Mnaotongoza msichana siku ya kwanza tu mnawezaje?

Nafikiri mleta mada alitaka kuzoea maisha tofauti kabisa besides alionayo yeye
 
Nakubaliana na wewe asilimia mia moja. Familia bora ndio msingi wa jamii, kuvunjika kwake inayumbisha zaidi watoto kuliko wazazi wenyewe na miaka kadhaa mbele tunapata kizazi ambacho hawaoni umuhimu wa msingi huo.

Wazazi wote, baba na mama wawe watu wenye kujiheshimu kwanza na kuheshimu taasisi waliyokubali wenyewe kuanzisha bila kulazimishwa. Jamaa mtoa mada ameonesha kukosa kujiheshimu na kumheshimu mke wake, anajipalia moto asipokuwa makini.

Na kwa bahati mbaya ndugu zangu 'me wengi wanaangukia hapo, wasahau mazima familia zao. Inaleta ukakasi fulani kila mara kusikia 'me in their prime years, kipindi sasa wanalia kivulini wanakula na wengine. Na inachukuliwa kama kitendo cha 'kawaida' ni hulka ya 'me hata wanyama wapo hivyo. Basi kama ni hivyo hata jike akiwa kwenye 'heat' anakitembeza kila kona mpaka apate alichokusudia atulie. Lakini sisi ni binadamu wenye utashi, sisi sio wanyama.

Unadhani kwa dunia ya sasa kuna 'ke yoyote atakaa avumilie? Bila shaka mtoa mada asingependa binti zake wakutane na vijana wenye tabia ya macho juu juu muda wote
 
Hivi hii kauli ikigeuzwa ikaja kwako utaipokea kweli πŸ˜€, kwamba wife acheat aseme anakupenda na kuku heshimu, ni tamaa tu za mwili ?

Something iko wrong kwa hizi marriage
Hapa pazito kwakweli ila tatizo ni ngumu mno kuishi bila kutoka hata mara moja tangu unaoa hadi unazeeka hii sidhani kama kuna mtu anaiweza ila nitajaribu.
 
Umezidi uzembe mkuu, wengine macho yakikutana tu ndio mwanzo wa kujuana na mengineyo yanaanzia hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…