Uchaguzi 2020 Mnataka haki na usawa, kwanini wanawake mmemtenga Queen Cuthbert Sendiga, Mgombea Urais kupitia ADC?

Umoja wa nini kama hatumpigii kura? Unafiki sio kitu kizuri. Haya mambo ya gender nyie wanaume mnayakuza sana. Na nina amini kama tungeungana kumsapoti huyu huyu mleta mada au wewe ungeleta mada ni jinsi gani wanawake walivyo wapumbavu kumsapoti mgombea asiefaa
 
Naturally mwanamke anaamini yuko salama hatma yake akiikabidhi kwa mwanamme sio mwanamke mwenzie
 
Mbona lawama kwa ccm tu?channel ten ndio inaonesha sana mikutano ya ccm na wote tunajua channel ni ya nani. Hata hivyo mbona huyo Mama wa ADC huwa tunamuona kwenye taarifa za habari hasa ITv.
Miaka mitano walikuwa huru mkuu, hafu Mimi sihangalii tv za bongo kabisa
 
Vyovyote vile usemavyo wanawake hampendani jua hivyo tuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tangu kampeni zianze yuko Handeni anahutubia watoto wanaocheza mpira
 
Tangu kampeni zianze yuko Handeni anahutubia watoto wanaocheza mpira
Ndio tunawaambia wanawake wajitokeze wakasikilize sera za mwana mama mwenzaobkuonesha sapoti,ila wao ndio kwanza wanasngalia vyama wanaenda kujaa kwenye mikutano ya ccm na chadema.
 
Huko mbeya shida sio tulia ka mwanamke huko mbeya huwa hawaipigii kura CCM so utaona utofauti, mbona kina bulaya na matiko walishinda ubunge tena kwenye mkoa wenye mfumo dume.
 
Kwahiyo wanawake hawaiwezi hiyo nafasi ya urais na ndio maana pamoja na marais wengi wa Marekani ila hakuna rais mwanamke hata mmoja?
Simply Yes, na kwa mtazamo wangu ni ngumu sana kutokea rais wa US mwanamke ndio maana ubao so far unasoma (me 45 v 0 ke). Ile nafasi ni zaidi ya rais wa US.
 
Kuunga mkono siyo lazima umchague, uko wapi ule umoja na usawa mnaoulilia wanawake mpewe?
... sio sahihi eti mtu vile ni mwanamke achaguliwe kwa kigezo Cha ujinsia wake
 
We mpaka Sasa sijaona sera nzuri ya magufuli ndio maana simhesabii kama mwenye sera ingawaje yeye ndie mwenye kushinda lakini wanawake mnafeli sana na hakuna siku itakayotokea hayo muyatakayo yatakuja kuwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Inawezekana tunafeli lkn si kwenye hili. Msitupangie cha kufanya..kila mtu binafsi ana haki ya kuchagua kiongozi anaeona anafaa. Sijaelewa why suala la jinsia limeraise hapa..
Na sisi wanawake tunaojitambua hatutamchagua mwanamke kwasababu ya uanamke wake. Apambane zaidi tuone uwezo wake...hakuna kuwezeshwa kijingajinga. Apambane na siku akionekana atapewa sapoti, kwasasa hata sura hatumjui.
 
Binafsi sikuona ubora wake, nilimjua wakati anagombea, huo ubora ningeuona saa ngapi? Waliofahamu ubora wake walimpigia kura.
Ninaamini hata kura hukumpigia ingawa ulimuona bora kipindi hicho.
 
Subiri october 28 ipite huyo mama baadae Lissu kwanza
 
HAKI sawa na mambo unayoyazungumza hapa ni vitu viwili tofauti kabisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…