Mnaotaka kuingiza bidhaa nchini kokotoo la TRA ndio hili

Mnaotaka kuingiza bidhaa nchini kokotoo la TRA ndio hili

Mjomba Fujo

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2012
Posts
2,438
Reaction score
6,313
Kwenye tembea tembea zangu mitandaoni nimekutana na kikotozi cha TRA kinachotumiwa kwenye uingizaji wa bidhaa hapa nchini, kwakweli kinatia kichefuchefu na kukatisha tamaa.

Jioneeni wenyewe nisiseme sanaa;

IMG_20230109_020225.jpg
 
Huo Utopolo wa taarifa haukusaidii kitu chochote mlipa kodi, unachotakiwa kujua ni ‘Finance Act’ ya mwaka gani wanatumia.

Kodi ni sheria sio maamuzi ya TRA. Muhimu ni kuilewa sheria husika TRA wanayotumia kutoza hizo kodi wao ni administrators tu wa kukusanya kodi kupitia sheria husika.

Sio mara zote administrators wa sheria wanakuwa sahihi, kwanini TRA wanapata shida kuelezea sheria husika, matters of fact ukijua sheria husika hata hesabu za kodi unazopigiwa unaweza challenge.
Hilo jambo sio sahihi kwa mlipa kodi, jukumu la TRA ni kutoa elimu ya kodi pia.

Ukizingatia wao sio wanaoamua viwango vya kodi, bali waziri wa fedha ni vyema walipa kodi watambue hizo sheria kujiridhisha what the law intended.

Tangazo la ovyo mno ambalo halina sheria, basically you are at their mercy,
 
Yaan kwa tafsiri hii
[emoji117]mzigo ukifika TU bandarini unapigwa V.A.T
[emoji117]Mzigo ukiingia K'koo,wholesaler anapigwa V.A.T
[emoji117]Mzigo ukiingia mtaani,retailer anapigwa V.A.T
Yaan nchi hii, Mungu atunusuru[emoji26]
 
Watu wanaojiita wasomi wanafanya wrong calculation, ovyo sana, yaani yani mtu ananunua nguo million arobain, Kodi inakuwa na gharama ya zaidi ya 51% , 40m + 26m, =66m, ongeza na faida ambayo mteja anahitaji Ili asongeshe maisha 15m, kwa hiyo 66+15= 81m.

Ndo hapo Sasa ukiangalia mzigo wa laptop Alibaba 1@ $500, ukija bongo mzigo huo huo 1@$1000
 
Mimi nikiangaliaga tu ushuru wa gari tena lililotumika nabaki kushangaa tu sijui tunaishi dunia ipi? Kuna kipindi tulikuwa nje ya nchi tukifanya kazi na mrundi alìkua akishangaa sana akisikia ushuru wa gari kwetu. Akituambia kwao kuingiza gari si issue kabisa...gharama ni kuinunua na kusafirisha tu lakini kuitoa wala alikuwa hawazii tax(Burundi)
 
Yaan kwa tafsiri hii
[emoji117]mzigo ukifika TU bandarini unapigwa V.A.T
[emoji117]Mzigo ukiingia K'koo,wholesaler anapigwa V.A.T
[emoji117]Mzigo ukiingia mtaani,retailer anapigwa V.A.T
Yaan nchi hii, Mungu atunusuru[emoji26]
It’s not supposed to work that way.

V.A.T kama ni mfanyabiashara unaweza idai huko unapo nunua. Kwa sababu uwezi lipa VAT nchi yeyote kama uishi huko kuna namna za kurudishiwa.

Kama importer halafu ni registered trade uwezi kudaiwa VAT at point of entry, ila utaitoza kwenye biashara wakati unauza and everyone on the value chain can claim it back mpaka kwa yule ambae anauza kwa final consumer ndio anaetakiwa kui-charge.

Technically ata mtu anae nini bidhaa Kariakoo kwa lengo la kusafirisha kuna mawili anaweza nunua bila ya VAT au akilipia basi anatakiwa aidai mpakani.

Kama ni trader wa ndani ukinunua bidhaa kwa lengo la kuuza, VAT uliyipia unatakiwa udai TRA wakurudishie the way it works in accounting unakuwa na VAT ledger.

However If the import is for personal use lazima kuna amount unaruhusiwa.

Ni hivi hakuna sheria ya kodi iliyo ya ovyo kama TRA wanavyodai, it’s so generic ilihali kodi azidaiwi ivyo.

Muhimu ni kujua sheria gani wanatumia kuonea watu; hakuna kitu kama icho kwenye sheria the way TRA works.

Hire qualified accountants kama biashara yako inafaida za kutosha. TRA sio alpha and omega wa kodi bali sheria.
 
Cheki sasa watanzania mtu unawapa elimu ya bure hata Shukran hawana.

Halafu kesho wanatandikwa.

Ama kweli kuna watu awabebeki

Haya goodluck if you think VAT is supposed to be carried over without being claimed.

Tatizo lenu kubwa ni ignorance

👋
 
Huo Utopolo wa taarifa aukusaidii kitu chochote mlipa kodi, unachotakiwa kujua ni ‘Finance Act’ ya mwaka gani wanatumia

Kodi ni sheria sio maamuzi ya TRA. Muhimu ni kuilewa sheria husika TRA wanayotumia kutoza hizo kodi wao ni administrators tu wa kukusanya kodi kupitia sheria husika.

Sio mara zote administrators wa sheria wanakuwa sahihi, kwanini TRA wanapata shida kuelezea sheria husika, matters of fact ukijua sheria husika ata hesabu za kodi unazopigiwa unaweza challenge.
Hilo jambo sio sahihi kwa mlipa kodi, jukumu la TRA nikutoa elimu ya kodi pia.

Ukizingatia wao sio wanaoamua viwango vya kodi, bali waziri wa fedha ni vyema walipa kodi watambue hizo sheria kujiridhisha what the law intended.

Tangazo la ovyo mno ambalo halina sheria, basically you are at their mercy,
Umeongea mengi ila hujatusaidia! Jaribu kuwa problem solver siyo problem creator
 
Yaan kwa tafsiri hii
emoji117.png
mzigo ukifika TU bandarini unapigwa V.A.T
emoji117.png
Mzigo ukiingia K'koo,wholesaler anapigwa V.A.T
emoji117.png
Mzigo ukiingia mtaani,retailer anapigwa V.A.T
Yaan nchi hii, Mungu atunusuru
emoji26.png
inamaana mzigo ukifika bandarini unapigwa VAT, Ukiingia kkoo whole saler anapigwa VAT kwenye faida yake tu nyingine anaweza kuiclaim, na mzigo Ukiingia mtaani retailer naye anapigwa VAT kwenye faida yake tu... nyingine anaweza pia kuiclaim
mwisho anayetakiwa kulipa VAT zote ni Mtumiaji wa Mwisho
 
Back
Top Bottom