Uchaguzi 2020 Mnataka haki na usawa, kwanini wanawake mmemtenga Queen Cuthbert Sendiga, Mgombea Urais kupitia ADC?

Uchaguzi 2020 Mnataka haki na usawa, kwanini wanawake mmemtenga Queen Cuthbert Sendiga, Mgombea Urais kupitia ADC?

Sio lazima kumchagua, ila kumuunga mkono Kama mwanamke anadhubutu kuwania nafasi kubwa karibu kuliko zote akiwa na washindani waliomzidi kila kitu na bado amesimama na anaongea kitu kinachoingia akilini pengine kuliko wote hao washindani wake.

Mleta mada amehoji u wapi umoja wa wanawake katika kutetea usawa ambao kila leo wanauimba, Kama wameshindwa kumuunga mkono hata kumpa tu hongera wameshindwa Hilo wanalolidai wanathani watalipata kwa wanaume?

Sent using Jamii Forums mobile app
Umoja wa nini kama hatumpigii kura? Unafiki sio kitu kizuri. Haya mambo ya gender nyie wanaume mnayakuza sana. Na nina amini kama tungeungana kumsapoti huyu huyu mleta mada au wewe ungeleta mada ni jinsi gani wanawake walivyo wapumbavu kumsapoti mgombea asiefaa
 
Naturally mwanamke anaamini yuko salama hatma yake akiikabidhi kwa mwanamme sio mwanamke mwenzie
 
Mbona lawama kwa ccm tu?channel ten ndio inaonesha sana mikutano ya ccm na wote tunajua channel ni ya nani. Hata hivyo mbona huyo Mama wa ADC huwa tunamuona kwenye taarifa za habari hasa ITv.
Miaka mitano walikuwa huru mkuu, hafu Mimi sihangalii tv za bongo kabisa
 
Umoja wa nini kama hatumpigii kura? Unafiki sio kitu kizuri. Haya mambo ya gender nyie wanaume mnayakuza sana. Na nina amini kama tungeungana kumsapoti huyu huyu mleta mada au wewe ungeleta mada ni jinsi gani wanawake walivyo wapumbavu kumsapoti mgombea asiefaa
Vyovyote vile usemavyo wanawake hampendani jua hivyo tuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tangu kampeni zianze yuko Handeni anahutubia watoto wanaocheza mpira
 
Tangu kampeni zianze yuko Handeni anahutubia watoto wanaocheza mpira
Ndio tunawaambia wanawake wajitokeze wakasikilize sera za mwana mama mwenzaobkuonesha sapoti,ila wao ndio kwanza wanasngalia vyama wanaenda kujaa kwenye mikutano ya ccm na chadema.
 
Huko mbeya shida sio tulia ka mwanamke huko mbeya huwa hawaipigii kura CCM so utaona utofauti, mbona kina bulaya na matiko walishinda ubunge tena kwenye mkoa wenye mfumo dume.
 
Kwahiyo wanawake hawaiwezi hiyo nafasi ya urais na ndio maana pamoja na marais wengi wa Marekani ila hakuna rais mwanamke hata mmoja?
Simply Yes, na kwa mtazamo wangu ni ngumu sana kutokea rais wa US mwanamke ndio maana ubao so far unasoma (me 45 v 0 ke). Ile nafasi ni zaidi ya rais wa US.
 
Kuunga mkono siyo lazima umchague, uko wapi ule umoja na usawa mnaoulilia wanawake mpewe?
... sio sahihi eti mtu vile ni mwanamke achaguliwe kwa kigezo Cha ujinsia wake
 
We mpaka Sasa sijaona sera nzuri ya magufuli ndio maana simhesabii kama mwenye sera ingawaje yeye ndie mwenye kushinda lakini wanawake mnafeli sana na hakuna siku itakayotokea hayo muyatakayo yatakuja kuwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Inawezekana tunafeli lkn si kwenye hili. Msitupangie cha kufanya..kila mtu binafsi ana haki ya kuchagua kiongozi anaeona anafaa. Sijaelewa why suala la jinsia limeraise hapa..
Na sisi wanawake tunaojitambua hatutamchagua mwanamke kwasababu ya uanamke wake. Apambane zaidi tuone uwezo wake...hakuna kuwezeshwa kijingajinga. Apambane na siku akionekana atapewa sapoti, kwasasa hata sura hatumjui.
 
Mimi ni mwanaume na nasema kuwa 2015 Mama Anna Mghwila alikuwa bora kuliko Lowassa na Magufuli,sasa nyie kama wanawake ambao ndio mnaolalamika na kukumbana na huu ubaguzi wa kijinsia ndio mnapaswa kuwa mbele katika kuwaunga mkono wanawake wenzenu wenye uwezo.
Binafsi sikuona ubora wake, nilimjua wakati anagombea, huo ubora ningeuona saa ngapi? Waliofahamu ubora wake walimpigia kura.
Ninaamini hata kura hukumpigia ingawa ulimuona bora kipindi hicho.
 
Kwa nini wanawake mnadai haki na usawa wa kijinsia huku mnashindwa kuonyesha umoja kwenye njia mnayoipitia katika kudai usawa na ile nadhalia ya kutaka kupewa nafasi kwenye mabalaza ya maamuzi?

[emoji117] Wanawake wanadai usawa kwenye kila jambo wanaloona wameachwa nyuma, tuzungumzie siasa na uongozi, taasisi na mikusanyiko ya kila aina inayokaa ili kudai nafasi kwenye siasa inafanyika kila siku.

Bahati mbaya au nzuri ni kwamba kupitia sehemu hiyo wao wenyewe wanashindwa kujua hawana ubavu kupata usawa au kuingia kwenye nafasi kubwa pasipo upendeleo au kusukumwa.

Queen Cuthbert Sendiga ni mgombea urais kupitia chama cha alliance for democratic ni mwanamke pekee kati ya wagombea wote wa nafasi ya urais, lakini mpaka sasa hakuna sehemu yoyote inayopiga kelele kama si kampeni kumnadi mama huyu.

Kwa nini tunasema haki wanayodai wanawake siyo ile ya kutoka moyoni, picha tunayoiona kupitia mgombea huyu ndiyo ukweli halisi wa tabia za jinsia hii pendwa.

Nilidhani kupitia mama huyu basi wanawake kama siyo wote wangeonyesha umoja angalau tushangae na kusema kitu, ila mpaka hapa wamekwama.

Mgombea mwenyewe alishasema kama siyo kulalamika kuwa "Wanawake hawana umoja" sasa haifahamiki kama tatizo ni chama au ni nini?

Karibu kwa mjadala.
Subiri october 28 ipite huyo mama baadae Lissu kwanza
 
Kwa nini wanawake mnadai haki na usawa wa kijinsia huku mnashindwa kuonyesha umoja kwenye njia mnayoipitia katika kudai usawa na ile nadhalia ya kutaka kupewa nafasi kwenye mabalaza ya maamuzi?

👉 Wanawake wanadai usawa kwenye kila jambo wanaloona wameachwa nyuma, tuzungumzie siasa na uongozi, taasisi na mikusanyiko ya kila aina inayokaa ili kudai nafasi kwenye siasa inafanyika kila siku.

Bahati mbaya au nzuri ni kwamba kupitia sehemu hiyo wao wenyewe wanashindwa kujua hawana ubavu kupata usawa au kuingia kwenye nafasi kubwa pasipo upendeleo au kusukumwa.

Queen Cuthbert Sendiga ni mgombea urais kupitia chama cha alliance for democratic ni mwanamke pekee kati ya wagombea wote wa nafasi ya urais, lakini mpaka sasa hakuna sehemu yoyote inayopiga kelele kama si kampeni kumnadi mama huyu.

Kwa nini tunasema haki wanayodai wanawake siyo ile ya kutoka moyoni, picha tunayoiona kupitia mgombea huyu ndiyo ukweli halisi wa tabia za jinsia hii pendwa.

Nilidhani kupitia mama huyu basi wanawake kama siyo wote wangeonyesha umoja angalau tushangae na kusema kitu, ila mpaka hapa wamekwama.

Mgombea mwenyewe alishasema kama siyo kulalamika kuwa "Wanawake hawana umoja" sasa haifahamiki kama tatizo ni chama au ni nini?

Karibu kwa mjadala.
HAKI sawa na mambo unayoyazungumza hapa ni vitu viwili tofauti kabisa!
 
Back
Top Bottom