Mnaotongoza msichana siku ya kwanza tu mnawezaje?

Mnaotongoza msichana siku ya kwanza tu mnawezaje?

Habarini wana jamvi,
Nimeona hii niulize kwenu na nitatumia mfano mmoja ulionikuta.

Kwanza kabisa kipindi sijao, enzi hizo nina ubrothermen mwingi sana siku hizi nishazeeka japo under 40, nilipita sana na wadada ila nimegundua nilikuwa nachukua Bar, kwenye clubs na sehemu za chakula so it was easy.

Ila sasa tangu nimeoa hali nitofauti siende Bar, clubsna chakula nikila restaurants ni mchana nikiwa kazini. Sasa hapa najikuta nikiwa safarini ndo nafanya timing nazo ni through mitandao tu kama tinder.

Miezi kadhaa iliyopita nikakutana na msichana mrembo sana yaani ile kazi ya kwenda kabisa nikiwa nasubiri daladala maeneo ya Kigamboni, siku ya kwanza ikapita sikusema chochote 😀.

Kesho yake ile natoka getini around saa 12 alfajiri nikakutana naye face to face na yeye anaelekea kazini daah nikaishia kusalimia tu, bahati nzuri kwenye daladala tukakaa seat moja ila nikajifanya kidume nikakaza sikuongea kitu kumbe ndo udomo zege, tukafika ferry dada card ya kuvuka haina hela nikamlipia akashukuru akaenda zake.

Wiki illiyofata yote nikaamua kutoka na gari ili nimpe lift may be tukiwa wawili kwenye gari nitafanya kitu. Aisee ile wiki yote sikukutana naye nikabahatika siku ya moja tu ile nafika stand nimpe lift na yeye hajajua ni mimi akapanda daladala maana nilifika pale na hiace inafika.

Wiki mbili zilizopita ndo mwisho wa kuonana naye tena nlikutana naye ferry tumeshuka tu kwenye pantoni demu alikuwa mbele yangu ile nimuwahi akapanda gari za Tegeta akapata seat ya dirishani na yeye kama aliniona ile nafika pale akanipungia kwa tabasamu zuri na mimi nkachukua zangu bajaji niwahi job Upanga kumbe ndo imetoka hiyo.

UDOMO ZEGE TABU SANAAAAA 🤠🤠
Nafikiri mleta mada alitaka kuzoea maisha tofauti kabisa besides alionayo yeye
 
Taifa hujengwa kuanzia ngazi ya familia,
Sasa kama familia zitavurugika tutakua na taifa la watu wa aina gani?
Mkewe akijua inaweza kupelekea mpaka akadai talaka,huoni kua watoto ndio watakao pata tabu?

Taifa bora hujengwa na familia bora,so familia yake ikivurugika,sio hasara kwake tu bali ni kwa taifa,so kumshauri mtu kama huyu sio mbaya,

The purpose of human life is to serve and to show compassion and the will to help others,the greatness of humanity is not being human,but being humane.
Nakubaliana na wewe asilimia mia moja. Familia bora ndio msingi wa jamii, kuvunjika kwake inayumbisha zaidi watoto kuliko wazazi wenyewe na miaka kadhaa mbele tunapata kizazi ambacho hawaoni umuhimu wa msingi huo.

Wazazi wote, baba na mama wawe watu wenye kujiheshimu kwanza na kuheshimu taasisi waliyokubali wenyewe kuanzisha bila kulazimishwa. Jamaa mtoa mada ameonesha kukosa kujiheshimu na kumheshimu mke wake, anajipalia moto asipokuwa makini.

Na kwa bahati mbaya ndugu zangu 'me wengi wanaangukia hapo, wasahau mazima familia zao. Inaleta ukakasi fulani kila mara kusikia 'me in their prime years, kipindi sasa wanalia kivulini wanakula na wengine. Na inachukuliwa kama kitendo cha 'kawaida' ni hulka ya 'me hata wanyama wapo hivyo. Basi kama ni hivyo hata jike akiwa kwenye 'heat' anakitembeza kila kona mpaka apate alichokusudia atulie. Lakini sisi ni binadamu wenye utashi, sisi sio wanyama.

Unadhani kwa dunia ya sasa kuna 'ke yoyote atakaa avumilie? Bila shaka mtoa mada asingependa binti zake wakutane na vijana wenye tabia ya macho juu juu muda wote
 
Hivi hii kauli ikigeuzwa ikaja kwako utaipokea kweli 😀, kwamba wife acheat aseme anakupenda na kuku heshimu, ni tamaa tu za mwili ?

Something iko wrong kwa hizi marriage
Hapa pazito kwakweli ila tatizo ni ngumu mno kuishi bila kutoka hata mara moja tangu unaoa hadi unazeeka hii sidhani kama kuna mtu anaiweza ila nitajaribu.
 
Umezidi uzembe mkuu, wengine macho yakikutana tu ndio mwanzo wa kujuana na mengineyo yanaanzia hapo.
 
Back
Top Bottom