kuna wanamke vichomi hawana malezi..anaweza akawa anatembea nje Na akaanza dharau

Kutwa kukukejeli, msosi hapiki...ipo siku utapandwa Na jazba japo umpe adabu
 
Wakati ameyapata hapohapo na walikubaliana watakua mwili mmoja mpaka kifo
Shetani anamhujumu Taasisi ya ndoa kupitia silaha ya POMBE.

Pombe zipigwe BAN 🙏
 
Je Mimi Sio falsafa zangu kupigawanamke..Ila Kuna wanamke vichomi hawana malezi..anaweza akawa anatembea nje Na akaanza dharau

Kutwa kukukejeli, msosi hapiki...ipo siku utapandwa Na jazba japo umpe adabu
Mungu awe kiongozi wa familia.

Ukitaka mkeo asitoke nje ya NDOA, mwonyeshe nini maana ya Uaminifu Kwa vitendo.

Mke hukopi na kupaste Toka Kwa mume.

Pombe zipigwe BAN 🙏
 
Salaam, Shalom,

Ilikuwa yapata kama majira ya saa tatu hivi usiku, tulikuwa tumemaliza kupata chakula Cha usiku, tulikuwa tukijiandaa kufanya Ibada kabla ya kwenda kulala. Wakati huo nilikuwa na umri wa miaka 10.

Tukiwa katika kusubiri kuanza Kwa Ibada, nilisikia kishindo kikubwa, yaani nilisikia mlio mkubwa wa kitu kama ubao ukitua sehemu Fulani, mlio Ule ulitufanya wote kutahamaki kusikilizia Ule mlio na kishindo kile kilitokana na nini,

Baada ya sekunde kadhaa, tulisikia sauti kubwa ya KILIO Cha mwanamke aliyekuwa akilia KILIO Cha uchungu mkubwa, Kwa kuwa mshindo na kelele Ile ya ubao flat uliotua juu ya kitu tusichokijua ulifuatana na sauti ya kulia mwanamke yule, wote tulijua kuwa mwanamke yule ndiye aliyeangukiwa na kitu kile kizito.

Tukiwa katika kuhamaki nini kimetokea, yalisikika maneno ya mwanamke akimlalamikia mumewe kwanini amempiga vile, Mwanaume alisikika akisema nitakuonyesha, Rudi hapa.

Kumbe, Jirani yetu Mhaya, aliyekuwa amemuoa mwanamke wa Kikurya alikuwa akitoa somo la kawaida Kwa mkewe. Nilijiuliza hivi Kweli mwanamke anaweza kupigwa vile na mtu aitwaye mume na maisha yakiendelea?

Mwanamke yule Jirani alikimbilia kwao, na baada ya siku kadhaa ya kuuguza maumivu, alirudi Kwa mumewe na waliendelea na maisha kama kawaida, na vipigo havikukoma ndani ya familia Ile.

Leo Mimi ni mtu mzima, nimeshavuka umri wa Ujana, Bado najiuliza,

Wanaume mnaopiga wake zenu Huwa mnawapiga wapi?

Huwa mnakuwa mmetumia kilevi Gani?

Maana Kwa Utafiti nilioufanya, sijaona sehemu yoyote katika mwili wa mke wangu inayofaa kupigwa.

Kumpiga mke ni kukosa kujiamini, ni kushindwa kuongoza Kwa akili na BUSARA.

Mungu atusaidie.

Karibuni 🙏
Yani hata kabla sijasoma uzi wako, niko hapa
 
Siku atakapo nyanduliwa na kidume chengine huko utajua kwanini wanapigwa😂
Tangu lini kipigo kimezuia mke mwenye TABIA ya UZINZI kuacha UZINZI?

Ukitaka mke asizini, usimfundishe UZINZI Kwa wewe kuwa na vimada na Malaya lukuki.

Mke hujifunza Toka Kwa mume.
 
Yani hata kabla sijasoma uzi wako, niko hapa
Sijaelewa,

Kabla hujasoma Uzi uko hapa,

Fafanua 🤔

Vipi, katika makuzi Yako, umeshihudia baba akimpiga mama sababu ya ulevi?

POMBE ipigwe BAN 🙏
 
Kuna jamaa amemramba kichwa mke wake mpaka akampopoa Meno ya mbele lakini mwanamke hataki kuondoka kwa msela...
Kuna wanawake wagumu nyiee me nimehudhuria
Hana pa kwenda huyo
Mimi ukinipiga tumeagana 😀
 
Hana pa kwenda huyo
Mimi ukinipiga tumeagana 😀
Huna pa kwenda.

Mume ni MMOJA tu, ubavu wako.

Solution ni kumgundua na kumfukuza huyo shetani wa kipigo, amtoke mumeo,

Maisha yaendelee.

Tukifanikiwa kufanikisha Pombe ikapigwa Ban, tutakuwa tumepiga hatua.
 
Wala sio pombe na kama ni pombe nitaondoka alale na hizo pombe kama ndo zinamfurahisha actually napenda mazungumzo tuzozane ila tusipigane sinamuda wa kumfanyia maombi mlevi wapo wagonjwa wanaohitaji maombi
 
Back
Top Bottom