Mnaotumia bidhaa za Apple® Mnapigwa sana. Sijui hata mnavyotoa hela mnafikiriaga nini?

Mimi hata Sumsung nanunua used, ambayo ni almost mpya kwa bei rahisi. Simu mpya hainisaidii chochote, matumizi ni yale yale.
 
Sony hazina kamera kali kushinda iPhone
 
Sio mbaya, ila nachozungumzia iPhone wanatengeneza processor zao wenyewe.
Mkuu Samsung Galaxy S24 (plain), international version inatumia chipset ya Samsung Exynos 2400 na iPhone 15 Pro inatumia Apple A17 Pro. Hii screen shot ya GSMarena wamezitest hizo chipset mbili ya Apple imeshinda kwenye CPU, ya Samsung imeshinda kwenye GPU kwa hiyo hamna bora kuliko mwenzake hapa.

Achilia mbali hivyo, Samsung yuko vizuri kushinda Apple linapokuja suala la ubora wa simu kuanzia hardware hadi software. Software ya Apple sanasana inakupa stability tu. Labda ba security ambayo probably hutoitumia. Ila One UI inakupa stability, features nyingi na endless customization ambayo huwezi pata kwenye Apple, plus Samsung DeX pia ni next level
Achilia mbali Samsung, tuje kwa Mchina. Unaifahamu vivo X100 Ultra? Hii simu iko vizuri kushinda iPhone 15 Pro Max karibia kila idara ila hautaona bei yake ikifika milioni 4
 
Naubaliana na wewe japo kuna sehemu nyingi za ushindanisha hizo processor, sio katika cpu na gpu pekee.
 
Nimechunguza na nimetumia zote, Sony clears.

Na Apple wanatumia Sony's camera sensors for almost a decade now, what are you trying to say??
Sijasema iPhone hazitumii sensor za Sony. Nimesema kamera za Sony (yani za kwenye simu za Sony) hazifikii ubora kamera za iPhone
Sasa kumuuzia mtu sensor ndio kumpita kwenye ubora wa picha ama. Xiaomi 14 Ultra inatumia sensor za Sony pia ila ukifananisha picha hiyo Sony Xperia 1 VI haiingii hata chembe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…