Mkuu una elewa nini kuhusu hiyo TAX BASE??
Mbona Serikali ametanua sana hiyo BASE mpaka tumeingia kwenye huduma za VING'AMUZI, MIAMALA YA SIMU NK.
Au ww hii tax base unaelewa nini?
Serikali inatakiwa kupunguza kodi, ili kuruhusu watu wengi walipe kwa hiyari, sambamba na kuweka sheria kali kwa wataokwepa kodi ikiwemo kifungo cha miaka si chini ya 10 au kutaifishwa mali.
Serikali imejitahisi mno hapo kwenye TAX BASE, au unataka nini kingine kitozwe kodi mkuu.
Mm binafsi nashauri wapunguze % ya kodi, na pia iangalie uwezekano kwa taasisi ambazo kimsingi zinakusanya NON TAX REVENUE kama, TPA, EWURA, BRELA nk waangalie namna ya kuviunganisha kwenye malipo ili kuondoa ukiritimba.
Mimi kama ningekuwa Waziri wa Fedha ningefanya yafuatayo.
1. Ningetoa GRACE PERIOD kwa makampuni mapya kwa miaka 3 kwenye CORPORATE TAX huku nikikazia sana kwenye PAYE, SDL, VAT ambazo hizi ndio zinarun NCHI. Yaan unahakikisha uhakiki wa wafanyakazi.
2. Personal Income tax ningeshusha kwa 50% na mashine ya EFD ni lazima, na kila biashara mpya anapewa Mashine mpya ya EFD au mfumo wa VFD. Na hapa naweke Sheria kali, kutotoa Risiti, Kifungo kisichopungua miaka 5 au kutaifishwa mali.
3. PAYE ningeshusha % kidogo.
4. Ushuru wa magari na bidhaa mbalimbali ningeshusha hadi kufikia 20 au 15%
5. BOT ingecontrol biashara ya madini, DHAHABU nk. Tuwe na akiba kubwa ya madini hayo, madini hayaozi na always yanapanda thamani.
Nitaendelea nikitoka hapa WAVUVI KEMPU......