Uchaguzi 2020 Mnataka haki na usawa, kwanini wanawake mmemtenga Queen Cuthbert Sendiga, Mgombea Urais kupitia ADC?

Wameumbwa tuwale kwanini mnataka watutawale?
 
Binafsi sikuona ubora wake, nilimjua wakati anagombea, huo ubora ningeuona saa ngapi? Waliofahamu ubora wake walimpigia kura.
Ninaamini hata kura hukumpigia ingawa ulimuona bora kipindi hicho.
Hata mie nilimjulia kipindi kile anagombea na ndipo nikaona ubora wake hata humu JF amezungumziwa sana tu,ila wagombea kama Magufuli na mwenzie Lowassa hata mdahalo waliukimbia na Lowassa ndio kwenye mikutano yake ya kampeni alikuwa anaongea dk 5 tu ila et hao ndio walionekana bora.
 
Simply Yes, na kwa mtazamo wangu ni ngumu sana kutokea rais wa US mwanamke ndio maana ubao so far unasoma (me 45 v 0 ke). Ile nafasi ni zaidi ya rais wa US.
Tunaona siku wanawake wanafanya kazi ngumu za nguvu na pia za kutumia akili,sasa huo ugumu unaouzungumzia wewe ni upi ambao wanawake hawawezi?
 
Tunaona siku wanawake wanafanya kazi ngumu za nguvu na pia za kutumia akili,sasa huo ugumu unaouzungumzia wewe ni upi ambao wanawake hawawezi?
Mkuu, kwa asili mwanamke is an auxiliary being, kuna majukumu hayamfai kwa kuwa kwa vyovyote vile yatakuwa juu yake.

Mwanamke kuwa rais inawezekana kwa kuwa kunakuwa na mifumo, katiba na mihimili mingine inayo muongoza/mdhibiti lakini when it comes to US mambo ni tofauti.

Rais wa US anakuwa ni kama rais wa 'dunia', anatawala na kufanya maamuzi ya maeneo ambayo hata hayajamchagua na wakati mwingine pasipo 'msaada' wa mifumo wala sheria.
 
Haya
 
Mkipendana nyie wanaume inatosha. Tumeumbwa hivyo hatuwezi kubadilika.
Basi mkubali tu asili ichukue mkondo wake kwamba mwanaume ndie kichwa na ndie anaepaswa kua mbele yenu katika mambo yote, huko kung'a ng'ani usawa ama haki yenu popote pale muachale mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio hujaeleza sasa ugumu upo wapi kwa mwanamke kwa hayo uliyoyaeleza?
 
Basi mkubali tu asili ichukue mkondo wake kwamba mwanaume ndie kichwa na ndie anaepaswa kua mbele yenu katika mambo yote, huko kung'a ng'ani usawa ama haki yenu popote pale muachale mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani wewe una matatizo sio bure. Uliyoyasema hapa hayaendani na mada., Kichwani mwako kumejaa mfume dume tu.
Haki tutaendelea kuzipigania na bahati nzuri tunazipata hatuna wasiwasi...wanawake wengi wapo juu wanaendelea kuelimika na kufunguka akili. Only time will tell.
 
Yaweza kua Niko na matatizo maybe lakini huo ni kwa wako mtazamo.

Mada inasema wazi wakina mama hawajaonyesha kwa dhahiri kile walicho na wanachokipigania kwa muda mrefu Cha kutaka kuoonyesha dunia kwamba na wao wanaweza kuongoza ama kufanya lolote sawa na mwanaume.
Kwa sababu ametokea kwa Mara ya pili mwanamke kuwania nafasi ya juu kabisa ya kiuongozi lakini kwa sababu wazijuazo wao wamekataa kumtambua.

Wamedai hana sera nk nk.

Ok hana sera sawa lakini je kule kuthubutu kuisogelea nafasi hio katikati ya wenye dola na sera Kama wangemuunga mkono au hata kumpongeza je kesho si wangejitokeza wengi tena wenye sera nzuri kwa sababu ya kuungwa mkono na wanawake wenzao?

Wacha tuendelee kua na mfumo dume maana ndio asili itakavyo. Lakini hamtafanikiwa hayo myatakayo, na hapo ulipojinasibu kuwa mmefika hamjafika bure zaidi ya kuwezeshwa na rushwa kwa wanaume ili wawafikise hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sasa mnataka wamuunge mkono kwa kuwa ni mwanamke au kama mgombea urais mwenye ilani ya chama na sera zinazowavutia wanawake, kumbukeni anagombea urais wa nchi sio urais wa wanawake kwahiyo anapimwa kwa vitu vingi ili apate kuungwa mkono na sio jinsi yake tu.
 
HAKI sawa na mambo unayoyazungumza hapa ni vitu viwili tofauti kabisa!
Hujaelewa mada, umesoma haraka haraka au hujui mambo ya women ministry how is working behind but issue hapa siyo haki sawa, hiyo haki sawa ni sehemu ya world agenda to win women's kwa hapa nimeigusia kwa sababu ni sehemu yao katika kudai uungwaji mkono.

KARIBU.
 
HOJA YAKO UMEIVURUGA ULIPOTAKA WANAWAKE KUUNGA MKONO WANAWAKE WENZAO KAMA SEHEMU YA KUFANIKISHA AJENDA YAO YA HAKI SAWA KWA WOTE! SUALA LA KUCHAGUA KIONGOZI (KWA KUMPIGIA KURA) HALIWEZI KUTAZAMWA KATIKA 'HAKI SAWA'! KATIKA VYAMA AU JAMII AU VIKUNDI MBALIMBALI, HILO LINAWEZA KUWEZESHWA KUPITIA MAPENDEKEZO TU LAKINI SIO KWENYE UPIGAJI KURA!
 
Narudia, hoja yangu haipo kwenye HAKI SAWA no, endelea kusoma uelewe mkuu.
 
Hongera Queen Sendiga kuteuliwa RC.
Pasco
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…