Hakika leo umeandika jambo kubwa na linaumiza sana!!
Eti kabla ya 2015 Kinana na CHAWA wake Zitto wanataka kutuaminisha kwamba uchaguzi ulikuwa huru na wa Haki!!
Wakati mwingine najiuliza hawa wahuni wanaoitafuna nchi usiku na mchana ni kweli wanaweza kutengeneza mifumo mizuri ili wengine waweze kutawala? Jibu ni kwamba HAPANA
KOSA kubwa la Magufuli labda tuseme ninkukataa kuwasikiliza hawa wezi!!
Nani asiyeujua ufisadi wa Kinana na genge lake!? Nani asiyeujua ufisadi na udalali wa Januari na wahuni wenzake? Januari katoa wapi pesa za kuhonga gari ya Milioni 500 baada tu ya Magufuli kufa?
Mzee Mwanakijiji Leo umenena jambo zito sana!!
Mwisho niwatahadhalishe vyama vya siasa kwamba, Kinana ni yule yule, JK ni yule yule, Mbowe ni yule yule, Januari na Rostam ni wale wale..... Hawa wote HAWAJASHIBA hata wakuandalieni uchaguzi huru na wa Haki.
Hawa wazalendo wameuza Bandari, wameuza Mbuga zetu, wanahujumu mradi wa Umeme n.k.!!! Tuendelee kuwapigia makofi ili watuuze na sisi