GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, amesema kumekuwa na ongezeko la ajali za bodaboda, hali iliyosababisha ongezeko la wagonjwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), hivyo kuigharimu sekta ya afya.
Amesema jumla ya wagonjwa wa ajali za bodaboda 10 hadi 15 kila siku hufikishwa MOI, huku kwa mwezi idadi ikiwa ni 300 hadi 400.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa Kongamano la Kimataifa la mafunzo la madaktari wa ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu, Waziri Ummy, alisema wagonjwa hao wengi wanafika wamevunjika mifupa ya miguu, ubongo na uti wa mgongo.
"Nimefungua mafunzo lengo ni kuongeza ujuzi, uzoefu na utaalaamu wa wataalamu wa afya na mafunzo yanaendeshwa na wataalmu wa MOI na kimataifa kutoka Marekani, Canada, Australia na nchi nyingine.
"Wamekuja kwa wakati kwa sababu tunashuhudia ongezeko la wagonjwa wa ajali za bodaboda, ambao wanahitaji kufanyiwa upasuaji," alisema.
Imeandaliwa na Aveline Kitomary kutoka HabariLeo_Tanzania.
.........................................
Na Wewe Waziri Ummy Mwalimu (Oddo) hukupaswa kuja Kututangazia kuwa kila Mwezi MOI inapokea Bodaboda 300 bali ulipaswa uje na Mikakati pamoja na Suluhisho la Hatari hii kwani Wengine (akina GENTAMYCINE) tumeshachoka kwenda Misibani na Makaburini Kuwazika hawa Bodaboda na hata Kulazimishwa kuwatolea Rambirambi kutokana na Uzembe wao uliowapelekea kufariki huko.