Mnataka kumbebesha Hayati Magufuli madhambi yenu?

Nisha wahi kuandika humu mara kadhaa,kwamba kitendo cha watu kumuona JPM kama mkosaji mkuu na kumuacha huyu mama,inahitajika uwe mwendawazimu wa akili na kujitoa ufahamu.

Kipindi yote yanatokea huyu mama alikuwa sehemu ya mfumo wa maamuzi,lakini leo hii watu wanajivika miwani ya mbao kujifanya hawaoni,wakati ukweli uko dhahiri kabisa.Leo hii hata matatizo madogo lawama anapewa JPM.

Sikumkubali JPM kwa baadhi ya vitu,lakini ukweli utabaki pale pale siku zote.
 
Jakaya Kikwete anautumia mpira wa miguu kwa nia ya kuikomoa Simba na kuipaisha Yanga. Hayati JPM alikuwa ikulu pale kwa miaka mitano na miezi kadhaa hata siku moja hakuutumia usimba wake kutaka kuionea Yanga.

Awe mwangalifu na apunguze ujuaji wake unaweza kabisa kuiharibia CCM ikapotezwa rasmi kuanzia mwaka 2025.

Nyerere alimkwaza Mwinyi kwa sababu ya upole wake lakini akakoromewa na Mkapa akaishia kulalamikia pembeni katika maongezi yasiyo rasmi.

Mkapa hakumuingilia kabisa JK akamuacha afanye kazi atakavyo kwa miaka yote 10. JK akakoromewa na JPM alipotaka kumletea ujuaji na tabia yake ya kupenda kuzunguka watu.

JK ana sauti sana mbele ya Samia, na Samia hana uwezo wa kuupinga ushawishi wa JK akiwa ndiye bosi wake wa zamani aliyemtoa Unguja na kumpandisha katika majukwaa yaliyompa kuonekana kila mahali.

Samia kukosa sauti ni mbaya kwake kwani kiongozi mwenye maono huwa anajua anatoka wapi yupo wapi na anakwenda wapi. Asipoangalia anaweza kuwa Rais wa mwisho wa CCM na JK wala haonekani kushtushwa na uhalisia wa maisha ya sasa, yeye anaendeleza hulka zile zile za ujuaji na dharau kwa masuala yaliyo nyeti kwa taifa.

Kero haswa ni kwa sisi watu wa mpira anafanya mambo ya kijinga akijificha nyuma ya GSM, Injinia Hersi na viongozi wengine wa Yanga. Huwezi kutaka kuwapa Power Dynamos milioni zaidi ya 100 ili eti waifunge Simba na isiingie katika hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa, kama kweli wewe ni mzalendo wa nchi yako!.

Anatengeneza mazingira ya watu wa mpira kuichukia kwa ujumla CCM na atampa wakati mgumu sana SSH haswa mwakani.

Mambo ya kipuuzi kama haya yana mwisho mbaya sana kwa hatima nzima ya urais wa SSH na CCM atakayokuwa pengine ndiye mgombea mpeperusha bendera.
 
Mleta mada anataka haya ya uchaguzi wa mwaka 2020 tuyafumbie macho:

VIDEO hii hapa chini imetunza kumbukumbu vizuri ya kilichojiri mwaka 2020

Your browser is not able to display this video.
 
Juhudi zisizo zaa matunda hukatisha tamaa,Vyama vya upinzani hupitia nyakati ngumu sana,kiasi kwamba mwisho watu hufanya maamuzi magumu ya kuunga juhudi,maana zawadi ya uhai ni mara moja tu.

Chaguzi nyingi wapinzani wamepitia katika kaa la moto,hakuna cha the state Wala nani anae oneshwa na kukerwa na mabaya ya chama tawala juu ya wapinzani,kwa sababu nao ni wanufaika wa huu mfumo wa hovyo.

Kitendo cha katiba kulinda maslahi ya viongozi na sio wananchi maana yake ni kwamba the state haina meno ya kusimamia maslahi ya nchi bali kundi la wachache nao wakiwemo,sasa kwanini iwe noma kwa wengine kuunga juhudi ili nao wanufaike na mfumo ?

Kazi zao hazionekani sababu hawana maana,Na uwepo wao ni kulinda maslahi yao na wenye nguvu.maana haiwezekani taifa linapita katika nyakati ngumu toka uhuru na malalamiko ni yale yale na mwisho lawama wanapewa wapinzani kwamba ndo wanachelewesha mabadiliko hapana.
 
Wapuuzi ktk ubora wao.
 
..kama kuna madaraja ya uhalifu wa kisiasa Magufuli na genge lake wako daraja la juu kuwazidi wenzao.

..kwa mfano, shambulizi dhidi ya Tundu Lissu, unaanzaje kumtetea Magufuli kwa ushenzi wa kiwango kile?
Hakuna mtu amewahi kuwindwa na serikali na ikamshindwa,ni wapumbavu tu wanao weza kuamini lissu alipigwa risasi kwa maelekezo ya serikali.
 
Hakuna mtu amewahi kuwindwa na serikali na ikamshindwa,ni wapumbavu tu wanao weza kuamini lissu alipigwa risasi kwa maelekezo ya serikali.
Unaijua story ya Ulimboka
Mbona hakukuwa na mafanikio?
Some hitmen are incompetent...so to say
 
Hakuna mtumishi yeyote yule wa umma au taasisi yoyote ile inayoweza kumpangia Rais cha kufanya chini ya katiba hii.
 
Umesahau Zanzibar 2000, 2005 na 2015
 
Ilitokea wakati wa uchaguzi, siku ya uchaguzi? Kwenye kampeni? Nani alimwaga damu kuelekea uchaguzi wa 2020? Ndiyo hoja iliyowekwa mezani.
Kwa maoni yangu, ni wazi kuwa unauliza maswali ya kijinga sana kwa level ya ufahamu wako..

Uchaguzi ni process. Haijalishi tukio baya au zuri limetokea kipindi kipi; kabla, wakati wa uchaguzi au baada ya uchaguzi..

Swali lako la kejeli linapaswa kuwa; Nani alikuwa Rais katika vipindi vyote hivyo vya uchaguzi vya baada, wakati wa kura na baada ya uchaguzi wa 2020?

Na jibu lako ni: John P. Magufuli..!!

Sasa tuambie unataka kujua nini kingine?
 
..kama kuna madaraja ya uhalifu wa kisiasa Magufuli na genge lake wako daraja la juu kuwazidi wenzao.

..kwa mfano, shambulizi dhidi ya Tundu Lissu, unaanzaje kumtetea Magufuli kwa ushenzi wa kiwango kile?
Vipi lile bomu lililoua watu 5 pale soweto arusha kwenye mkutano wa machadema alikuwa jpm yule?

Mwangosi kule Nyororo iringa alikuwa jpm yule?

Uzuri ccm wakiona hivi wanafurahi sana na 2025 watawatia madole tena.
 
Sawa. Kiasi nimekuelewa. Ingawa common wisdom inaniambia hakuna mtu mwenye utendaji bora anayebana vyombo vya habari visiandike habari za kazi zake kiasi cha kutesa na kotowesha baadhi yao.

Kwangu mimi huu mjadala wa kuangalia nani alikuwa nafuu kwa hawa viongozi wa CCM hauna maana. Hakuna cha kutetea wala kusifu. Magufuli was no better than the others. Wote walikua mafisadi, wavuruga chaguzi na wapinzani wa demokrasia na utawala bora.
 
Kama akili yako iko sawa usingeandika huo utumbo. Kwa taarifa yako huyu Samia akiwa VP hakuwa na nguvu yoyote kwenye utawala wa Magufuli. Kwanza mara 3 hivi alikwisha tamani kujiuzulu akazuiwa na Mzee wa Msoga.
 
Whether one agrees or not it's clear that Magufuli's mindset displayed animosity towards certain groups or individuals. This is evident in his actions and statements, which were divisive and often targeted particular communities or political opponents.

It's evident that there's a stark contrast between Magufuli's leadership style and the perception of Samia's approach. Many appreciate Samia for her more inclusive and less divisive approach, which stands in contrast to Magufuli's tendencies towards animosity. If her leadership continues to resonate positively with the people it's understandable why there might be support for her to serve a second term
 
Unajitoa ufahamu kwa
K
 
Hakuna mtu amewahi kuwindwa na serikali na ikamshindwa,ni wapumbavu tu wanao weza kuamini lissu alipigwa risasi kwa maelekezo ya serikali.

..sio kweli.

..serikali ni watu sio MUNGU, hivyo kuna wakati hukosea.

..kuna watu wamesalimikia kwenye shambulizi la bomu la Nyuklia kwa hiyo sio jambo la kushangaza Lissu kusalimika shambulizi la genge la
Vipi lile bomu lililoua watu 5 pale soweto arusha kwenye mkutano wa machadema alikuwa jpm yule?

Mwangosi kule Nyororo iringa alikuwa jpm yule?

Uzuri ccm wakiona hivi wanafurahi sana na 2025 watawatia madole tena.

..ndio maana tunamsihi Rais Samia atende haki kwa kuunda Tume ya Ukweli, Haki, na Usuluhishi, ili waliodhulumiwa wajitokeze na maovu waliyotendewa yajulikane.

..tunaposema uovu wa Magufuli hatumaanishi kwamba ndiye mtawala pekee aliyotendewa uovu ktk nchi yetu.
 
Unaijua story ya Ulimboka
Mbona hakukuwa na mafanikio?
Some hitmen are incompetent...so to say

..wakati mwingine mtu anasalimika kwa bahati yake tu.

..Fidel Castro ali'survive 7 assasination attempts za CIA.

..kuna watu wamesalimika kwenye ajali za ndege, wakati inaaminika ndege ikianguka hakuna anayesalimika.

..na ukiangalia tukio la Lissu utaona kwamba his chances of surviving zilikuwa ndogo sana sana, lakini baada ya operations 20+ amesalimika.
 
Kama akili yako iko sawa usingeandika huo utumbo. Kwa taarifa yako huyu Samia akiwa VP hakuwa na nguvu yoyote kwenye utawala wa Magufuli. Kwanza mara 3 hivi alikwisha tamani kujiuzulu akazuiwa na Mzee wa Msoga.
Kumbe unajua..mtu aliyeamua kujiuzulu huwa kuna mtu anaweza mzuia akakubali km hakuna linalowaunganisha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…