Mnaotumia bajaji route za barabara kuu kama Morogoro rd kwa wakazi wa Dar kuweni makini

Mnaotumia bajaji route za barabara kuu kama Morogoro rd kwa wakazi wa Dar kuweni makini

musicarlito

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2020
Posts
591
Reaction score
909
Wasalaam

Vijana wengi wamejiajiri au kuajiriwa katika sekta hii nyeti.Wengi wa vijana hawa hawana weledi wa kutumia vyombo hivi na wengineo kama wana weledi basi ni wahuni

Mara mbili napanda bajaji tunasurika na ajali...gari ziko kwenye mwendo yeye anafosi kuingia

Leo aliingia kwenye lane ya mwendo kasi kwa ghafla,bahati nilikuwa kwenye basi la mwendo kasi...kama dereva wa basi angekua na roho ngumu angewafagia...dereva alichepusha gari kulia tukasababisha ajali nyingine

Mpaka natoka eneo la tukio watu wawili walikuwa chini (bodaboda) na mwingine uvunguni mwa basi nikaacha watu wakihangaika kumtoa

Tuwe makini na babjaji afadhali hata boda boda
 
Hakika, mie bajaji akishafanya foul kusimamia tu nlipomuita naghairi afya yangu ni Bora zaidi
 
Wasalaam

Vijana wengi wamejiajiri au kuajiriwa katika sekta hii nyeti.Wengi wa vijana hawa hawana welding wa kutumia vyombo hivi na wengineo kama wana weledi basi ni wahuni

Mara mbili napanda bajaji tunasurika na ajali...gari ziko kwenye mwendo yeye anafosi kuingia

Leo aliingia kwenye lane ya mwendo kasi kwa ghafla,bahati nilikuwa kwenye basi la mwendo kasi...kama dereva wa basi angekua na roho ngumu angewafagia...dereva alichepusha gari kulia tukasababisha ajali nyingine

Mpaka natoka enjoy la tukio watu wawili walikuwa chini (bodaboda) na mwingine uvunguni mwa basi nikaacha watu wakihangaika kumtoa

Tuwe makini na babjaji afadhali hata boda boda
Ni kama serikali imewaacha wajiamulie watakavyo! Vile vidogo vihuni vihuni vilivyokuwa kwenye boda boda ndo vimehamia huko kwenye bajaji. Yaani uhuni wote unaouona kwenye maboda boda sasa hivi ndo uko kwenye baji, mamlaka zisipochukua hatua mapema soon tutaanza kulia.
 
Ni hatari mkuu
 
3 lanes ya kimara to mbezi unakuta bajaj anakomaa lane juu,kipiston chake ki1 anataka kushindana na piston 4,jn short serikali inabidi itoe darasa namna ya kutumia highway,bajaj na malori zinatakiwa zipite lane ya chini,lane ya kati gari isie na haraka zake,juu huku kuanzia speed 60 na kuendelea
 
Bajaji au boda sio usafiri, usipendelee kupanda, ikitokea una dharura ya lazima kupanda kuwa selective,,,chagua mtu mzima mzima hivi anaejielewa ukimuangalia unasema huyu walau ana majukumu, hata anavyoendesha huko Road anakumbuka nyumban ana mke na watoto wanaomtegemea,,,, Sio hawa vijana wahuni wavuta bangi, walevi wa visungura, mtu hata chumba hana anakaa geto wamechangia watu watano,,,, boda ya mkopo,,, Huyo kwa kifupi maisha yamemchapa,,, hana familia, biashara ama kiwanja, pengine kwao huko mkoani hawajui yuko wapi na anafanya kazi gani ! Mtu wa hivo hana cha kupoteza, akifa poa ,akipona poa,, Anaendesha kama amekata ticket ya akhera!
 
3 lanes ya kimara to mbezi unakuta bajaj anakomaa lane juu,kipiston chake ki1 anataka kushindana na piston 4,jn short serikali inabidi itoe darasa namna ya kutumia highway,bajaj na malori zinatakiwa zipite lane ya chini,lane ya kati gari isie na haraka zake,juu huku kuanzia speed 60 na kuendelea
Kabisa leo hawa jamaa wanaweza kuwa wamesababbisha mauti ya watu
 
Back
Top Bottom