•itel kiswaswadu
•Tecno kiswaswadu
•bontel kiswaswadu
•O king kiswaswadu
Na misimu yote ya kichina isiyofahamika ndio wazazi wetu wanatumia tena huku tukijinadi ooh mimi mzazi wangu yupo fresh kumbe dakika mbili tu simu yake chaji imeisha na hapatikani hewani
Kuna vile viswaswadu fulani vya Nokia vya mwanzo mwanzo vile. Miaka karibia 10 kinapiga kazi bila tatizo na kinakaa na chaji balaa. Mpaka ukimpa simu nyingine mama alikuwa anakataa kuwa yeye ni kale ka simu kake tu. Alipofariki alimpa binti yake (dada yangu) na mpaka leo kipo hewani kinapiga kazi; na namba bado ni ile ile.
Na mimi huku mjini nadunda na iTel yangu bila wasiwasi. Hata sioni tatizo liko wapi mleta mada 😁