Mnavyosema kuwa Mama Samia kakopa sana, oneni hii ripoti ya IMF

Misri wanakopa sana ila mikopo yao inaendana na maendeleo
Vipi Tanzania pesa tunazokopa zinaendana na maendeleo? Zaidi zinafikia mifukoni mwa Mafisadi

Hii nchi ina kirusi kibaya kinaitwa Chawa..!
Nabii hakubaliki kwao
 
Kweli mkuu upuuz upo Sana ila hatuna Mikopo Kama majirani
Tatizo umebase kwenye takwimu za imf ambazo ukute asilimia ya mikopo tunayochukua inachangia asilimia 10 au 20 kwenye mikopo yote kwa ujumla
 
Horodha???
 
Watanzania tunapaswa tujiulize, Nchi kama hii iliyojaliwa ardhi yenye rutuba,Madini,Maziwa,Bahari na Mbuga za Wanyama za kutosha.Tuanze kupigia upatu suala la kukopakopa Jamani hebu tumuogope Mungu jamani.
 
Hapa tungelitafakari hatima ya Taifa letu kiuchumi,siyo mikopo kausha damu kama hiyo.Tungeliangalia kwanza hizo raslimali zetu zinatija gani katika ukuzaji wa uchumi wetu,Watu wake wananufaika vipi na raslimali hizo.Makusanyo la pato la ndani yakoje Kila mwaka wa bajeti unapofika,usmamizi wake ukoje,Uongozi uliopo unafaa katika utekelezaji wake,ama haufai?Hapo Sasa ndipo upembuzi yakinifu ungelipewa nafasi ya kutathmini ubora naudhaifu wa Serikali ya Mapinduzi.
 
Unasomaga report za CAG?
 
Watanzania tunapaswa tujiulize, Nchi kama hii iliyojaliwa ardhi yenye rutuba,Madini,Maziwa,Bahari na Mbuga za Wanyama za kutosha.Tuanze kupigia upatu suala la kukopakopa Jamani hebu tumuogope Mungu jamani.
Acha upuuz wewe kwahyo unadhani ukiwa na mabonde na milima ndio nn ,pesa zinatakiqa kuekeza katk rasilimali hzo siyo blaha blaha ,,kopa upate maendeleo yako ,Kama unajisifia ukopagi Basi wee n maskini
 
Uandishi gani huu, hata binti yangu wa std 7 hawezi kuandika hivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…